Kwani neno kiumbe maana yake nini? Mungu ameumba viumbe tunavyoweza kuviona na tusivyoweza kuviona, tena hata tunavyoweza kuviona anaruhusu mwenyewe kuviona/kuvumbua/gundua kutokana na wakati. Mfano Mwanzo ilijulikana dunia ni kama meza, kumbe ni mviringo. Kuna watu walitangaza laana kwa wale walokwenda kwenye mwezi kwa kuwa wanaenda kumchokoza kwenye makao yake, walifikiri mbinguni ni juu ya utosi wao, leo ni safari za kawaida. Na vyombo vya masafa vipo zaidi ya Pluto sayari iliyozaniwa ni ya mwisho kumbe zipo nyingine kibao kwa jina la Gallaxy, kuna wakati Joshua 'alisimamisha jua', kumbe dunia ndo iliacha kuzunguka, jua halitembei wala kuzunguka!
Mungu hashindwi kitu, Funguka ufahamu!kuna viumbe kama nyungunyungu wanaishi ardhini,hewa wanapate, lkn wanaishi,kuna bacteria,virus etc, mfumo wao wa kuishi ni tofauti kabisa na sisi, funza chooni, seal chini ya maji ambayo juu yameganda barafu huko Canada, Alaska nk. Wameanza kuonekana UFO, Alliens nk. Kuna Wanefil na Waanaki nk.
Je majini, Shetani, Maroho, Mizimu, Voudoo, Angles etc. Nenda kwa ma Yoga na Budhaa(google) huko ndo utachanganyikiwa! Naamini, vile Mungu aliziumba hizo sayari pia kunaweza kuwa kuna viumbe vya namna yake, ni jambo ka wakati tu kuvigundua tena pale atakapotufunulia Yeye.