Shida siyo polisi, shida siyo CCM, shida siyo CHADEMA, shida siyo serikali wala siyo Katiba, shida ni sisi watanzania (Waafrika) hata leo tuletewe katiba mpya ya aina gani bado uzandiki wetu ni uleule...hata Mh Mbowe akiwa Rais leo bado uchafu ni uleule, hata Mh Samia aendelee kuwa rais uchafu ni uleule...Sisi waafrika ni viumbe wa ajabu sana, tuna ubinafsi, tuna chuki za ajabu, ni wenye tamaa, ni wezi, wala rushwa, upendeleo umetutawala, leo hii nchi hata iongozwe na CHADEMA, CUF, TLP, ADA-TADEA, ACT nk hakuna chochote tutapata viongozi wataendelea kujishibisha wao, ajira watapeana wao, watoto wao kwanza wataingia BoT, TANAPA, BANDARI, NSSF, BUNGENI, IKULU, TRA, na sehemu zote zenye mboga saba watatawala wao. Mnataka katiba mpya nawashangaa hakuna kipya kitatokea, mnao ikataa katiba Mpya nawashangaa pia hamna la maana la kutueleza. Mtanzania unayejitambua unaweza kuamua kuachana na upuuzi wa kufikiria ni jinsi gani taifa lako linaendeshwa, ukashika jembe ukalima maisha yatakuwa ya kadri....unavunjwa miguu eti unadai katiba mpya...ni ushenzi kama ushenzi mwingine maana hata iwe mpya haitakusaidi chochote bali wana siasa wataendelea kuneemeka.Mbowe, Zito, Msigwa, Mdude, Lisu nk wanahangaika ili wawe kwenye mfumo, wakisha ingia kwenye mfumo hizo kelele hutazisikia tena...wako wapi akina Esta Matiko, wakoa wapi akina Halima Mdee,(covid19) nk. Mbona hawadai katiba mpya kwa sasa, je unafikiri wangekuwa hawakupewa keki na akina Ndugai na Magufuli sasa hivi si na wao wangekuwa rumande kwa harakati za kudai Katiba Mpya? Ampherey Polepole sasa hivi anatembelea kwenye uzi mwembamba unaona yuko kinyume na serikali lakini sababu ni kwamba umeshatemwa na mfumo, je kipindi cha Magufuli hata usiku angeuita mchana ili mradi aendelee kula mema ya nchi. Mfano mzuri tukumbuke ya akina Lowassa (2015), kumbuka yule kijana Patrobas Katambi, kumbuka MWITa Waitara, kumbuka Vicent Mashinji, kumbuka Joshua Nassari, kumbuka Silinde, nk kuna watu walivunjwa miguu kwa sababu tu ya hao wazandiki niliotaja hapo juu, kuna watu wamewekwe rupango, kuna watu wameacha wajane na yatima kwa ajili ya Wapuuzi hao, kuna watu wamepoteza mwelekeo wa maisha kisa wanadai haki kwa kupitia migongo ya hao.....leo akina Mwita Waitara wanakula keki ya Taifa lakini waliowavujia damu na jasho wanawaona wapuuzi tuu. Vijana achaneni na siasa, shida sisi waafrika ni viumbe wa hovyo sana....mnaopoiga kelele leo mkipewa keki mnanyamaza....oooh kumbe hamdai haki bali ni njaa za Uafrika zinawasumbua...fanya kazi zako tafuta pesa utaishi kwa raha sana ukiyafikiria ya Serikali basi utaishia kuumia kila siku.