Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Nguruvi...
Mimi nakubaliana sana na wewe.
Abdul si lolote hata baba yake si chochote.

Hata sijui ilikuwaje ikawa yeye kitabu chake kimetikisa kiasi hiki.
Kitabu hakijatikisa kiasi hicho, ni hype tu. Kwa jinsi ulivyokiandika hakuna shaka wengi wamesombwa na wimbi. Baada ya kutanabahisha, wengi wanarudi kujiuliza nini kilitokea !! Wanaanza kuchuja chuya na punje
Wanairejea ngano kwa jicho upembe!

Wengi hawakujua kuwa AA na TAA ziliendeshwa kama family business, hakuna muongozo, katiba n.k.
Hawakutambua kuwa aliyebadilisha siasa za ukumbini na vibarazani ni Mwalimu Nyerere
Hawakujua , kwamba, Abdul alimpokea Nyerere ni changa la macho.
Hawakujua kuwa Abdul hawakuwahi kugombea na kushinda uchaguzi wowote wa siasa
Hawakujua kuwa Abdul aliongoza genge la wahuni kushikisha adabu wazee wa Dar kwa kiu ya utawala
Hawakujua kuwa Abdul hakuwahi kufanya mkutano wowote nje ya kipata na Tandamti
Hawakujua Mwanzilishi wa AA ni Mwalimu Matola na wenzake na si kazi pekee ya Kleist
Hawakujua Wazaramo waliwakataa wazulu miaka mingi tu na kwamba uzulu na umanyema una harufu za kihalifu
Hawakujua kuwa Wazulu walikuja kuwapiga Watanganyika na hasa Waislam wakishirikiana na wakoloni

Orodha inaendea, nawahi Tengeni kuchukua nazi nikirudi nitaendelea
 
Nguruvi...
Nakusoma.
 
Nyerere alikuwa mjanja, isitoshe alitamani historia ingeandikwa in his favour kwamba ni yeye pekee katika nchi hii ndiye aliyedai uhuru.
Tena alikuwa mjanja sanahakutaka hata kuandika '' historia au wasifu wake'' mwenyewe kama alivyofanya Mkapa. Nyerere alijua Historia itaandikwa tu na hakuna jinsi.
Sasa mheshimiwa, tuonyeshe basi huyu Abdul katenda nini kikubwa katika nyanja za siasa?
 
Nguruvi..
Hana moja alilofanya kaka.

Mimi ni Irving Wallace naandika riwaya utasema kweli.
 
Aisee. Huu ndiyo mjadala sasa. Asante kwa kutufungua macho. Eti kitabu kilitikisa. So what? Hata Mein Kempf si ilitikisa? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 


Kama umeshindwa kumuelewa Mohamed said, historian, utanielewa mimi??!!
 
Tumefika huku kote kwa sababu ya Mzee Said. Laiti kama angezileta hizi historia za Wazee hawa bila ajenda fiche kila kitu kingebaki sawa.

Kila Mtu abaki na heshima yake kwa mchango wake lakini kamwe mambo yasipindishwe maana yanaibua hasira za wengine.
 
Aisee. Huu ndiyo mjadala sasa. Asante kwa kutufungua macho. Eti kitabu kilitikisa. So what? Hata Mein Kempf si ilitikisa? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Shimba...
Yawezekana kitabu cha Hitler kilishtua watu.

Kitabu cha Abdul Sykes mtikisiko wake ulikuwa tofauti.

Watu walitambua kuwa historia iliyokuwa ikufundishwa siyo.
 
May Day,
Hakuna aliyedhalilishwa katika kitabu changu.

Wahariri wasingeruhusu kitu hicho.

Wahariri walikataa kutumia neno "kuibiwa," nilipoandika kuwa kuna nyaraka muhimu zimeibiwa ndani ya majalada yaliyokuwa Maktaba ya CCM Dodoma na National Archive.

Wakabadili ikawa "hazionekani."

Baada ya utafiti niliandika kuhusu nyaraka za taifa zilizopotea.
 
Huna lolote wee muddy. You are so full of yourself, kama tumbo lilojaa ushuzi. Hapa JF unapapenda sababu unapata angalau a semblance of an audience, lkn its clear 99.9 % of the contributors here are firmly against your biased, divisive, hogwash. Huna credentials za kuwa Mwanazuoni wa somo la Historia chuo chochote duniani hata Chuo Kikuu cha Kiislamu Tanzania kule Morogoro. Umebaki kuwa one-man show, kutwa kushinda JF kutafuta wasomaji wa “tall tales” zako aka porojo ulizosimuliwa na Wazee wako wa Kariakoo.
 
Kipengele namba 5 kinachohusu ukatibu wa chama Tabora sijaelewa. Na ni lini alichaguliwa kuwa katibu?
 
Hajawahi jitokeza mtu hata mmoja jukwaa hili ambaye amewahi soma kitabu chako, but yey unadai “kilitolisa’. Umeishia kukipigia debe kila posting but still nobody’s interested in paying 2 cents for essentially a waste of paper and nothing more than a compendium of lies and half- truths.
 
Hahaha...Umbea Mtupu huu

Jisikie Aibu Mzee mzima kuandika Uongo.
 
Kipengele namba 5 kinachohusu ukatibu wa chama Tabora sijaelewa. Na ni lini alichaguliwa kuwa katibu?
Akida..
Soma hapo chini:
Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais) M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika. Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Mary's School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama.

Imechanganywa AA na TANU nadhani alikusudia AA.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes).
 
Sema yote lakini hilo ndilo jambo wapinga ukweli wa historia wasingependa kulisikia.

juu ya yote, don't fear anything for the truth as a truth sets one free.
Nyie kulialia na kulalamika ndio jadi yenu
 
Nyie kulialia na kulalamika ndio jadi yenu


Hata Yesu alilia na kulalamika msalabani:- Eloi Eloi lamasabchtan.

Yaani; Ewe Mungu, ewe Mungu mbona waniacha.

Kama Yesu pamoja na utukufu na ukubwa wake wote alimlilia Mungu, vipi mimi mtu hohehahe nishindwe kulia???!!!.
 
M...
Zamani nikiandika tanzia. Abdilatif Abdallah mtaalamu wa Kiswahili akaniambia hicho ni Kiswahili cha bara.

Sisi watu wa pwani tunasema "taazia," kwa kuwa neno lenyewe asili yake ni Kiarabu.
Kwa kiarabu lina maana gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…