Nini kifanyike kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania?

Bila kuitoa ccm madarakani uzalendo itakuwa ngumu kuwepo nchi hii. Sasa hivi kuna uzalendo wa mdomoni na tumboni na sio moyoni. Hali hii imesababisha kuwa vigumu kutofautisha uzalendo na ujinga.
 
Na Ndo mana mwaka huu tunawapa nchi Chadema. Enough is enough!!!
 
Tafuta clip moja ipo youtube magufuli alipoonana na viongozi wakuu wastaafu. Kuna maneno aliambiwa na Majaji wakuu wastaafu Augustino Ramadhan (Mungu amrehemu) na Barnabas Samata. Majibu ya hilo swali lako yapo kwenye michango yao kwenye kile kikao

Kama huwezi kuiona mwambie mkuu bagamoyo akuletee ile clip humu
Sawa ila nafikiri uzalendo ni kwetu wote sio kwa mtu mmoja ingawa Rais anatakiwa kuwa mzalendo namba moja. Hili Magufuli ameliweza
 
Ili uzalendo urudi ni lazima wanasiasa watambue kwamba wamechaguliwa na wananchi kuongoza serikali iliyowekwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya wananchi na sio kutumia wananchi kama ngazi ya kujinufaisha wao na kikundi cha marafiki zao wachache.
 
Huu ulikuwa mkutano mubashara na ni Rais aliyeuita. Hamuoni kuwa hapo ni uzalendo kwa Rais kutaka kijifunza kutoka kwa wazee hao?
Je baada ya huo mkutano kulikuw na mabadiriko??? Raisi alijifunza nini baada ya kupewa hizo nondo???
 
Ni mara ngapi tumewalaumu ndugu na jamaa zetu kuwa wamepata nafasi nzuri lakini wameshindwa kula (kuiba)?
 
Tutoe kwanza boriti kwenye macho yetu halafu ndio tushughulike na kibanzi kwenye macho ya wanasiasa. Sisi Kama wananchi, uzalendo wetu uko wapi?
 
Uzalendo uliisha pale Nyerere aliponga'tuka. Sisi wazee tulikuwa wazalendo wa kweli vijana waliozaliwa baada ya 1985 kwanza hawaelewi nini maana ya uzalendo alafu tamaa ya fedha za haraka haraka. Lakini tatizo la uzalendo sio TZ pekee inayolia hata nchi kubwa kama Russia, Ufaransa na nchi karibu zote za kiafrika zina matitizo ya raia kukosa uzalendo labda kidogo nchi za Arabuni zinajitutumua na hii ni kwa sababu utamaduni wao umeungana (linked) na dini vigumu kutofautisha culture na dini. Hii mada ni nzuri na muhimu sana hasa kwa taifa letu ambalo linapitia wakati mgumu sana usisahau pale viongozi walipoanza kulimbikiza mali na kupora mali za serikali wao na familia zao, walipojiingiza kupora mali asili, wanyama n.k na hasa muhimu ni hawa wahamiaji haramu waliojaa nchini wanakimbia kambi za wakimbizi alafu wanachanganyika na raia na vitambulisho vyote wanavyo
 
Tupewe Lissu wetu.. Mumkabidhi tu kiti chake cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Uzalendo uliisha pale Nyerere aliponga'tuka. Sisi wazee tulikuwa wazalendo wa kweli vijana waliozaliwa baada ya 1985 kwanza hawaelewi nini maana ya uzalendo alafu tamaa ya fedha za haraka haraka. Lakini tatizo la uzalendo sio TZ pekee inayolia hata nchi kubwa kama Russia, Ufaransa na nchi karibu zote za kiafrika zina matitizo ya raia kukosa uzalendo labda kidogo nchi za Arabuni zinajitutumua na hii ni kwa sababu utamaduni wao umeungana (linked) na dini vigumu kutofautisha culture na dini. Hii mada ni nzuri na muhimu sana hasa kwa taifa letu ambalo linapitia wakati mgumu sana usisahau pale viongozi walipoanza kulimbikiza mali na kupora mali za serikali wao na familia zao, walipojiingiza kupora mali asili, wanyama n.k na hasa muhimu ni hawa wahamiaji haramu waliojaa nchini wanakimbia kambi za wakimbizi alafu wanachanganyika na raia na vitambulisho vyote wanavyo
Umesema vizuri sana kiongozi. Sasa nini Kifanyike? Ilikuwaje Mwl. Nyerere akafanikiwa? Labda na sisi tuige hapo
 
Back
Top Bottom