Nini kifanyike ili kuthibiti wanaharakati,magaidi na CHADEMA wasikwamishe salamu za mama kwenye matamasha ya miaka 30 ya bongo fleva?

Nini kifanyike ili kuthibiti wanaharakati,magaidi na CHADEMA wasikwamishe salamu za mama kwenye matamasha ya miaka 30 ya bongo fleva?

NgerukeAbra

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
4,253
Reaction score
5,789
Baada ya kufanya uchunguzi wa kina na timu yetu toka Lumumba tumegundua kuwa wanaharakati, magaidi na CHADEMA ndio walionzisha zomea zomea wakati mwana FA alipotaka kuwasilisha salamu za serikali kwenye tamasha la bongo fleva.

Tuligundua wanaharakati , magaidi na vijana wengi wa CHADEMA waliingia kwenye tamasha viingilio vyao vilipwa na Maria Sarungi kwa kushirikiana na Mange kimambi pamoja na mataifa ya kibeberu.

Lengo kubwa la tamasha hilo ni kujaribu kuwafanya watanzania wasahau mambo ya October 29,30 na 31 pia wananchi wasijadili mambo ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Maamuzi ni kwamba kwenye matamasha yajayo viongozi wa chama ngazi za wilaya na mikoa ambayo tamasha hilo litapita watafanya mambo yafuatayo.

a)Kuhakikisha vijana wengi wa sisiem wanahudhuria hata kama hawana viingilio.

b)Vijana hao wataelekezwa wakae sehemu gani ya ukumbi ili itakapofika muda wa kuleta salamu za mama washangilie kwa nguvu zote.

c)Getini lazima uonyeshe kadi ya sisiem.

Wadau naomba michango yenu ya mawazo ili niifikishe kwenye kamati ya tamasha.

Alamsiki.
 
Mods sio 'kuthibiti' ni 'kudhibiti' naomba marekebisho kwenye kichwa cha habari
 
Cha kufanya ni kuacha kuleta uchawa kwa watu waliotumia pesa zao.

Watu wamelipa pesa zao waka enjoy, pale ndani kuna watu wa kila kabila, kila imani, kila itikadi, wameunganishwa na muziki na wamelipa pesa zao, wakaburudike, wasahau shida zao ziliwemo za kisiasa, wewe unaenda kuwakumbusha mambo ambayo wengine hata hawayataki, what do you expect?

Wafanye hivyo kwenye matamasha yao ya free entry sio sehemu ambazo watu watu wamelipa jasho lao. Sina chuki nao ila mambo yao yanakwaza
 
Samia arudi kwao na Tanganyika iongozwe na Rais Mtanganyika atakayechaguliwa na Watanganyika wenyewe kinyume cha hivyo zomea zomea hizi zitazidi kila uchao.
 
Back
Top Bottom