Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Nimefuatilia mahojiano mbalimbali kwa miaka ya hivi karibuni ya vyombo vya ndani ya nchi na nje ya nchi. Nilichobaini Taifa lina wanasiasa wasiofika ishirini ambao wanaweza kutofautisha mahojiano maalumu na uwasilishaji wa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa.
Katika ngazi za vyombo vya habari vya magharibi na vya Dunia tunao wanasiasa waandamizi wafuatao wanaoweza kujieleza na dunia ya wasomi ikachambua hoja zao. Naomba nitaje wachache:
1. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
2. Mhe. Tundu Lissu
3. Mhe. Zitto Kabwe
4. Mhe. January Makamba
5. Mhe. Freeman Mbowe
6. Mhe. Emmanuel Nchimbi
7. Mhe. James Mbatia
Nimewataja hawa baadhi kwa kuwa wamewahi kwa vipindi tofauti kupata nafasi na kuhojiwa kwenye vyombo vikubwa vya kimataifa katika kipindi ambacho Taifa linapitia wakati mgumu na linahitaji dira na mawazo yasiyoendana na hotuba za majukwa ya siasa. Naweza nikawa nimewasahau baadhi lakini mifano hii itoshe kuonyesha nawalenga watu wa kariba gani.
Kitaifa hao niliowataja hapo wote wana uwezo mkubwa wakujenga hoja bila kushambulia personalities. Sambamba na hao wapo viongozi kama Mhe. Mwinyi, PM, Makamu wa Pili wa Rais, Halima Madee, Mnyika, Kabudi, Mtaka, Mtanda, Wenye, Heche, Pambalu, Mhe. Biteko NK
Kwa idadi hii utabaini tunao watu wachache wanaofanya vizuri kimatiafa, tunao wachache pia wanaofanya vyema kwenye public speaking ndani na tuna kundi kubwa la viongozi wasioweza kutenganisha mahojiano maalumu na mkutano wa adhara.
Hali hii ipo tofauti sana na kipindi wakina Warioba na wazee wa umri wake wakiwa wanakabidhiwa madaraka. Kwanza walikuwa hawana exposure, shule haikuwa kubwa sana vichwani mwao lakini waliweza kusimama kwenye majukwaa ya ndani na nje ya nchi.
Wazee wa umri wa akina Butiku wakihojiwa leo vijana watazana kwenye TV na wakienda kwenye majukwaa ya kisiasa wananchi watanyamaza kuwasikiliza. Tuambieni leo hii viongozi gani waliochini ya 60 yrs ambao wanaweza kumudu mahojiano serious ya kimataifa na wakaweza kumudu jukwaa la siasa wananchi wakatulia kusikiliza hoja.
Kutokana na kushuka kwa capacity ya kujenga hoja nchini , vyama vyote vimewekeza nguvu kwa comedian, wanamziki na wasanii. Jukwaani wanakaa wasanii muda mrefu then wanasiasa ambao ndio wenye jukwaa wanaishia kupanda kusema oyeeeeeeeeee, safiiiiiiiiii, bomba si bombaaaaa, mtanipaaaaaa.
Tufanye nini tupate wakina Mkapa, Butiku, Warioba, Salim, Shivji, Hassard wengi?