Naamini katika Burudani, Msanii ndiye kiongozi wa Shabiki.. kwa mfano wako bado kuna uwezekano mkubwa wakuwauzia Viatu na Suti hao wamasai ikiwa tuu wataweza kumudu gharama kutokana na ushawishi wako. Bongo tunafeli katika ushawishi kwasababi Ubunifu ni Ziro..!!
Ni hivi
Shabiki ni mkubwa kuliko msanii kwa maana kwamba ukifungua duka la suti kwa masai, biashara yako ili iende na kukua inategemea na wamasai wangapi wananunua bidhaa zako na kukubali.
Ingekuwa msanii ana uwezo wa kumshawishi shabiki kungekuwa na wasanii wengi sana wangetoka hata wewe ungekuwa msanii pia.
Mwanzoni kipindi bongo fleva inaanza nyimbo zilikuwa nyingi sana zenye ujumbe na zilikuwa zinapokelewa na mashabiki kwasababu mashabiki walikuwa na maadili ndiyo maana Afande Sele alichukua tuzo.
Jamii ya sasa wengi ni vijana wa miaka 2000 na maadili hakuna sasa yameporomoka mno.
Mtu mzima ukienda kwa jirani, watoto wanakusalimia tena wanakupa na kiti ukae ila sasa hawa wazazi maadili yameshuka na wanawalea watoto wao pasipo kuzingatia maadili.
Utashangaa mtoto wa darasa 7 anakuangalia tu hakusalimii, akikutukana ukamchapa mzazi wake anakuja juu km mbongo.
Turudi kwenye muziki, kutokana maadili kushuka kizazi kimekuwa ni cha kusifia pombe, ngono, uvutaji bangi na wizi.
Usipoangalia mashabiki wanataka nini muziki wako utakufa ndiyo maana kuna nyimbo ukiisikiliza unabaki unashangaa halafu ni hit song... Honey by Zuchu.
N.B
Shabiki ni mkubwa kuliko msanii pasipo shabiki kazi na msanii mwenyewe wanapotea kwenye ulimwengu wa muziki kwahiyo ili msanii awepo lazima amsikilize mashabiki wake wanataka nini.
Sikiliza nyimbo zinazoshika 1-10 Tanzania zinaongelea nini? Nyimbo ili iwe hit song lazima usifie ngono, pombe, utumiaji wa madawa na wizi.