Kule serikalini kuna likizo ya mwaka siku 28, na katika kila likizo za miaka miwili, mojawapo mtumishi analipwa nauli yake na ya familia yake pamoja na mizigo. Huku private sector havipatikani kwa utaratibu, inategemea na huruma ya Management.
Kule nilikuwa napata allowance za semina, wakati mwingine semina ya siku mbili inarefushwa hadi siku saba, ya siku saba inaenda siku 14. Hata kama ilikuwa inawezekana kufanyika ndani ya chumba kimojawapo ofisini, itapelekwa nje ya mkoa ili perdiem zisomeke sh. 150,000/= kila siku, local transport (taxi) 30,000/= kila siku na transport ya bus itategemea. Huku sector binafsi, semina ya siku tatu inafanyika kwa siku moja na hakuna malipo.
Kule nilikuwa naweza kuomba study leave na nikaendelea kulipwa kila kitu ikiwa pamoja na ada plus stipends, huku ukitaka kusoma uache kazi, au tafuta programme za nje ya muda wa kaxi kwa gharama zako.
Kule nikifiwa na mtoto au mzazi, nitapewa kila kitu cha mazishi ikiwa na usafiri wa Coaster iwapo nitahitaji kusafirisha popote. Huku nitatumiwa mjumbe asome salamu za rambirambi.
Kule nikipata mauti kwa ajali nikiwa kazini, njiani kwenda kazini au njiani kurudi kutoka kazini, basi familia yangu itaendelea kupata 70% ya mshahara niliokuwa ninaupata hadi siku ambayo ningestaafu kisheria. Huku familia itasomewa salamu za rambirambi na mwakilishi.
Kule nilikuwa napanda cheo kila baada ya miaka mitatu, na nyongeza ya mshahara ya mwaka. Huku hata cheo nilichopewa hakiko katika mfumo maalum