Nini kauli ya Mahakama kama Muhimili kwa kauli ya Rostam Aziz kuidhalilisha mahakama ya Kisutu?

Nini kauli ya Mahakama kama Muhimili kwa kauli ya Rostam Aziz kuidhalilisha mahakama ya Kisutu?

ATHARI ZA RAIS KUWA NA MAMLAKA KISHERIA KUTEUA MAJAJI

  • Uhuru wa mahakama unaminywa.
  • Utendaji kazi wa mahakama unadhorota.
  • Usawa katika utoaji wa haki unapungua.
  • Ni chanzo kikubwa cha rushwa katika mahakama.
  • Rais anakua juu ya sheria.
  • Ni chanzo cha ubadhilifu ndani ya serikali maana nguvu ya kuwashitaki wabadhirifu ambao ni viongozi wa juu.
 
Rostom Aziz amesema hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.

Na kwamba mahakama zetu hazina uwezo wa kusikiliza kesi za kimataifa hivyo lazima tuzipeleke huko nje.

Je, kauli hizi zinapotolewa na kiongozi na mfanyabiashara siyo dharau kwa mahakama zetu? Je, tukubali tu kwamba mtu anaweza kudharau mahakama na akaachwa kisa ana fedha? Je, kauli hizi zikitolewa na wananchi wasio na fedha mahakama itakaa kimya?

Kwanini hawa watu wamepata nguvu ya kudharau sana wananchi na mifumo yao?

Haiwekani tukakodisha mahakama ili iheshimiwe?
MAHAKAMA haina cha kumfanya RA
 
Back
Top Bottom