Comoro (Huitwa 'The Comoros' kwa kuwa ni mkusanyiko wa visiwa vitatu vya Ngazija (Ngazidja/Grand Comore), Anzwani (Anjouan) na Mwali (Moheli). Kisiwa cha nne cha Mayotte kilicho jirani, kiutawala kipo chini ya Ufaransa. Kuna tetesi kuwa enzi za Rais Ahmed Abdallah Sambi, serikali ya Comoro iliomba kujiunga na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; lakini ikaonekana aina au muundo wa muungano tulionao kati ya Tanganyika na Zanzibar hauruhusu nchi nyingine kujiunga!comoro ikijiunga na tanganyika itaipiku zanzibar. Sijui kwa nini kina nyerere hawakuona umuhimu wa kuviunganisha visiwa hivyo na tanganyika. Muda upo kama vipi mazungumzo yafanyike comoro iwe sehemu ya tanzania, wale ni waswahili wenzetu tuwajumuishe kama zanzibar