DOKEZO Nini kifanyike bajaji na bodaboda kutosimama kwenye zebra?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Msisahau Hawa ni wapiga kura
 
Kwani urefu wa kamba ya matrafiki ni mita ngapi?
 
Inasikitisha Jeshi zima la polisi linashindwa kusimamia Bajaj na bodaboda waiting sheria. Wako busy kung'oa 3D numbers!
mkuu watu hawajashindwa,wanakwepa lawama za kipuuzi bila ulazima.

kama unakumbuka zamani kulikuwa na watu kwenye junction wanakamata piki piki,hayo makelele yake utadhani walikuwa ni vibaka wanaua watu.

acha kila mtu ashikilie pumbu zake.
 
Sheria ziko wazi tatizo wasimamizi wapo likizo
 
Polisi waambiwe na kupewa ruhusa kuwa hizo ni pesa za kiwi ....yaani waruhusiwe wakimkamata boda kafanya hivyo nusu ya pesa wanachukua na iliyo baki wanawekewa kwenye mfuko wa kukopesha polisi wote nchi nzima
Unadhani kwa njia hii tutatkuwa tumetatuwa tatizo?
 
Usalama wetu hatarini,mi nadhani kwenye kika kivuko wanachovuka wengi awepo trafiki
Fine on the spot yaani kila kosa msimbazi wa hapo hapo unabaki watarejesha heshima ya kufuata SHERIA za Nchi.
Ushamba unawasumbua

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app

mkuu watu hawajashindwa,wanakwepa lawama za kipuuzi bila ulazima.

kama unakumbuka zamani kulikuwa na watu kwenye junction wanakamata piki piki,hayo makelele yake utadhani walikuwa ni vibaka wanaua watu.

acha kila mtu ashikilie pumbu zake.

Inasikitisha sana jamaa hawana utu
Iwekwe kamera jioni trafiki wanareview,au kulia zebra inayovukwa na wengi awepo trafiki na urafiki au uneg usiwepo hapo ni sheria tu
 
Mada nzuri sana hii, binafsi hii tabia inaumiza sana na watu wengi wamekufa, kupata vilema na majeraha, RPC wapo, RTO wapo, Traffic police wapo, IGP yupo, inaumiza sana
Kwahiyo hawa nao kumbe wanachangia huu ujinga,.
 
Inasikitisha sana maana wala Hakuna anayejali


Boda boda wengi na waendesha bajaji hawajaesha driving school mtu amejua tu kuendesha mtaani kabeba pikipiki kaingia road na ni wengi na ni kama vile aina ya watu waliojisusa Yani wanaishi bila future Yani ni mtu ambaye yupo tayari kwa lolote & unakuta anaendesha pikipiki amebinuka kakunja kiuno anaendesha ndala ipo chini ya sehemu ya gia

Hawahofii magari wala sheria lakini wanaoingia hasara ni watu wenye familia zao maana wanabeba watu wenye kutegemewa na familia zao
 
Au uvutaji bangi,pombe na mafuta yanawaathiri nini?
 
Ni kufunga camera kwenye vivuko na kunasa namba za bajaj au pikipiki ambazo dereva wake anakiuka sheria. Akinaswa mtu wa hivyo atozwe 30,000 hapo hapo lakini ndani ya siku 30 apeleke 70,000 mamlaka ya leseni. Zoezi likisimamiwa kwa uadilifu bila ufisadi, itakuwa mwisho wa ukiukwaji sheria.
 
Wafute huduma za bodaboda na bajaj mijini, miji ya nchi za kusini mwa Afrika South Africa, Namibia n.k na hapa Bujumbura Burundi hakuna usafiri wa umma wa bodaboda na bajaj na watu wanafika wanapokwenda.

Bodaboda na bajaj ziwe za usafiri wa vijijini na nje kabisa ya miji huko ndanindani. Pia huko vijijini zisiruhusiwe kutumia barabara kuu .

Nawasilisha hoja.
 
Kuna la kujifunza hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…