Nini kilikufanya uache kula kwa majirani

Nini kilikufanya uache kula kwa majirani

Mda mwingine unaona njaa itaniua unaamua kugusa gusa (kula) kwa majirani, baada ya hapo masimango ya kuwa "mpaka hapo ulipofikia bila sisi ungekuwa umeshakufa uwe unatushukuru kila kukicha[emoji51]" na kadhalika.

Binafsi masimango ndio sababu iliyonifanya niache kula kwa majirani
Sasa huko kwa majirani ulikuwa unawaomba chakula au ulikuwa unapiga chabo wakitenga chakula tuu unatia timu?
Huna familia?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa alikua anapenda sanaa ubwabwa... Na hajui kutafuta hela pia ana mke na watoto kama watano hivi...

Nyumbani kwake alikua anaacha unga na maharage au mboga za majani..

Sasa jirani yake mmoja alikua single mama na biashara zake za kuuza mchele... Kwahiyo jamaa alikua anatabia za kumvizia akitoka kwenye biashara anampokea mzigo then anazama ndani kusubiri ubwabwa uive als aende kwake...

Kuna siku yule mama baada ya kula chakula akafunga mlango akamwambia umezoea kula vyakwangu bure sasa ni zamu yako kuchakata mbususu hii.... Shida jamaa alikua mlokole wacha aanze kupiga kelele majirani njoeni hahaha..

Majirani nao wakamwambia umezoea kula ubwabwa wa bure haya chakata hiyo mbususu sasa hakuna cha bure... Basi ikawa fedheha kwa jamaa mtaa mzima...

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
TAPETA
☕☕☕
 
Nakumbuka nikiwa mdogo nilikatazwa kabisa kula kwa jiran, hata jiran akinikaribisha namjibu nimeshiba hiyo ni nidham njema kabisa.
ilifika hatua hata nikisafiri na mama nikikaribishwa chakula ugenini nasubiri ruhusa ya mama kwa kumuangalia machoni Hadi aniambie Lucha kula.

Na ustaarabu wa kula ni kula kilicho mbele yako siyo unazungusha mkono sahani zima, huku unalamba vidole na unatafuna huku umefunga mdomo Hadi umeze kilicho mdomoni ndo unaruhusiwa kumega chakula kingine , sasa yale maadili yamenifanya nisione kuwa ni kitu Cha kawaida tu kula kwa jiran na hata Kama unanjaa na huna namna ukikaribishwa usianze kupakua kwa pupa unajaza sahani kama unasafari ya miguu kutoka Dar-Kigoma.

Kwa jirani siyo kwako ukijenga mazoea ya kula kula hovyo utashusha heshima yako.
 
Aisee,hii dunia kuna vijana wamekosa aibu kabisa
 
Nakumbuka utotoni,skan maza alikuwa ikitokea harusi wanaondoka wote wananiacha mim,coz nilikuwa sipendi kutembea hasa kwenye masherehe,Sasa ikifika usiku inabidi nimendee kwa jirani alikuwa msukuma,nalala pale kalimbia na mlango wao kulikuwa na kiukuta flani hivi,waniniita nikale,daa! Kunarafiki yangu mmoja hivi alikuwa anaitwa masanja daa,nakukumbuka mwanangu jamaa alikuwa namkuta tayari kashanawa Ila mim nikitaka kunawa na yeye anajifanya anataka kunawa xo anachokifanya ananifinya ili nisile 😆😁 xaxa Mimi naelewa kitu naufinya ubweche alafu baada ya hapo nakikataa
 
Kupenda kula kwa jirani ni matokeo ya malezi mabaya kabisa ktk familia, kwa hiyo kinachokusumbua ni malezi uliyolelewa...
 
Mambo ya kula ndo yamenifanya sinaga kabisa nguvu ya kwenda hata kutembelea ndugu zangu.

Kula kwa watu siko huru kabisa, nafikiri sababu kubwa wakati niko shule ya msingi niliwahi kupita kula kwa ndugu upande wa baba muda wa mchana kutoka shule. basi taarifa zikafika home kuwa nna tabia ya kula pale.
Nilipopata taarifa nilijiskia vibaya kwa sababu home sio kama maisha magumu, ila kwenye ile familia kuna ndugu mmoja alikuwa ananipenda sana akasema siku hiyo nisikatae kula chakula ila baadae taarifa ikafika home.
Tangu siku hiyo sijawahi kanyaga tena mpaka leo 15+ years.

Niko nje ya mada ila kiukweli ni aibu kula kwa watu.
 
Sipendi kula kwa watu.
Sipendi wageni wa ghafla wanakuta mmepanga bajeti yenu na wao wanajumuika
 
Back
Top Bottom