Nini kifanyike kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania?

Nini kifanyike kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania?

Wanajamvi.

Ili nchi yoyote iweze kiendelea inahitaji wananchi wake wawe na uzalendo. Kwa maoni yenu, nini Kifanyike ili kukuza uzalendo miongoni mwetu sisi raia wa Tanzania?
Kunatakiwa umoja wa kitaifa ambao utajadari jambo la kitaifa, hiyo fursa haipo zinatumika akili zile zile kufikiri kwa niaba yetu 'We can not solve our problems with the same level of thinking'
 
Mithali 14:34
"Haki huinua taifa,bali dhambi ni aibu kwa watu wo wote"

Shida iko hapo!
 
Kunatakiwa umoja wa kitaifa ambao utajadari jambo la kitaifa, hiyo fursa haipo zinatumika akili zile zile kufikiri kwa niaba yetu 'We can not solve our problems with the same level of thinking'
Hapa nachukua wazo la kuunda kamati ya kitaifa itakayokuja na mapendekezo ya nini Kifanyike. Wazo hili nimekuwa nalo muda Sasa
 
Haki sawa.
Uchumi kwa wote.
Elimu bora na nafuu kwa wote.
Huduma bora na nafuu kwa wote.
Miundombinu bora na safi kwa wote.
Maendeleo ya Taifa yafaidiwe na wote.
Siasa safi na uongozi bora wenye usawa.
Demokrasia sawa kwa wote..

Uzalendo utakuja tu automatic bila fimbo..
 
Uzalendo uliisha pale Nyerere aliponga'tuka. Sisi wazee tulikuwa wazalendo wa kweli vijana waliozaliwa baada ya 1985 kwanza hawaelewi nini maana ya uzalendo alafu tamaa ya fedha za haraka haraka. Lakini tatizo la uzalendo sio TZ pekee inayolia hata nchi kubwa kama Russia, Ufaransa na nchi karibu zote za kiafrika zina matitizo ya raia kukosa uzalendo labda kidogo nchi za Arabuni zinajitutumua na hii ni kwa sababu utamaduni wao umeungana (linked) na dini vigumu kutofautisha culture na dini. Hii mada ni nzuri na muhimu sana hasa kwa taifa letu ambalo linapitia wakati mgumu sana usisahau pale viongozi walipoanza kulimbikiza mali na kupora mali za serikali wao na familia zao, walipojiingiza kupora mali asili, wanyama n.k na hasa muhimu ni hawa wahamiaji haramu waliojaa nchini wanakimbia kambi za wakimbizi alafu wanachanganyika na raia na vitambulisho vyote wanavyo
Sasa hao waliozaliwa 1985 ndio walioanza kujilimbikizia mali ?
Hivi Chenge kazaliwa 1985 ?

Tangu hapo nyinyi wazee baadhi yenu sio wazalendo ni wabinafsi kupindukia.
 
Mmmh! huyo SI ndio yule aliwataka wazungu waache kushirikiana nasi kwasababu anaamini serikali ndio ilimshambulia? Yaan kwasababu yake yeye mmoja watanzania wengine M55 wacheleweshewe maendeleo.

Ndio, ni yeye anaetaka ushoga Tanzania
Ndio, ni yeye anayepinga kila jema
Ndio, ni yeye asietaka tulimde rasilimali zetu kwa kigezo kuwa tutashughulikiwa
Mbona hiyo serikali yenu ya ccm huwa inawaita wazungu hao hao mabeberu.

Nyie kweli ni vilaza mliokubuhu.
 
Wanajamvi,

Ili nchi yoyote iweze kiendelea inahitaji wananchi wake wawe na uzalendo. Kwa maoni yenu, nini Kifanyike ili kukuza uzalendo miongoni mwetu sisi raia wa Tanzania?
Cha kwanza kabisa ni kuiondoa ccm madarakani, wamefanya watanzania kuichukia nchi yao..
 
Uzalendo umeondoka na Mwl.Nyerere, Uzalendo unaanzia kwa viongozi ngazi ya juu kuelekea chini.
Ili viongozi wapimwe uzalendo wao walitungiwa MWONGOZO ,ulibaini miiko na kanuni ya uongozi.
Lakini baya zaidi kinachouwa uzalendo ni CCM na serikali yake baada ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi.Walio madarakani wanapambana kuwamaliza wapinzani wanawaona hawafai kwa lolote.Ni wazi katika hali kama hiyo hakuna kuaminiana ni kushuka kwa uzalendo kitu hicho ni hatari sana kwa siku za mbeleni .
Dawa yake ni kwanza kuheshimiana kuachana na unafiki,na kutowapa nafasi madaraka ya aina yoyote watu wapuuzi .
 
Hao akina Msekwa ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom