Nini kilikuvunja moyo ulipofika Dar es Salaam kwa Mara ya kwanza?

Nini kilikuvunja moyo ulipofika Dar es Salaam kwa Mara ya kwanza?

Nilishangaa watu wanakula utumbo wa kuku , kichwa na miguu !! wakati mkoani hivi vitu vinatupwa !! Hiyo hiyo siku nafika jirani kulikua na Arobaini nikasema ngoja nikaoshe macho kidogo !! hicho kisingeli kinavyochezwa na kina dada aseee !!!
ila tuseme ukweli hii bongo hakuna mkoa unaoifikia Dar hata nusu ya kwa kila kitu kuanzia maovu na mishemishe na uchafu hadi bata linalolika DSM.

Tunahitaji majiji manne makubwa kama DSM. Nchi itakuwa imefanya jambo kubwa na kuchochea uchumi wa taifa
 
Nilijua dar hakuna vumbi, kila kona lami na kusafi...maana mkoa nilipokua kila aliekua anakuja akitokea dar alikua ana ng'aa,, doh kufika ndo kwanza nikafikia mabibo karibu na kigogo luhanga, kwa wanaopafahamu wataelewa tena luhanga ya enzi zile
 
nilifikia mbagara nikitokea temeke dar!....kweli ile ni daaaaah!
 
Shauri yako vijana wa hovyo watatimba pm.
Joto la Dsm ni kero hasa kwa siye walamba udongo(watembea kwa miguu)
😂😂 Kwamba magari mnaenda nayo kila pahala mnayabebelea kichwani au? Yani kama saiv jasho linanitiririka ila niliokaa nao hapa wamejifunika na masweta wamevaa eti kuna kibaridi
 
Nilijua dar hakuna vumbi, kila kona lami na kusafi...maana mkoa nilipokua kila aliekua anakuja akitokea dar alikua ana ng'aa,, doh kufika ndo kwanza nikafikia mabibo karibu na kigogo luhanga, kwa wanaopafahamu wataelewa tena luhanga ya enzi zile

Hatari sana Huko
 
Wapi nitapata nyumba ya kupanga kwa Dar? Nataka owe ya kupanda Bus 1 kufika Biafra! Sitaki usumbufu! Self contained na sijui ni gharama kiasi gani?
 
Coco Beach. Huko Nyakanazi nilikuwa naiona Coco beach kwenye sherehe za mwaka mpya za magazeti ya Sani na Bongo. Watu wanakula bata, beach safi, wanacheza volebo nk. Kuja kuiona kwa macho nilikuwa dissapointed sana.
Mtu yoyote wa mkoani anapoiona Coco beach kwa mara ya kwanza lazima awe dissapointed.
 
Back
Top Bottom