Nini kifanyike ili kuondoa hii dhana kwamba Traffic police wapo kwa ajili ya kupata pesa za waendesha magari?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Ni wakati sahihi wa kuondoa hii dhana iliyojengekea kuwa askari wa usalama barabarani wako kwa ajili ya pesa za waendesha magari (madereva)... iwe kihalali au rushwa ni kuwa kuna dhana kwamba matrafiki wanawaza pesa tu. Hii sio sawa. Mimi naona trafiki wako kwa ajili ya usalama barabarani na sio pesa.

Je, wewe unaona nini kifanyike ili kuondoa hii dhana?
 
Funga cctv cameras mabarabarani kila mahali. Ajiri watu (au hao askari peleka mafunzo) wa ku monitor kila wilaya iwe na kituo cha ku monitor traffic activities.

Toa askari barabarani.
 
Waache kupaki magari ya gharama wanapokwenda kwenye check points, imekuwa kama fashion siku hizi,
Askari barabarani napakki klugger chassis number,
 
Ni wakati sahihi wa kuondoa hii dhana iliyojengekea kuwa askari wa usalama barabarani wako kwa ajili ya pesa za waendesha magari (madereva)... iwe kihalali au rushwa ni kuwa kuna dhana kwamba matrafiki wanawaza pesa tu. Hii sio sawa. Mimi naona trafiki wako kwa ajili ya usalama barabarani na sio pesa.

Je, wewe unaona nini kifanyike ili kuondoa hii dhana?
Kwani wewe unaona hii ni dhana.nadhani ni dhahiri na ndiyo ilivyo wapo kwa ajili ya kukusanya fedha kutoka kwa wanchi,wala siyo kwaajili ya kutoa elimu na ushauri.
 
Hii dhana haitaondoka, si tunaona sisi tunaopanda daladala? Akisimamisha gari ni upigaji na sio kukagua gari. Wenye magari yao binafsi hawataelewa.
 
Mheshimiwa hiyo siyo dhana bali ni kweli kabisa, waache hizo tabia ndipo fikra za watu ziondoke vichwani, POLISI TZ kwa asilimia kubwa ni wala rushwa, haijalishi walioko barabarani au ofisini, kazi kubwa ni kufanya dhuluma kwa wahanga na si kuwa saidia.
 
Ni wakati sahihi wa kuondoa hii dhana iliyojengekea kuwa askari wa usalama barabarani wako kwa ajili ya pesa za waendesha magari (madereva)... iwe kihalali au rushwa ni kuwa kuna dhana kwamba matrafiki wanawaza pesa tu. Hii sio sawa. Mimi naona trafiki wako kwa ajili ya usalama barabarani na sio pesa.

Je, wewe unaona nini kifanyike ili kuondoa hii dhana?

Wale kwa urefu wa kamba zao - Mama Kizimkazi.

Wapewe fedha za kubrashi viatu - Jiwe
 
Ni wakati sahihi wa kuondoa hii dhana iliyojengekea kuwa askari wa usalama barabarani wako kwa ajili ya pesa za waendesha magari (madereva)... iwe kihalali au rushwa ni kuwa kuna dhana kwamba matrafiki wanawaza pesa tu. Hii sio sawa. Mimi naona trafiki wako kwa ajili ya usalama barabarani na sio pesa.

Je, wewe unaona nini kifanyike ili kuondoa hii dhana?
Kwani huko barabarani huwa wanafanya kazi gani ya maana zaidi ya kupokea rushwa na kukusanya ushuru wa serikali kupitia makosa ya kubambikia?

Weka camera na vituo vya ukaguzi kwenye maeneo machache! Na hao trafiki warudishwe vituoni wakawalinde raia na mali zao. Hili ndilo jukumu lao la msingi. Masuala ya kukusanya mapato wawachie TRA
 
Back
Top Bottom