Rostom Aziz amesema hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.
Na kwamba mahakama zetu hazina uwezo wa kusikiliza kesi za kimataifa hivyo lazima tuzipeleke huko nje.
Je, kauli hizi zinapotolewa na kiongozi na mfanyabiashara siyo dharau kwa mahakama zetu? Je, tukubali tu kwamba mtu anaweza kudharau mahakama na akaachwa kisa ana fedha? Je, kauli hizi zikitolewa na wananchi wasio na fedha mahakama itakaa kimya?
Kwanini hawa watu wamepata nguvu ya kudharau sana wananchi na mifumo yao?
Haiwekani tukakodisha mahakama ili iheshimiwe?