Yesu alikuwa na Pesa nyingi sana kuliko watu wa dini wanavyotueleza.
Ushahidi.
1: Alikuwa na Muhasibu. MTU binafsi bila kampuni wala biashara kufikia hatua ya kushindwa kutunza kipato chako hadi Uwe na Muhasibu basi utakuwa na Pesa nyingi sana.
2: Aliwazuia mitume wasifanye biashara zao. Aliwakuta jamaa wakinapetro ni wakokozi na wavuvi nguli akawaambia waache alafu wamfuate.
Kulisha breakfast, lunch na dinner wanaume 12 wasio na Kazi miaka mitatu mfululizo inabidi Uwe na Pesa. Ushahidi Baada ya kufa Petro aliwashawishi warudi kwenye Biashara zao.
3: Hakuna kifungu Yesu kaishiwa Pesa au kashindwa kufanya muamala wowote kisha hana salio. Aliwahi kudaiwa kodi ya hekalu, akamtuma Petro akavue samaki aliyekuwa na Pesa tumboni.
4: Muhasibu wake alikuwa mwizi na mwenye uchu wa Pesa. Huku tunaona makampuni maduka Yenye wahasibu wezi huwa yanafirisika. Yuda hakuwahi kufirisi mkoba wa pesa za mwalimu wake Yesu.
Wakuu Yesu alikuwa yuko vzr kiuchumi.
Sasa najiuliza nini nilikuwa chanzo chake cha fedha ikiwa
Alikuwa hana biashara
Hakuwa na gawio LA sadaka masinagogini na hekaluni?
Je alikuwa anawafadhili?
Je alikuwa anakusanya Sadaka kwenye mihadhara yake?
Je Alikuwa anashushiwa kimiujiza.?
Mathayo 6
24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.