Un
Unaporesha mifumo ya elimu sawa,lakin hii mikataba kwanza ni Siri na pili , mikataba inasukwa kwa njia ya kifisadi. Kuna wahuni ambao hao wazungu wakilipwa na wao wanapata mgao.Ili kukomesha tatizo hili:-
1. Tuboreshe Mifumo yetu ya Elimu, iwe mifumo inayoendana na mahitaji ya kidunia ya Sasa, mifumo iliyo Bora na imara, yaani iwe mifumo yenye kutoa Elimu Bora inayweza kushindana kimataifa tofauti na mifumo iliyopo Sasa hivi ambayo inatoa 'Bora Elimu.'
2. Kuwepo na Demokrasia na Uwazi (Transparency) kwenye Michakato yote ya awali wakati Taifa au Serikali inapotaka kuingia Mikataba na Taasisi, Makampuni, au hata na Serikali nyingine ya nje. Mikataba yote kabisa iwekwe hadharani na Wananchi washirikishwe kikamilifu katika kutoa Maoni yao (Civilians or Public Participatory Approach) izingatiwe kikamilifu.
Ikiwezekana kuwe na Kifungu au Ibara maalumu kwenye Katiba ya nchi kinachozuia usiri kwenye suala hili la Mikataba ihusuyo Serikali na Makampuni binafsi.
3. Kuwepo na Sheria Kali sana za Kulinda Rasilimali za Nchi ili zisiuzwe hovyo hovyo kiholela. Kitendo Cha kuuza au Kuingia Mikataba ya kuuza au kubinafsisha rasilimali za nchi kwa Siri au kiholela ihesabike kuwa ni kosa kubwa zaidi sawasawa na kosa la UHAINI katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuuza au kubinafsisha kiholela rasilimali muhimu za nchi ihesabiwe Kama ni kitendo kiovu Cha Usaliti dhidi ya Nchi hii na dhidi ya Watanzania wenzako. Hii itasaidia Watu kuheshimu rasilimali muhimu za nchi zilizopo ambazo zinatumika kwa maslahi mapana ya wananchi wote.