Bwana
salmin siraj Mimi napingana na wewe. Serikali imefanya mengi tu kwenye sekta ya kilimo na ufugaji. Miradi ya ASDP ipo tangu miaka ya 2008 kuwaelimisha kilimo na ufugaji wa kibiashara. SAGCOT, MIVARF yote imekuja miaka takribani 10 iliyopita. Kuna mabwana mifugo kila halmashauri mpaka kwenye majiji. Kuna kata Zina bwana/bibi mifugo. Ulitaka serikali ifanye nini la ziada?
Tangu enzi na enzi (ukiacha mwaka Jana 2021) huwa Kuna maonesho ya nanenane, unajua lengo lake ni Nini??
Pale kuna wakulima wakubwa na wadogo, wafugaji wakubwa mpaka ranch, Kuna vyuo vya kilimo na ufugaji, Kuna VETA/SIDO. Pale unakuta mbegu Bora za ng'ombe, mbuzi, kondoo, kanga, Bata, hata malisho. Shamba la mifugo la Mafinga wanazalisha mbegu za nyasi nzuri kwa ajili ya malisho, uliwahi kuzitafuta ukakosa?
Mfugaji gani anazitafuta elimu anaikosa?
Mimi mwenyewe nimewahi kwenda kuonesha ufugaji wa Bata bukini pale John Mwakangale Uyole nikanunua na mbegu za lucina.
Swali ni je Hawa wafugaji wanahudhuria sehemu kama hizi?
Wafugaji wanawekeza kwenye elimu?
Acheni Lawama za kipuuzi. Ngozi nyeusi wengi hatuzingatii maarifa na technology. Tunafanya ili mradi. Hata umwelimishe vipi anarudia Mambo yake vilevile. Unless soko limwekee masharti ndipo atalazimika kuyafuata mfano kwenye tumbaku na Parachichi.