Nini kilikufanya usifikie ndoto yako ya Upadrisho?

Nini kilikufanya usifikie ndoto yako ya Upadrisho?

Wakuu zamani vijana wengi wa kikatoliki moja kati ya ndoto zetu ilikuwa ni kuwa Mapadre.

Mimi binafsi nilijichanganya sana Huko Rombo, parokia ya Mkuu wakati huo nilikuwa napenda sana Shirika la mtakataifu Aloyce, kutumikia altareni huku ndoto zetu ikiwa ni baadae kwenda seminari hadi Upadrisho

Asee wakati huo nilikuwa najitoa sana nilikuwa sipendi mademu wala pombe yaani nilikuwa nikisikia mtu anakkunywa pombe namuona kama ibilisi, shetani kabisa.

Nilipofika kidato cha tatu mwamba nikaanza kujichanganya na wadau,Pombe kwa sana mademu full yaani unalewa hadi walevi wanakuita mlevi. Malaya kuwazidi hata wale uliowakuta kwenye tasnia ya zinaa

Nikaanza kupotezea masuala ya kutumikia na mawazo ya upadre yakakata kabisa, Nilikuwa na washkaji wengi sana wakati Huo wanaitwa Gilliadi, Imma,Isdovic, Ireneusi, Fredias, Hillary n. katika ile timu ni Hillary na Evaristi tu ndio mapadre kwa sasa.

Wale vijana wengine ndio tumekuwa na tabia mbaya kuliko watu wengine mtaani.

Binafsi ndoto yangu ilikatika kwa sababu ya Ulevi na zinaa.

Vipi wewe nini kilikufanya usifikie, na maisha yako hapo kitaa kwa sasa yanaendeleaje?
padre anakatazwa ulevi? au umeamua tu kuandika vitu vya uongo
 
Nilitumikia Kristu Mfalme hapo 1989 to 1994 kiukweli nilikuwa na malengo ya kufika ngazi ya upadre shida ilikuwa kujuana Sana nikaishia kwenda shule za Serikali by then Old MOshi hapo. Pls mwenye nyimbo ya shirika la MT Aloyce Ile tuliimbia kabla na baada ya kukutana kila jumamosi mwenye nao anisaidie au autupie hapa
mara mia salaaam huo au upi
 
inaelekea kuna kitu hukijui, au wewe ni mtoto sana. hujielewi
Padre hata ukimtembelea anakoishi bia zpo kwenye friji, wewe unaniuliza maswali ya kijinga hapa
kwa hiyo kuwa na bai ndio ulevi sio? huoni kwamba wewe ndio mtoto
 
Yes ni nyuma ya kanisa la KKKT, pale ndio shetani alipatumia kuzima ndoto yangu ya upadri.
Nilishauriwa sana na masista na mabruda lakini wapi, maana ndio walikuwa watu wangu wa karibu sana kutokana na nilichokuwa nakitaka.

Kuna mmoja nilikuwa nasoma nae kwa sasa ni padri aliniambia ameniota huku napokimbilia ni kubaya, nitakuja kujutia na itakua too late, kuna kipindi mahusiano yalinipiga kweli kweli nikawa nayakumbuka sana maneno yake.
pole sana mkuu. achana na ndoa haha
 
Wewe haujawahi hata kukanyaga Seminari, wewe ulikuwa na ndoto ya kuwa padre lkn hakuwahi kukugusa hata hatua moja ya huo wito.
kwani hiyo hatua inaanzaia seminari au inaanzia ndani ya Mtu kisha parokiani wanaichochea ndio uanednelea huko mbele?
 
Honestly, hivi unaanzaje kupenda kazi ambayo masharti yake ni no women no sex

1718011603704.png
 
Mkuu hawakukufanyizia kweli?maana naskia wengi ndio michezo yao Kwa alter boy.Have you tell us the whole truth?
 
Back
Top Bottom