Nini kifanyike kuondoa kero ya kukatika umeme mara kwa mara?

Nini kifanyike kuondoa kero ya kukatika umeme mara kwa mara?

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Kwa umri wangu huu ninapoingia miaka 60 sijawahi kushuhudia umeme kuwa stable hapa nchini kwetu Tz. Kuna sababu nyingi zimekuwa zikitolewa ambazo zimekuwa zikijirudia hizohizo miaka yote:
1. Maji kupungua bwana la mtera
2. Kukosekana kwa mvua
3. Hitilafu ya mitambo
4. Mitambo kufanyiwa maintenance
5. Kubadilisha nguzo
6. nk, nk, nk, nk

Muda mwingine nashangaa mvua zikinyesha tunaambiwa maji yamezidi.

Muda mwingine tunaambiwa mvua imeharibu au kuangusha nguzo.

Kabla ya kuanza ujenzi wa bwawa la Nyerere, nakumbuka tulishaahidiwa mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na gesi ya mtwara kuwa ingemaliza shida ya umeme, nakumbuka kipindi cha utawala wa Kikwete kuna kauli zilikuwa zikitolewa kuwa tatizo la umeme litakuwa ni historia ( akamaliza muda wake).

Baada ya kuanza huu ujenzi wa bwawa la Nyerere naona wana siasa ndio wamepata pa kushikia kuwa likikamilika tatizo la umeme nchini itakuwa ni historia.

Kipindi cha Magufuli, ALHAMDULILAAH kuna muda tulisahau tatizo la umeme japo kuna muda ulikuwa ukikosekana, NINAAMINI NI KUTOKANA NA UKALI WAKE KWA WATENDAJI , nakumbuka alikuwa akiwaeleza mawaziri husika na watendaji wa sekta ya umeme kuwa hataki kusikia umeme unakatika KWASABABU YOYOTE ILE. Binafsi nampongeza sana JPM kwa ukali wake hasa kwa watendaji wa wizara na taasisi za serikali MAANA KIUKWELI TUNAFAHAMIANA SANA TABIA ZETU WATANZANIA.

IFIKE WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI YATAKAYOONDOA HII KERO MOJA KWA MOJA. NA MIMI BINAFSI NAONA NI BORA SHIRIKA HILI WAPEWE WAZUNGU WALIENDESHE.

IMENIUMA SANA SIKUKUU KUKOSA UMEME
 
Inasikitisha sana ila viongozi wetu nao wapo kimya kwenye hili
 
Back
Top Bottom