Nini kifanyike juu ya majengo ya kwenye viwanja vya Nanenane na Sabasaba ambayo hukaa bure na wazi kwa mwaka mzima?

Nini kifanyike juu ya majengo ya kwenye viwanja vya Nanenane na Sabasaba ambayo hukaa bure na wazi kwa mwaka mzima?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hasa majengo ya nane nane. Kwenye viwanja hivi ambavyo vipo karibu kila mkoa, utakuta taasisi nyingi zimejenga majengo mazuri na ya kudumu. majengo haya huwa hayatumiki na watu kwa mwaka mzima isipokuwa Kwenye sherehe za nane nane au sabasaba. Tunawezake kuyatumia majengo haya kwa faida kwa mwaka mzima?

Maoni yangu. Serikali za majiji zingeanzisha digital parks kwenye viwanja hivyo. Wasupply internet kwenye viwanja hivyo bure. Watu wenye kufanya kazi mtandaoni waende kutumia majengo na internet ya hapo. hili linawezekana kabisa, kuna miji kama Kinondoni, Mbeya na Dodoma yameanzisha timu na yanazihudumia. hawawezi shindwa kuweka internet ya bure kwenye viwanja hivyo.

Siku hizi mitandaoni kuna vikazi vingi sana vinavyoweza mpatia mtu kipato. kwa kufanya hivyo itakuwa ni hatua fulani kuelekea kutatua tatizo la ajira.

Unafikiri majengo hayo ambayo hukaa bure yanawezaje kutumika kwa faida.
 
Back
Top Bottom