Nini kilikuvunja moyo ulipofika Dar es Salaam kwa Mara ya kwanza?

Ilikuwa likizo ya high school, nikaja Dar kwa mara ya kwanza .. Tulipanda zile coaster toka Moro kuja Dar, huyu mwanafunzi mwenzangu, ndiye mwenyeji Dar... Akasema twende alipokuwa anakaa au atakapofikia Oysterbay... Nakumbuka tulishuka kituo cha fire...Mdogo mdogo kwa miguu, UN road, mara Salendar bridge, hapa ndio Kaunda tukakata , mbele tukaenda Msasani road, ndiko tulikokuwa tunaenda... Kama saa nne hivi ya usiku tukafika, Tukamkuta Maza house amekaa na shoga ake wa kishombe shombe fulani la kiarabu ...Wanakunywa bierre,... Yaani walivyokuwa warembo na ile hali ya kigiza , ni kama niliona niko ndotoni........ Wakatuambia tuingie ndani...Basi kuna mdogo mtu na maza house, akawa anajishaua hatari, mara kaweka nyimbo hii anacheza au anaimba .... Nililala kwa mang'amung'amu sana kwa zile , anasa kama za peponi zilizoonekana kwenye nyumba ile.. Kesho yake mwenyeji, akanipeleka ofisini kwa ndugu yangu mitaa ya samora, enzi hizo ofisi za maana zote zipo samora...Mwenyezi akauliza ulifikia wapi, nikamweleza Oysterbay kwa mtu fulani.. Akaniambia mpeleke akachukue mzigo wake ... Tukachukua mzigo nikaenda zangu Keko....

Sasa Keko, ndiyo ilinishangaza kwa wanawake walivyokuwa tayari na nje nje kwa kufanya uzinifu...Ingawa Keko palikuwa hapana utukufu kama Oysterbay, kwa kweli nilipafurahia sana , likizo hiyo fupi ya mwezi wa tisa nilipata mpenzi mwanafunzi mwenzangu, ingawa anasoma chuo cha ufundi pale Keko...Nilipata likizo fupi na tamu na ndivyo , nilivyopata nguvu kumaliza form six , kwenda JKT kwenye bogi la Urubani, nikasepa pale kikosi cha Ukonga, kuwahi penzi langua la Keko, kuja kushtuka makuruta wenzangu washarudi kumalizia service....... Ashukuriwe jamaa mmoja mjanja mjanja aliyekuwa na connection karibu na masoldier wote enzi hizo, akaniaandikia memo, nikaenda nayo Makao makuu ya JKT , nikapokelewa kama mfalme na kupelekwa kombania na nikapewa alama nzuri za uaskari wa operesheni yetu...

Kweli sitasahau nilivyoingia Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, hiyo hisia sijawahi kuipata kwenye miji mbalimbali nimetembelea duniani. Siku hizi nikipita Keko , siachi kumkumbuka ...Y...
 
HARUFU MBAYA

Dar es salaam inanuka

Inanuka uozo wa uchafu majalalani, jasho za watu, na vinyesi vya kwenye chemba kila kona

Aidha,inanuka shombo hasa maeneo ya feri

Pia kuna maeneo mengi ya Dar es salaam kunanuka Ngono
 
Watu kunywa maji kwenye mfuko
Maarufu kama Maji ya Kandoro

Pamoja na miaka mingi kupita ila still maji hayo ya Kandoro bado yapo, tena unakuta ya baridi kabisa 🙌
 
Nilikutana na hali ya mazingira ya uchafu ambayo kwa mtu aliyestaarabika asingeweza kuivumilia.

Lakini baada ya muda nikawa nimeizoea hadi kutafuta Kiwanja na kuanza Ujenzi 🙌

Nilichojifunza pamoja na Changamoto za DSM lakini ndiyo Mkoa, ama Jiji zuri kuliko Majiji mengi hapa Nchini.

Ukiona umeshindwa kuishi jiji la DSM na fursa zake hizi zilizopo hutaweza kuishi Majiji mengine na ukafanikiwa.

Wale waliobahatika kufanya kazi ama kuishi Arusha, Mwanza, Dodoma n.k mtakuwa mashahidi.

Kitu ambacho ningeshauri kwa Serikali ni kununua ama kulipa fidia baadhi ya Wananchi wa maeneo ya Manzese, Ubungo, Buguruni, Msasani, Sinza, Keko n.k kisha kujenga majengo marefu na kisha kuyapangisha ili kupunguza Ujenzi holela wa maeneo hayo pamoja na kuvutia Jiji.

Yaani ukipita hayo maeneo, nyumba zake hazivutii kabisa utasema Nchi haina Viongozi wenye maono

Kila mtu mwenye uwezo na nafasi na aje DSM.

Karibuni kuwekeza DSM (Kwa Sauti ya RC Chalamila).
 
1. Kumuona mwanamke anavuta fegi
Mlimani City(Kwetu sijawahi kuona
hii kitu miaka 21 ya uhai wangu)
2. Mwanaume ambaye ana pigo za
kike(Nilifadhaika sana aisee)
3.Joto
4.Kunyolewa kwa afu tatu(Barbershop)
wakati Mkoani kwetu ilikuwa 700
tu(Saluni za kawaida) na bado
wakataka kunipiga 5000 ya kusikrabu
sijui nini. Niligoma aisee!
 

Hapo kwenye Afu tatu hapo😂😂
 
Asante umeiwakilisha vizuri keko bila kuinyima haki yake lakini je haukutendwa na vibaka ?

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mara ya kwanza natimba mjini,kwanza mvua ilinipokea kibaha, wingu km lote.
Halafu niko nyuma ya Land rover 110 huku huyu mdingi alienipa lift kapakia Mbuzi anawapelekea ndugu zake.
Safari enzi hizo hakuna lami,tumechapa vumbi toka mikoa ya kati huko mzee ndo kwanza kufika bongo kaanza kutwanga bia.
Brother akachukua gari fasta twende home ukalale.
Nafika maskani Chipsi yai nusu kuku,Bro huyo karudi mzigoni.
E bana kulikua na kibinti cha mwenye (kizaramo)Nyumba Zena kikazama ndani.
Nikala punyenye vya kutosha
Aisee hapo ndo ilikua karibu mjini.
Badae mengine tunaweka koponi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…