SoC01 Nini kifanyike kuondoa fikra ya kuajiriwa miongoni mwa wimbi kubwa la vijana Tanzania

SoC01 Nini kifanyike kuondoa fikra ya kuajiriwa miongoni mwa wimbi kubwa la vijana Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Neema Kapinga

New Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1
Reaction score
0
NINI KIFANYIKE KUONDOA FIKRA YA KUAJIRIWA MIONGONI MWA KUNDI KUBWA LA VIJANA TANZANIA.

UTANGULIZI.
Suala la ukosefu wa ajira limekua tatizo kubwa sio Tanzania tu bali dunia nzima. Tanzania ina idadi kubwa ya vijana ambao hawajaajiliwa pia bado kila mwaka idadi kubwa ya vijana wanahitimu mafunzo kutoka vyuo mbalimbali nchini wakiwa na tumaini la kuajiriwa, na kitu cha kusikitisha ni kwamba ajira ni chache sana. Fikra ya kuajiriwa inadumaza akili ya vijana.

YAFUATAYO YANATAKIWA KUFANYIKA ILI KUONDOA FIKRA YA KUAJIRIWA MIONGONI MWA VIJANA.

1.Kutolewa kwa elimu na uhamasishaji juu ya ujasiriamali na uwekezaji kwa vijana , elimu inaweza kutolewa na.
●Taasisi za kifedha kama banks mfano asilimia kubwa ya vijana waliopo vyuoni wana mikopo wanaweza kuhamisishwa kuweka akiba bank kwenye kwenye account maalumu kama fixed account ambapo pesa inaongeza kutokana na kiasi cha riba, mwisho kijana anaweza itumia pesa hiyo kuanzisha biashara akimaliza masomo yake

●Pia jamii husika(wazazi) wajenge mazingira kwa vijana kujihisisha katika shughuli za uzalishaji mali kutokea umri mdogo mfano jamii ya ufugaji ijenge misingi ya ufugaji kwa vivazi vyao, pia jamii ya kilimo na zinginezo. Hii itafanya vijana wakue katika mazingira ya uzalishaji hivo kuacha kutegemea ajira.

2.Kubadilishwa kwa mtaala wa elimu, Asilimia kubwa ya elimu inayotelewa Tanzania siyo ya vitendo na haiendani na mazingira pamoja na rasilimali zilizopo hivo kushindwa kumuuandaa kijana kupambana na mazingira yanayomzunguka na kusubiri kuajiriwa. Kwahiyo elimu itolewe kwa vitendo zaidi na iendane na rasilimali zilizopo nchini ili vijana wazitumie katika shughuli za uzalishaji mali na kuondokana na fikra za kuajiriwa.

3.Serikali ijenge mazingira mazuri kwa uwekezaji na ujasiriamali ambayo yatavutia vijana, mfano
●Uwepo wa soko la uhakika kwa malighafi na bidhaa zinazozslishwa nchini, soko la uhakika liaweza tengezezwa na serikali kupitia diplomasia nzuri ambayo italeta mahusiano mazuri baina ya nchi na kuhamasisha biashara, pia kuweka mazingira mazuri ya wageni kuja kuwekeza miradi mikubwa ambayo italeta soko kwa malighafi nchini. Pia kuweka mbei nzuri elekezi kwa mazao ili kuvutia vijana kwenye uzalishaji.

●Pia serikali itoe mikopo yenye masharti nafuu ili wapate mitaje na kuanzisha shughuli mbalimbali kama kilimo, ufugaji, uvuvi n.k ili waache kupoteza muda kwenye kutafuta ajira ambazo ni chache.

●Uboreshwaji wa miundombinu kama umeme, barabara na maji ambayo ni chachu kwenye uzalishaji hii itavutia vijana wengi kwenye uzalishaji.

4.Taasisi binafsi, makampuni, blogs, NGO's ziwe mstari wa mbele kuwezesha vijana. Kupitia elimu, mitaji, mafunzo mbalimbali ya kiujasiriamali ili kuleta mageuzi kwenye fikra za vijana.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom