mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Utajiri wa nchi yetu ni mkubwa ktk rasilimali mbalimbali kama misitu,madini,Mafuta na Gesi.
Mikataba ya siri mingi tulioingia na wawekezaji mingi imekuwa na matobo ya kutuadhibu inapotokea tumevunja,kusitisha ama vinginevyo..
Inavyoonekana mapungufu ya kimkataba yamekuwa yakichukuliwa kama kinga na siraha za wawekezaji kuendelea kunyonya au kutuumiza kiuchumi..
Nchi yetu imekuwa ikilipa mabilioni ya fedha kama fidia,adhabu na n.k na kutikisa uchumi wetu dhaifu na kusababisha maumivu makubwa.
Ni wakati wa kuweka mikakati sawa ya kuhakikisha tunakuwa na nguvu kubwa ya kupambana na ukoloni mamboleo.
Napendekeza hatua zifuatazo:-
1: Hatua kali zichukuliwe kwa wote wanaohusika kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa taifa.Na hili lisiishie kwa wanasiasa pekee bali pia watendaji na maofisa wa umma wenye dhamana..
Mapana ya hatua yahusishe hata wakiwa wastaafu.
2: Mikataba inayohusisha rasilimali za nchi iwe wazi na ijadiliwe kwa kina na kwa uwazi
3: Vyuo vyetu viwezeshwe kimkakati kuwa na kozi mtambuka ktk masuala ya kisheria..Madini,Misitu,mafuta na gesi.
4: Makampuni yanayotushitaki kwa nia ovu ya kuendelea kutufanya maskini yawe blacklisted (Yenyewe,wabia,wanahisa,na watendaji wao wakuu)..Wawe maadui wa taifa letu.