Nini kifanyike kwenye bongo fleva ya Sasa?

Nini kifanyike kwenye bongo fleva ya Sasa?

Wakuu mambo vipi ?
Kutokana na maoni ya mashabiki wengi wa huu muziki wetu pendwa wa bongo fleva kwamba muziki wa Sasa hauna ladha kama muziki wa zamani ,
Je nini kifanyike? Tufanye kama zamani au vipi?
Na generation ya sasa hivi wanasemaje kuhusu muziki wetu wa Sasa tuendelee nao au kama maproducer tushirikine na maproducer wa zamani au wasanii wazamani?
Je wanasema muziki umeharibiwa ,wamlaumu nani mwenye makosa,
Je ni sisi maproducer,wasanii,media,wadau,au mashabiki wanaohitaji sound ya Sasa?
NB:Maoni yako ni muhimu ,
Changia hoja kistaarabu bila kejeli,dhihaka, na matusi.

Hapo chini nimekuwekea baadhi ya midundo ya zamani na ya Sasa.

Nawapenda mashabiki zangu.
Zombie ktk mix zako ile violen kinanda kiwe kinatoka sana peke yake au Bongo zile ngoma tatu za kupigwa na mkono ziwe zinasikilizana zaidi utakuja kunipa jibu .
 
washauri ndugu zako wa sanii wa kizaz chako wapunguzo copy and paste.., afu s2 hv hz id wasanii wanapokuja studio kwako mnawapa ushaur nn wafanye au mnapokea tu pesa au mnawarecodia bure, unakuta ikitamba trend flan wote wapo hili jambo linatokana na nn? Nataka jua toka kwako maana ww ndie unaehusika na mapishi
 
Siku hizi mziki wetu maudhui ni 25%, beat sijui midundo 75% ila sidhani kama hilo linahusiana na producer?
 
Naamini katika Burudani, Msanii ndiye kiongozi wa Shabiki.. kwa mfano wako bado kuna uwezekano mkubwa wakuwauzia Viatu na Suti hao wamasai ikiwa tuu wataweza kumudu gharama kutokana na ushawishi wako. Bongo tunafeli katika ushawishi kwasababi Ubunifu ni Ziro..!!
Ni hivi
Shabiki ni mkubwa kuliko msanii kwa maana kwamba ukifungua duka la suti kwa masai, biashara yako ili iende na kukua inategemea na wamasai wangapi wananunua bidhaa zako na kukubali.
Ingekuwa msanii ana uwezo wa kumshawishi shabiki kungekuwa na wasanii wengi sana wangetoka hata wewe ungekuwa msanii pia.
Mwanzoni kipindi bongo fleva inaanza nyimbo zilikuwa nyingi sana zenye ujumbe na zilikuwa zinapokelewa na mashabiki kwasababu mashabiki walikuwa na maadili ndiyo maana Afande Sele alichukua tuzo.
Jamii ya sasa wengi ni vijana wa miaka 2000 na maadili hakuna sasa yameporomoka mno.
Mtu mzima ukienda kwa jirani, watoto wanakusalimia tena wanakupa na kiti ukae ila sasa hawa wazazi maadili yameshuka na wanawalea watoto wao pasipo kuzingatia maadili.
Utashangaa mtoto wa darasa 7 anakuangalia tu hakusalimii, akikutukana ukamchapa mzazi wake anakuja juu km mbongo.
Turudi kwenye muziki, kutokana maadili kushuka kizazi kimekuwa ni cha kusifia pombe, ngono, uvutaji bangi na wizi.
Usipoangalia mashabiki wanataka nini muziki wako utakufa ndiyo maana kuna nyimbo ukiisikiliza unabaki unashangaa halafu ni hit song... Honey by Zuchu.
N.B
Shabiki ni mkubwa kuliko msanii pasipo shabiki kazi na msanii mwenyewe wanapotea kwenye ulimwengu wa muziki kwahiyo ili msanii awepo lazima amsikilize mashabiki wake wanataka nini.
Sikiliza nyimbo zinazoshika 1-10 Tanzania zinaongelea nini? Nyimbo ili iwe hit song lazima usifie ngono, pombe, utumiaji wa madawa na wizi.
 
Bado haujanielewa... Hivi wateja ndio walitaka Toyota watengeneza gari aina ya IST au ubunifu wa mtengenezaji ndio umewavutia wanunuzi..?

Huo mfano utumie katika dhana ya ubunifu... njoo kwenye bidhaa na uhitaji... bado nakataa kwamba nyimbo za sasa ni kwasababu mashabiki wanazitaka zisifie pombe starehe na ngono. Hizo sifa utazipata kwenye mashahiri ambacho katika mziki mashahiri hayana athari kuubwa kama ilivyo kwa mitindo na milibdimo ya sauti ya mtu na vyombo vya mziki.

Leo hii Bado mziki wa ngoma za kitamaduni una mvuto kuliko bongodleva timekoaa ubunifu wakuufokisha masokioni na machoni mwa watu kwasababu wafikishaji nao ni kama wewe hamuamini katika ubunifu zaidi ya trending.

Swali... MSANII NI KIOO CHA JAMII...

Tutathibitisha huo usemi kwa msanii kufanya wanachotaka mashabiki.. au kwa msanii kufanya anachokitaka kwa mashabiki.?
 
Back
Top Bottom