Nini kifanyike kunusuru huu mradi wa Magomeni Kota?

Nini kifanyike kunusuru huu mradi wa Magomeni Kota?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Nimesikitishwa na hii habari ya gazeti la the citizen kuhusu maghorofa ya Magomeni Kota. Lawama wametupiwa zaidi wapangaji kwa kushindwa kutunza mazingira ya hilo eneo zikiwemo majengo. Pia wamekuwa wakikaidi kulipa gharama za usafi na zingine za kuhakikisha mradi unakuwa sawa. Wewe una maoni gani? Je, hawa wapangaji wapewe notisi ili kuleta wapangaji wenye uwezo wa kuishi hapo? Au, washauriwe kuuza hizo apartments kwa wenye uwezo?


View: https://www.instagram.com/p/DM42bu9oNdm/?igsh=MW1obDV2NDM3Z3Buaw==
 
nmekaa hapo kota block two floor ya juu. Changamoto kuu hapo ni maji aisee yaan maji hayapandi hivyo lift ndo kama mkokoteni japo lift ni nzima na inapiga kaz fresh tu. Kingine ni kama hamna property manager wa kuhakikisha usafi na mambo mengine. Watu wabish kutoa michango yaan kiufupi maskini habebegi. Mwisho the citizen nao wameongeza chumvi sana hapo kweny matatizo
 
CCM hawawezi kila kitu
Emu watz tuwe na utaratibu wa kujenga hoja na kutafuta suluhishi. Kwan wakitoka CCM si watakuja wengine je watafanyeje kuhakikisha hayo matatizo hakuna, nadhan ndo ungekua msingi wa hoja kuliko kuleta spinning za kisiasa kweny critical issues
 
Hiyo ni sifa kuu ya muafrika hasa mtanzania hakuna tunachoweza kuendesha ushapushamba wa kutosha hapo magomeni kota ni uwakilishi wa 1.mwendo Kasi
2.Uwanja wa Mkapa
3.stand ya magufuli
4.Udsm
5.Udom
6.shule mbali mbali za akina akumbukwe
 
Duniani Kuna kazi kuu ngumu sana kushinda chochote;

Mosi ni kutafuta hela na

Pili ni kumfadhili masikini (masikini )hafadhiliki, habebeki kwa namna yyt ile, haelimiki, hashauriki, hastaarabiki, hatunziki, haambiliki, hashikiki, ..........kwa kifupi masikini ni mzigo mzito ambao hata mnyamwezi hawezi kuuvumilia.
 
Watu wanafikiri kuishi kwenye apartments ni rahisi. Hata ukiinunua kila mwezi lazima ulipe SERVICE CHARGE. Shida inaanzia hapa. Mtu akishanunua au akilipa kodi hataki kulipa service charge. Service charge ndio inagharamia usafi,ulinzi,umeme kwa ajili ya lift,taa za nje au water pump na mafuta ya generator kama ipo. Sasa hawa wa Magomeni hata service charge ya 30,000/- wanasumbua je wangeweza huko ambako service charge tu inaweza kuwa $200?
 
Nadhani kichwani una minyoo. Kila kitu CCM
CCM ndiyo. Hatujawahi kuongozwa na chama kingine. Culture na tabia za mtu mmoja mmoja zilizojijenga Tanzania huwezi kuzitenganisha na CCM. Jiulize ni kwa nini kila nchi watu wanakuwa na tabia nyingi ambazo ni unique...? Hii inatokana na uongozi unavyoi-shape jamii husika. Ukiwa na serikali isiyoruhusu shortcut kwenye kipato, matokeo yake unakuwa na jamii inayochapa kazi kwa sababu hakuna njia nyingine ya kupata mlo.
 
nmekaa hapo kota block two floor ya juu. Changamoto kuu hapo ni maji aisee yaan maji hayapandi hivyo lift ndo kama mkokoteni japo lift ni nzima na inapiga kaz fresh tu. Kingine ni kama hamna property manager wa kuhakikisha usafi na mambo mengine. Watu wabish kutoa michango yaan kiufupi maskini habebegi. Mwisho the citizen nao wameongeza chumvi sana hapo kweny matatizo
Hatari sana.

Dkt. Gwajima D "Planning"
 
That's was poor plan kuwaweka masikini kuishi huko.

Masikini Kama anashindwa kutoa buku tatu huku uswahili ndo aje atoe elfu 30 ya service charge ahaaaa .

Ushauri hizo apartment wapewe watu wenye vipato Vya kati na juu .
 
Nyumba walizonyang'anywa wenyewe Upanga, Kariakoo na mjini kati wakawekwa 'wanyonge' zilikosa matunzo. Hata bomba za majitaka zilipoziba hazikuwa zikizibuliwa.

Taratibu walianza kuzirudisha kwa wamiliki wa awali kwa kulipwa vilemba.
 
CCM ndiyo. Hatujawahi kuongozwa na chama kingine. Culture na tabia za mtu mmoja mmoja zilizojijenga Tanzania huwezi kuzitenganisha na CCM. Jiulize ni kwa nini kila nchi watu wanakuwa na tabia nyingi ambazo ni unique...? Hii inatokana na uongozi unavyoi-shape jamii husika. Ukiwa na serikali isiyoruhusu shortcut kwenye kipato, matokeo yake unakuwa na jamii inayochapa kazi kwa sababu hakuna njia nyingine ya kupata mlo.
Wewe naona umeamua kuwa mjinga kwa sababu unazozijua wewe mwenyewe. Basi hata huu ujinga ulio nao ni CCM wamekusababishia.
 
Back
Top Bottom