Nini kifanyike kupunguza/kumaliza ajali barabarani?

Nini kifanyike kupunguza/kumaliza ajali barabarani?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Hapa nakaribisha michango ya namna ya kupunguza/kumaliza ajali barabarani. Nategemea kupata mawazo mapya na yanayotekelezeka. Angalizo, faini kubwa haiwezi kuzuia ajali!

1. Kuhusu mwendo kasi hasa wa mabasi ya abiria, nafikiria kuangaliwe utaratibu wa kupunguza mabasi mengi ya njia moja kuondoka muda sawa. Mfano kutokea stand kuu za miji mikubwa ambayo ni salama, kwa nini wasiangalia utaratibu wa kuruhusu mabasi kuanzia saa kumi: 04h00/04h30/05h00/05h30/06h00/ inamaana hadi inafika saa kumi na mbili na nusu mabasi yanakuwa yameshaondoka.

Sasa hivi abiria wanapenda mabasi ya kuwahi hasa wale wanaounganisha magari kwenda vijijini, baada ya kufika kituo cha mwisho: suluhisho yawepo mabasi yanayo ondoka mapema ili kusiwe na haja ya kukimbia.
 
Ajali nyingi kwetu sisi zinachangiwa na miundombinu mibovu ya barabara, uzembe wa madereva unakuta mtu amelewa bado anaendesha gari ten sio private ni ya abiria kbs na sheria zetu za barabaran ni mbovu kbs imagine uko ulaya halaf mtu ajulikane anaendesh gar akiwa amelewa faini yake inavyokuwa kubwa?

Yote kwa yote rusha nayo inachangia pakubwa mnooo kuondosha uhai wa ndug zetu mabarabarani
 
Moja turekebishe barabara zetu. Tutoke kwenye njia 2 twende njia 4 hadi 6. Hii itasaidia kiasi fulani.

Tufunge mifumo vithibiti mwendo palipo na uhitaji wa kudhibiti na sio tochi za vichakani. Gari ikizidi speed itakutana na faini zake mbele kwa mbele.
 
Ajali zinasabaishwa na miundo mbinu mibovu..na mwendo kasi bila kusahau ubovu wa vyombo vya usafiri..tukitibu hayo matatizo tumesolve tatizo.

Twende kwa njia 4 za barabara...sheria kali ziwekewe kuzuia mwendo kasi katika maeneo yaisiruhusiwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom