Nini hufanya thamani ye fedha ishuke au kupanda

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Habarini wana JF, naomba kujua kutoka kwenu wataalamu wa uchumi ni nini kinasababisha fedha ya nchi kushuka thamani? Pia naomba kufahamishwa ni sababu zipi zimepelekea kushuka thamani kwa fedha ya Tanzania (Shilingi). Je uwepo wa fedha nyingi za bandia unaweza kuchangia kushusha thamani ya Fedha? Kuna uhusiano wowote wa thamani ya fedha na maendeleo ya nchi?
 
Moja ya sababu ni kwamba hatuuzi sana bidhaa nje ya nchi bali tunanunua sana toka nje ya nchi.
 
Ni kitu gani kinafanya thamani ya fedha ya nchi fulani itofautiane na nchi nyingine na unakuta labda 1usd=1678tshs saa saba mchana lakini jioni 1usd=1655?
 
Supply and Demand for Tanzanian Shilling. Hii ndio sababu kuu.

Kama Demand ya Tsh ni kubwa thamani yake itapanda also the viceversa is also true.

Kuna sababu nyingine pia

- Food Inflation
- Economic Performance
- Interest Rate
 
kwahivo kwakua demand ya tsh haiwezi kukua this means value of money will be a determinant factor for the growth of economy?
 
kwahivo kwakua demand ya tsh haiwezi kukua this means value of money will be a determinant factor for the growth of economy?

Kifupi ni hivi,

Unaweza kufanya vingi ukiwa na dola than Tsh...

So dola itaendelea kuwa juu zaidi ya Tsh...

Ni kama sun LG bodaboda na Suzuki vitara gari, unatakiwa inipe bodaboa kama kumi ili nikupe gari tajwa.

Floating of currency inaathiriwa zidi na demand ya particular currencies.
 
Kifupi ni hivi,

Unaweza kufanya vingi ukiwa na dola than Tsh...

Floating of currency inaathiriwa zidi na demand ya particular currencies.
kama faranga ya rwanda ipo juu ya tsh, ni vitu gani vya ziada unaweza fanya na faranga ushindwe kufanya kwa tsh.
 
kama faranga ya rwanda ipo juu ya tsh, ni vitu gani vya ziada unaweza fanya na faranga ushindwe kufanya kwa tsh.

Tuanzie hapo,

Ipo juu kivipi?, in terms of nominal value or Real value?.

Kama ni Nominal value hiyo inaweza ikawa kwa sababu za evaluation ya currency yao
against yetu au devaluation ya currency yetu dhidi ya yakwao.

Devaluation ni kitendo cha hiyari kinachofanywa na serikali mahsusi kwa ajili ya kuboost exportation volume

ambapo tanzania inaongoza kwa mazao ya kilimo.

Hela yetu inapokua chini muda mwingine inasaidia ku incourage export na ku discourage imports.

Incase ya real value of money ya Rwanda kuwa juu zaidi ya TZ hiyo sina uhakika.
 


rwanda franc = tsh 2.4610
http://www.exchange-rates.org
 
kama faranga ya rwanda ipo juu ya tsh, ni vitu gani vya ziada unaweza fanya na faranga ushindwe kufanya kwa tsh.

Hapa kuna kitu kinaitwa devaluation na hii ni kwasababu ya kupromote exports sana. China na Japan ni mabingwa wa kufanya hii kitu
 
Hapa kuna kitu kinaitwa devaluation na hii ni kwasababu ya kupromote exports sana. China na Japan ni mabingwa wa kufanya hii kitu

china na japan wanakila sababu ya kushusha thamani ya hela yao, kwa maana wana uwezo mkubwa wa kuhimili soko lao la ndani. Kwa nchi kama yetu ambayo ina nakisi ya biashara ya nje yaani thamani ya export - import = -ve, ukishusha thamani ya fedha yetu unasababisha mfumuko wa bei, hili tumeliona kipindi cha Mh. Mwinyi; thamani ilishushwa sana kiasi mfumuko ulikuwa kwenye tarakimu mbili.
 

Kuna wakati opportunity costs zinahitajika kufanyika, mnadevaluate kwa expense ya kuimport luxuries.

Inflation yetu inachangiwa sana na food price hick up.
 
Fedha....currency ya nchi moja inauzwa na kununuliwa kama bidhaa nyingine yoyote kama fedha yako itahitajika sana lazima itauzwa na itakua juu lakini kama haihitajiki itazid kushuka maana yake ni nini bidha unazo uza inje ya inchi ndizo zitakazo determine fedha yako kununuliwa.kila unapo agiza bidhaa yoyote unahitaji currency ya nchi ile ili upate bidhaa husika
 

mfano poa. lakini na shaka kuna pesa ya arab ya oman na Kuwait ziko juu zaid ya $ nazinafanya poa. bado chumi zao ndogo ukilinganisaa na u s a
na hata wachina wa hindi. lakini pesa kama kuwait demand sio kubwa kama dola hem niweke sawa hapa mkuu?
 
kwahivo kwakua demand ya tsh haiwezi kukua this means value of money will be a determinant factor for the growth of economy?

Demand ya tsh itakuwa iwapo tutakuwa tunazalisha bidhaa na kuziuza nje hivyo wanunuzi toka nje wataihitaji tsh ili kufanya hayo manunuzi...ktk hilo hakuna mbadala
 

Nadhani hili ni somo muhimu sana kwangu na nitahitaji kufahamu mengi zaidi.
 
Maelezo ya wadau hapo juu ni sahihi. Lakini pia matumizi ya currency ktk nchi husika yanachangia sana mfano Tzania tunatumia sana dola hasa kwa matumizi ya kiserikali hiyo inaongeza mahitaji ya dola. Nchi km Botswana inatumia hela zao huwez kununua chochote kwa hela nyingine hata dola! Hiyo husaidia kutengeneza mahitaji ya fedha ya ndani na kupanda kwa thamani yake.

Lakn Pia maamuzi km haya yanategemea na reserve ya nchi husika
 
US dollar huwa inatumika km base currency kwenye nchi nyingi tanzania tukiwemo..ili upate hela ya canada kwa mfano utabadlisha Tsh kwenda Usd then Usd kwenda canadian currency.

Kinachofanya thamaninya pesa yetu kuwa imara au kupungua thamani ni kuhitajika kwake(demand)nje nchi...na nje ya ya nchi wataihitaji tu km wana cha kuifanyia nchini mwetu..kwa maana nyingine km tuna cha kuuza nje ya nchi kunasababisha thamani ya pesa yetu ipande(basing on usd)

Kingine kinachoshusha thamani ya pesa ni upunguzaji(devaluation of currency)unaofanywa makusudi ili kuincourage exports.
 
Fedha zinauzwa katika soko la kimataifa kama bidhaa nyingine, na kama bei ya bidhaa nyingine inavyopatikana kwa sepply and demand, thamani ya fedha hupatikana hivyo hivyo.

Ingawa pia, benki kuu huchangia kupanga bei za fedha kwa kudhibiti mzunguko wa fedha na namna nyingine za udhibiti (e.g the Chinese Yuan is undervalued deliberately by the Chinese central banking system in order to promote the export of Chinese manufactured products)/
 
mfano poa. lakini na shaka kuna pesa ya arab ya oman na Kuwait ziko juu zaid ya $ nazinafanya poa. bado chumi zao ndogo ukilinganisaa na u s a
na hata wachina wa hindi. lakini pesa kama kuwait demand sio kubwa kama dola hem niweke sawa hapa mkuu?

Kuwait ni moja ya ambazo zinaongoza kwa uzalishaji wa mafuta, right?,

na mafuta yanahitajika kila sehemu duniani, so the more you demand the product the more you demand for particular
currency.

NB mafuta yanauzwa kwa dollar lakini arab countries zinatumia hela zao baada ya mauzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…