Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KWA NINI BENJAMIN MKAPA ALISHINDWA KUCHAPA TAAZIA YA ABDUL SYKES KATIKA THE NATIONALIST BRENDON GRIMSHAW AKACHAPA "OBITUARY" YA ABDUL SYKES KATIKA SUNDAY NEWS (TANGANYIKA STANDARD)?
Mgogoro wa EAMWS nimeueleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Vyombo vilivyohusika katika mgogoro ule kuanzia gazeti la Uhuru na The Nationalist Mkapa akiwa Mhariri, Radio Tanzania Dar es Dalaam Martin Kiama akiwa Mkurugenzi, Polisi Geofrey Sawaya akihusika na Usalama wa Taifa alikuwapo Rashid Kayugwa.
Wote hawa walikuwa wakiamrishwa kutoka juu wengine wameyasema haya kwa kujuta kabla ya kufa kwao.
Hakika ni mkasa wa kusisimua.
Nataka nikupe mfano mmoja.
Kifo cha Abdul Sykes katikati ya mgogoro wa EAMWS maziko yake yalikuwa hayajapata kuonekana Dar es Salaam.
Mazishi yale yalikuwa habari kubwa kutokana na mchango wa Abdul Sykes katika TANU na uhuru wa Tanganyika achilia mbali kuwa yeye ndiye aliyempokea Nyerere Dar es Salaam na kuishinae nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Haya hakuna aliyekuwa hayajui na hii ndiyo ilikuwa sifa yake kubwa akitambulika kama mwezeshaji wa mambo yote ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.
Sasa jiulize vipi magazeti ya TANU chama alichounda Abdul yasimwandike inavyostahiki?
Mkapa kama mwandishi bila shaka alijua uzito wa stori iliyokuwa mbele yake na pengine kwa kufahamu uhusiano wa Abdul na Nyerere alimtaka Nyerere mwenyewe amwandikie rafiki yake taazia kwa mkono wake au amhoji (exclusive interview).
Yawezekana kuwa Mkapa aliyataka yote haya kwa Mwalimu na yeye akakataa?
Hapa ndipo panapoumiza kichwa.
Kuamini kuwa Mkapa kwa kutaka kwake tu aliamua kupuuza kifo cha Abdul Sykes huu ni muhali mkubwa sana.
Mwandishi mpumbavu peke yake ndiye anaeweza kuchagua uamuzi wa kijinga kama huu.
Benjamin Mkapa hakuwa mtu zuzu.
Kama ulivyohitimisha kuwa Allah ni mjuzi wa siri na dhahiri nami nasema hivyo hivyo.
Yapo mengi Mkapa aliyafanya hata alivyokuwa rais lakini kwa hali ya siasa zetu Tanzania, alijikuta mikono yake imefungwa na si kufungwa tu bali imefungwa nyuma ya mgongo wake.
Hapo chini ni taazia ya Abdul Sykes katika Sunday News la 20 October, 1968.
Lakini taazia hii ilileta mgogoro mkubwa ofisi ya TANU Lumumba.
Kuna baadhi ya viongozi ndani ya TANU walikerwa na taazia hii.
Hapo chini kuna Kumbukumbu ya Abdul Sykes kama zilivyochapwa na magazeti ya Chama na Serikali Uhuru na Daily News ya tarehe 12 Oktoba 1988.
Kumbukumbu hizi nazo zikafikwa na mkasa pia.
Wahariri walitishika na waliyoyasoma wakasema hawatachapa hadi wamepata kibali kutoka Dodoma.
Walipopewa ruhusa ya kuchapa Kumbukumbu ya Abdul Sykes yale yote muhimu katika kumuelewa Abdul Sykes yaliondolewa.