Nini kazi ya hizo Sayari zilizobaki ukiondoa Dunia?

Nini kazi ya hizo Sayari zilizobaki ukiondoa Dunia?

Inasadikika kuwa jua ni nyota ila inaoneka hivyo sababu iko Jirani nasi, kama jua ni Nyota he kuna nyota ngapi angani? Na je haziwezi kuwa Na tabia kama za jua hili? Je hakutakuwa Na mfumo kama huu Wa sayari zinazolizunguka jua? Kama zipo je sayari itakayokuwa ya Tatu, haiwezi kuwa Na hali ya hewa kama yetu?

Kama ndio kwanini kusiwe Na viumbe kama sisi?!
 
Hapo hujaeleweka vizuri kuhusu hiyo shortcut ya blackholes hebu fafanua vizuri kwanini inashindikana? Na hiyo black hole inapitika?
Hadi sasa "shimo la mnyoo" (wormhole) ni nadharia tupu. Maanake si uwongo lakini habari zake hadi sasa zatokana na makadirio na matumizi ya mantiki ya kanuni asilia pekee.

Hata kuwepo kwa shimo jeusi (black hole) hadi sasa ni hipotesi (yenye uwezekano mkubwa). Neno shimi jeusi inasema ya kwamba huwezi kuiona; nadharia ya Hawking inakadiria ya kwamba kuna aina ya mnururisho ("Hawking radiation") unaotoka na kama upo ungepimika; ila tu hadi sasa hakuna kilichopimwa.

Ni mada nzuri kwa watungaji wa riwaya za scifi na filamu zao; na pia kazi kubwa kwa watu wenye kichwa kwa hisabati. Sisi hapo chini tutaendelea kusubiri daladala au matatu.....
 
Inasadikika kuwa jua ni nyota ila inaoneka hivyo sababu iko Jirani nasi, kama jua ni Nyota he kuna nyota ngapi angani? Na je haziwezi kuwa Na tabia kama za jua hili? Je hakutakuwa Na mfumo kama huu Wa sayari zinazolizunguka jua? Kama zipo je sayari itakayokuwa ya Tatu, haiwezi kuwa Na hali ya hewa kama yetu?! Kama ndio kwanini kusiwe Na viumbe kama sisi?!
Kuhusu idadi ya nyota kunamakadirio tu.. nyingi! Ona Nyota - Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu nyote zenye mfumo wa sayari elimu yetu ni ya juzi tu inaendelea kubadilika kila mwaka haraka sana. jinsi wanaastronomia wanagundua sayari mpya kwa kufanya utathmini vipimo vya vyombo vya angani. Sayari nyingine ziko, taz. Sayari - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Sidhani Kama Mungu Aliamua Kutuweka Katika Sayari Ya Dunia Halafu Sayari Nyingine Zibaki Kama Mapambo.

Ninachoami Kwenye Hizo Sayari Nyingine Kuna Viumbe Wanaishi Na Either Wana Mungu Wao Au Ni Huyuhuyu Mungu Wa Dunia Ndiye Wanaemuabudu.. Pia Kuna Uwezekano Na Wao Pia Wana sheria Zao Za Kumtii Mungu Na Kuna Wasomi Pia Wenye Akili Na Maarifa Kutushinda Sie Wanadamu..

Nawaza Tu, Kuna Sayari Kubwa Kushinda Dunia,labda Humo Kuna Viumbe Wengi Zaidi, Ila Hatuwezi Kuwaona Kutokana Na Mpango Wa Mungu #freeman
Kuna viumbe vingine lakini uwezekano mkubwa ni kuwa si lazime viwe viumbe kama vilivyo katika sayari yetu. Vinaweza kuwa viumbe ambavyo hatuwezekani kuviona kwa kuwa vimeumbwa tofauti. Vinaweza kuwa viumbe vyenye uelewa na maendeleo kisayansi na kiteknolojia kuliko tulivyo sisi. Miaka kadhaa inayokuja uvumbuzi wa anga za juu unaofanywa sasa hivi utatoa majibu kwa maswali haya.
 
Nakubali jibu lako kabisa. Tatizo kubwa ni wakati na umbali. Dunia yetu inakadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.6 hivi. Kipindi cha kuwepo kwa viumbehai wanaoweza kuuliza maswali jinsi tunavyofanya hapa ni muda mfupi, labda miaka 100,000. Je, tutakaa hapa kwa muda gani tena?

Ukiangalia umri wa sayari nyingine (hili ni swali la kuhisi tu hadi sasa) uwezekano ni mdogo ya kwamba wengine wako pamoja nasi wakati huohuo. Labda kipindi chao kimeshapita, labda bado.

Pamoja na umbali mkubwa wa miaka ya nuru uwezekano wa kuwafikia wakati wako ni mdogo zaidi. Wengi wako katika umbali ambako hatutafika kamwe - isipokuwa kama siku moja teknolojia ya "shimo la nyoo" inapatikana - jambo ambalo hadi sasa halionekani kabisa.
 
I am talking stars, not planets.

We have gathered much of the information about planets in our local solar system. Complete with a Pluto flyby.

To get to exoplanets we need to do interstellar travel

Umbali wa Alpha Centauri, the nearest star, ni about 177,778 times umbali wa Mars.

Kwa makadirio yako hayo, tutachukua miezi 8.5 x 177,778 = miezi 1,511,111 = miaka 125,926.

Teknolojia ya sasa haipo tayari kwa interstellar travel. Hata kwa kwenda nyota iliyo karibu nasi kuliko zote.

Na kuna nyota ziko mamilioni na mabilioni ya umbali huo. Maana yake uchukue miaka 125,926 uizidishe kwa mamilioni na mabilioni.

Kwa mfano ili kwenda kwenye nyota iliyo 6 times umbali wa Alpha Centauri system, just in the neighborhood by interstellar standards.If we have to go to a star 6 times the distance to Alpha Centauri that, by your figures, will take us 755,555 years.The Milky Way Galaxy is 100,000 light years across, Alpha Centauri is just under 4.4 light years away from us, we have to go 11 times the distance to Alpha Centauri to travel half the distance across the Milky Way)
Thanks Mkuu.
 
Nakubali jibu lako kabisa. Tatizo kubwa ni wakati na umbali. Dunia yetu inakadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.6 hivi. Kipindi cha kuwepo kwa viumbehai wanaoweza kuuliza maswali jinsi tunavyofanya hapa ni muda mfupi, labda miaka 100,000. Je, tutakaa hapa kwa muda gani tena?

Ukiangalia umri wa sayari nyingine (hili ni swali la kuhisi tu hadi sasa) uwezekano ni mdogo ya kwamba wengine wako pamoja nasi wakati huohuo. Labda kipindi chao kimeshapita, labda bado.

Pamoja na umbali mkubwa wa miaka ya nuru uwezekano wa kuwafikia wakati wako ni mdogo zaidi. Wengi wako katika umbali ambako hatutafika kamwe - isipokuwa kama siku moja teknolojia ya "shimo la nyoo" inapatikana - jambo ambalo hadi sasa halionekani kabisa.
Mkuu teknolojia ya shimo la vyoo ni ya namna gani?Naomba unijuze!
 
Hapo hujaeleweka vizuri kuhusu hiyo shortcut ya blackholes hebu fafanua vizuri kwanini inashindikana? Na hiyo black hole inapitika?
Kinadharia, black holes kwa jinsi zinavyo distort space time inawezekana ukizipanga mbili pamoja ukapata bonge la shortcut litakalokata millions of billions of light years in distance.

Ni kama vile uwe na meza kubwa sana, halafu kuna sisimizi yuko katikati ya meza kwa chini anataka kwenda sehemu kama ile kwa updande wa juu. pale kuna bonge la shortcut kama akiweza kutoboa tobo katika ile meza, anaweza kufika upande mwingine (juu) wa meza. A black hole creates a hole in the fabric of spacetime and in theory, two black holes arranged on either side could create a wormhole and could be used as a shortcul to travel through great spatial distances.

In practice, our current science is just beginning to understand black holes and we do not have the required energy, tools and scientific understanding to manipulate them. The best thing we could do is observe them from afar.

Kwa Zaidi soma hapa Wormhole Wonders: Hunting Down Spacetime Shortcuts : DNews

WORMHOLE “Shortcut” through Space and Time?
 
Mkuu teknolojia ya shimo la vyoo ni ya namna gani?Naomba unijuze!
Teknolojia ya mashimo haya ni kuchimba tu, kwa koleo, pasipo na mawe mengi mno ardhini.

Ila tu nilitaja "teknolojia ya shimo la mnyoo". Hii haiko hadi sasa. Hata zile "wormholes" hadi sasa hazikuthebitishwa. Ni uwezekano kutokana na makadirio ya wanafizikia lakini hakuna uthebitisho - kile kinachoitwa "hipotesi". Tusubiri (lakini sikui kama jibu litapatikana wakati wa maisha yetu..)
 
It is very anthropic (or quasi-anthropic), hubristic and arrogant to think that the universe exists for mankind or it's equivalent in other places.

There are elements in the original post that seems to look at the universe in this way.

This flaw mainly emanates from a creationist point of view, which assign purpose generously without as much as having any evidence of doing so.

Purpose is overrated. I would put entropy and the laws of physics above that.
 
ukifa unahamia sayari ingine,ila hujijua kwani memory za nyuma zinakuwa deleted
Kweli Mkuu, mi nahisi zangu hazijawa deleted kwani kuna vitu nakumbuka,
nakumbuka kabla ya leo nilikuwa napaa sasa sijui nilikuwa ndege hapo ndo
kumbukumbu hazijakaa sawa. Si ajabu hata wewe utakuja kuwa Fisi au Nguruwe
kwenye sayari nyingine
 
Utafiti unaonyesha kuwa hapo kwenye mwezi tu hakuna hewa ya oksijeni.Hao waliotua mwezini miaka ya 1976 back ward walijibebea hewa ya oksijeni.So kama kwenye sayari nyingine kuna viumbe kabda kwa mfumo mwingine wa maisha na sio huu kwa sababu huko hakuna hata maji. Kama mahali hakuna maji ni jangwa.Nilifurahia sana jamaa mmoja hapa jf intelligence alieleza sana akasema kama wapo viumbe wengine watakuwa sio CARBON BASED Kama sisi bali labda SILCON BASED N.K Maana yake ni kwamba wanaopumua hewa nyingine. Lakini tujiulize kama mwezini hapo karibu ukilingasha na sayari nyingine hakuna hewa je huko ipo?Ni kwa zaidi ya miaka 40 wana anga (astronauts) wanafanya utafiti na hawana majibu. So naamini kama kuna mengi yatakayofahamika kuhusu SPACE sio kwa kizazi hiki.ACHENI MUNGU AITWE MUNGU. UTUKUFU UWEZA VINA YEYE MILELE NA MILELE AMINAAA!
Mbali kutoka wapi? Maana ni space mwanzo mwisho.
 
Sidhani Kama Mungu Aliamua Kutuweka Katika Sayari Ya Dunia Halafu Sayari Nyingine Zibaki Kama Mapambo.

Ninachoami Kwenye Hizo Sayari Nyingine Kuna Viumbe Wanaishi Na Either Wana Mungu Wao Au Ni Huyuhuyu Mungu Wa Dunia Ndiye Wanaemuabudu.. Pia Kuna Uwezekano Na Wao Pia Wana sheria Zao Za Kumtii Mungu Na Kuna Wasomi Pia Wenye Akili Na Maarifa Kutushinda Sie Wanadamu..

Nawaza Tu, Kuna Sayari Kubwa Kushinda Dunia,labda Humo Kuna Viumbe Wengi Zaidi, Ila Hatuwezi Kuwaona Kutokana Na Mpango Wa Mungu #freeman
sayari, nyota na miezi inayo zunguka huko juu vyoote ni chakula ya BLACK HOLE .... tundu jeusi (lenye nguvu kubwa sana ya Graviti ambapo atom haiweze kusavaivu) ambalo wana sayans wameshindwa ku pambanua
 
Kuhusu shimo nyeusi: hapana si vile.

Menginevyo nahisi ya kwamba ulichagua njia ngumu kurudia hekima ya kale:
Hakuna kitu kinachodumu katika dunia hii! Mambo yote yanapita...

(Sijui nimewahi kuiona Biblia? Qurani? Bibi yangu?)
 
Back
Top Bottom