Nini kauli ya Mahakama kama Muhimili kwa kauli ya Rostam Aziz kuidhalilisha mahakama ya Kisutu?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Rostom Aziz amesema hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.

Na kwamba mahakama zetu hazina uwezo wa kusikiliza kesi za kimataifa hivyo lazima tuzipeleke huko nje.

Je, kauli hizi zinapotolewa na kiongozi na mfanyabiashara siyo dharau kwa mahakama zetu? Je, tukubali tu kwamba mtu anaweza kudharau mahakama na akaachwa kisa ana fedha? Je, kauli hizi zikitolewa na wananchi wasio na fedha mahakama itakaa kimya?

Kwanini hawa watu wamepata nguvu ya kudharau sana wananchi na mifumo yao?

Haiwekani tukakodisha mahakama ili iheshimiwe?
 
Pamoja na yote, tuje kwenye ukweli.

Ni mara ngapi mahakama zetu zinatumika kupora haki za watu? Wenye fedha wamekuwa na mkono mrefu katika kuamua hatma ya kesi.

Rostam kasema ukweli mkubwa.
 
We ulitaka asemeje Kwa mfano? Mahakama zetu zimejaa weledi? Bure kabisa wewe
 
Rostam hajaonesha dharau kwa mahakama bali mahakama isha jidharau kupitia majaji na mahakimu wake.Hili hata makamu mwenyekiti wa CDM mara kadhaa kasha wahi sema kwamba mahakama zetu haziaminiki kimataifa.

Ni mjinga pekee ndio atakuwa na imani kwamba Tanzania Kuna mahakama huru ambazo zinatoa haki,ndio maana Kuna Jaji alisema Kuna waziri aliwahi kuchana hukumu yake sababu kuu ni ni kwamba mahakama si lolote si chochote.

Nilipo chukua umakini kufuatilia kesi ya Mbowe pale niliendelea zaidi kuipuuza mahakama na majaji wa nchi hii jinsi walivyo vilaza.
 
Mfumo mzima wa haki justice system Tanzania hautabiriki na haujisimamii kukataa kutumika. Rostan Aziz mbunge mstaafu wa CCM na mfanyabishara mkubwa Tanzania na wa kimataifa amesema kweli.



Kesi ya Ugaidi iliyokuwa inamkabili Mbowe na wenzie 3 ni mfano tosha kwa watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kutokuwa na Imani na Mahakama pia serikali


Kesi ya Wangwe kuhusu wakurugenzi kushiriki uchafuzi wa chaguzi Tanzania imechapishwa kwa kiingereza, kifaransa, Portuguese, kiarabu, espanol. Je serikali itaacha kutumia wakurugenzi wa majiji na halmashauri baada ya hukumu hii iliyotokewa na Mahakama ya Afrika ?
Application 011/2020 – Bob Chacha Wangwe and Legal and Human Rights Centre v. United Republic of Tanzania13 Jun 2023 | Judgment Summary
EN FR AR PT SW SP


Kesi za Mzee Lugemalila, Sethi imetishia wafanyabishara wakubwa


SETHI HARBINDER SINGH NA JAMES RUGEMALILA
 
Ni kweli kabisa Mahakama haipo huru

Mhimili huu muhimu wa dola unapaswa sasa kuanza kuacha kutumiwa na ufanye kazi kwa haki ndiyo utakuwa mhimili huru unaosimamia sheria na katiba bila kupokea amri toka mhimili wa executive (wanasiasa / serikali)

Jaji Mkuu mstaafu jaji Barnabas A . Samatta ameandika kitabu kuhusu uhuru wa mahakama inatakiwa raia wote ikiwemo jaji mkuu aliyepo ofisini, majaji, mahakimu kukisoma na kuwa rejea kuhusu umuhimu wa mhimili wa Mahakama katika nchi hususan yetu ya Tanzania




5 July 2018

Umuhimu wa utawala wa sheria - Jaji Barnabas A. Samatta

Sheria zinazopelekwa mbele ya bunge (bills) lazima kwanza zichunguzwe kwanza kama zinakiuka katiba, sheria na haki anasisitiza jaji mstaafu B.A Samatta na kusisitiza kila mmoja ktk ngazi za maamuzi wasisitize haki ikiwemo maDC, maRC n.k maana nikusikiliza radio au kutazama TV amri wanazotoa watendaji zingine zina kukakasi mkubwa anamalizia jaji mstaafu B. A Samatta almaarufu "B.A.S" anavyojulikana na washikaji wenzie wa karibu.
 
Rostam is absolutely right. Mahakama is a joke na bandari kuwapa wawekezaji ni lazima sio ombi wala kubembelezana kama tunataka kuendelea.
 
Huo ndio ukweli wenyewe.kwa tz hatuna mihimili inayojitegemea ispokuwa mhimili wa rais tu.mhimili wa urais ndiyo huamua namna mihimili mingine ifanyeje kazi.
 
Mafisadi na wafirisi nchi wamekuwa na nguvu kubwa na mamlaka kubwa pia Sauti kubwa..Jeuri kubwa,Ukwasi Mkubwa..Dharau Kubwa..Kejeli kubwa,Haki miriki ya ushauri sahihi..
 
26 June 2023

Published By:LYDIA CHURI


VYOMBO VYA UPELELEZI VYATAKIWA KUTUMIA NJIA ZA KISAYANSI KUKUSANYA USHAHIDI​


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Mustapher Siyani ametoa rai kwa vyombo vya upelelezi nchini kutumia njia za kisayansi katika kukusanya Ushahidi ili kurahisisha na kuharakisha kazi ya Mahakama ya utoaji wa haki.

Akizungumza na wadau wa utoaji haki katika Mkutano wa Tume mkoani Tabora, Jaji Kiongozi alisema mchakato wa haki jinai utarahisishwa endapo vyombo hivyo vitatumia njia za kisayansi ikiwemo vinasaba (DNA Profiling Tests) mazingira yanaporuhusu na waendesha mashtaka kuwasilisha mahakamani Ushahidi huo.

Alisema kwa zama tulizo nazo hakuna ufanisi bila matumizi ya teknolojia, hivyo alitoa rai kwa vyombo vya upelelezi kwenda sambamba na maendeleo ya karne ya 21 kwa kukusanya ushahidi kisayansi.

“Matumizi ya ushahidi wa vinasaba sio mageni katika nchi yetu. Wakati mauaji ya albino yaliposhamiri nchini na watuhumiwa kufikishwa mahakani, upande wa mashitaka ulitumia ushahidi wa vinasaba kuthibitisha makosa pasipo kuacha mashaka yoyote”,alisema.

Alisema ni matarajio ya Tume na Mahakama kuwa huduma ya utambuzi wa kisayansi wa vielelezo vihusuvyo makosa ya jinai, inayopatikana Dar es Salaam na maeneo mengine machache itapanuliwa na kutolewa katika kila kanda/Mkoa nchini ili kuharakisha zaidi uchunguzi.

Jaji Kiongozi alisema Tume na Mahakama pia inatarajia kuimarishwa kwa matumizi ya ushahidi wa picha na video katika kuthibitisha makosa ya jinai yaliyowasilishwa mahakamani kwa mujibu wa kifungu cha 36 (1) (2) & (3) cha sheria (the Police Force and Auxiliary Services Act (Cap. 322 R.E 2002) pamoja na Kifungu cha 59 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (the Criminal Procedure Act (Cap 20 RE 2019).

Akizungumzia wajibu wa Serikali katika kuweka mazingira bora ya Mahabusu na wafungwa kutoka Mahakama za Mwanzo, Jaji Siyani alisema ni wakati sahihi kwa Serikali kuanzisha mahabusu kwenye kata zilizo na Mahakama za mwanzo ili Mahakama hizo ziweze kutimiza wajibu wake kwa ufanisi na kurahisisha uhifadhi wa mahabusu na wafungwa.



Alisema zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanaotafuta haki mahakamani ikiwemo haki jinai, wanahudumiwa na mahakama za mwanzo nchini. Mahakama za mwanzo nyingi ziko mbali na makao makuu ya wilaya ambako kuna uwezekano wa kuwa na gereza la mahabusu na wafungwa.



Kwa mujibu wa kifungu cha 70 cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu, Wizara ya Mambo ya Ndani, imepewa jukumu la kujenga au kuanzisha Mahabusu kwa ajili ya watuhumiwa na wafungwa wanaohukumiwa na Mahakama za mwanzo kupata hifadhi kabla ya kupelekwa gerezani.

Aidha, sheria imetoa wajibu kwa mamlaka ya Serikali za Mitaa kusimamia mahabusu husika.



“Sote tunafahamu kuwa magereza mengi yalijengwa miaka mingi iliyopita yakikusudiwa kuchukua mahabusu na wafungwa wachache kwa wakati huo. Aidha wilaya nyingi nchini hazina magereza na hivyo kuweka mazingira magumu zaidi ya utekelezaji wa amri za Mahakama za Mwanzo.

Kuhusu umuhimu wa vikao vya Kamati za kusukuma mashauri Kamishna huyo wa Tume alisema kuwa wajumbe wanaounda Kamati hizi wanapaswa kushiriki vikao husika na hivyo kufikia dhamira ya kuanzishwa kwake. Alisema pale inapolazimu kuwakilishwa wahusika wahakikishe wanawapa mamlaka wawakilishi wao na taarifa za mashauri yanayojadiliwa ili kuwawezesha kufanya maamuzi.

Alisema taarifa zilizopo, zinaonyesha kuwa wajumbe wanaotajwa na waraka unaoanzisha kamati hizi za kusukuma mashauri, hawahudhurii vikao husika wao binafsi bali hutuma wawakilishi ambao hawana mamlaka ya kufanya maamuzi na hivyo tija kukosekana
 
Ukiona hivyo ujue kuna aidha.
1. Ameionga serkali i.e viongozi wenye mamlaka ya mwisho.

Na vitabu vya Mwenyezi , subuhana wataalah vinasema " Rushwa hupofusha macho na kuondoa hukumu ya kweli"
2. Huyo anakula nao hivyo hawamfanyi chochote hii ni kuwadharilisha . Ukiwa kiongozi msafi unakiri kula naye na kujiuzulu. Ni Mzee Mwinyi tu aliwahi kukiri kukosea na kujiuzulu.
3. Vyombo hivyo havina weledi wala professionalism ni mwendo wa ubabaishaji hakuna mtu anasimamia kile anajua ni sahihi. Ukisikia CHAWA elewa huyo mtu ameweka akili rehani maana mtu yoyote aweza kukosea ila chawa huwa haoni kosa. Chawa ni PARASITE ni mnyonyaji kwa HOST wake.

Mwl Nyerere aliwahi kusema juu ya Mzungu aliyetamba kuiweka serkali mfukoni. Na nini kilitokea.

Binafsi Rais wetu athubutu aweke heshima kwa ajili ya Haki mbele zake na mbele za Mola wake maisha yanapita. Umr kiyama yaja.
Basi tumpe sua zetu, hekima iwe juu yake. Wasiitukane ofisi yake na wasaidizi wake.
Basi ikibidi Mh mama aje DM niwe mshauri wake na kumuombea dua sitaki uchawa. Wala asinitangaze
 

Hoja ni kwamba alichosema ni sahihi au sio sahihi..?
 
Mafisadi na wafirisi nchi wamekuwa na nguvu kubwa na mamlaka kubwa pia Sauti kubwa..Jeuri kubwa,Ukwasi Mkubwa..Dharau Kubwa..Kejeli kubwa,Haki miriki ya ushauri sahihi..
Matajiri wengi hawaogopi au wanazarau Mahakama kwa sababu Watumishi wenyewe wa Mahakama wakiwaona matajiri Wana kesi,wanaanza kujipendekeza kwa matajiri,hata Kama ni wakosaji!!
 
Mheshimiwa kawa compromised na papa nyangumi, kisa donation ya royal tour hadi amefikia kukashfu mhimili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…