Kati ya dhambi kubwa hapa duniani, ni dhambi ya kumsingizia marehemu, haisameheki!.
Huu urongo wa Abdul kumpokea Nyerere Dar es Salaam, ni urongo Mtakatifu wa mchana kweupe unaorudiwa na Mkuu Maalim Mohammed Said mara 100 ili uonekane ni ukweli!.
- Mwalimu Nyerere baada ya kumaliza Tabora School, amesoma St. Francis, Pugu, ni Dar es Salaam!, angalia ni mwaka gani, sio kuja kuongopa humu kuwa kuna Sykes ndio wamempokea Mwalimu Nyerere jijini DSM!.
- Baada ya Pugu, Mwalimu amekwenda Makekere, nchini Uganda na ameondokea Dar es Salaam na kurejea Dar es Salaam!, angalia ni mwaka gani?.
- Mwalimu Nyerere baada ya Makerere, amekwea pipa kwenda kusoma chuo kikuu cha Edinburgh nchini Uingereza!, hiyo ndege hakupandia Butiama!, alipandia Dar es Salaam!.
- Mwalimu amerudi Kufundisha Pugu, aliingilia Dar es Salaam na kuondokea Dar es Salaam.
- Mwalimu ndio alikuwa Katibu wa TANU wa Tabora, alikuja Dar kuhudhuria Mkutano Mkuu wa TAA mwaka 1948 wala hakupokelewa na Sykes!.
Kitu ambacho ni kweli, baada ya Mwalimu kuacha ualimu na kukitumikia chama full time, ni kweli yeye na Mama Maria, waliishi nyumbani kwa Sykes na ni kweli waliwahifadhi na kuwasaidia kwa kipindi kifupi kabla ya kuhamia Magomeni.
Mwaka 1996, nilisimuliwa na mjane wa Sykes, Mama Daisy aliyekuwa akiishi pale Opposite California Dreamer, na nilipelekwa na mjukuu wake, Mwamvua Mlangwa.
Kitu ambacho namkubali sana Maalim Mohammed Said ni uwezo wake wa uandishi, na umahiri wa kusimulia, he is gifted, ana kipaji, na kufuatia kipaji hicho, ni mtu wa kuaminiwa, hivyo ana agenda fulani hivyo kutunga uongo na kuu craft vizuri kabisa na kuonekana kama ukweli ili tuu kuitimiza hiyo agenda!.
Niliwahi kutoa angalizo humu kumhusu mtu huyu!.
Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!.
Sasa ni jana tuu tumetoka kumpumzisha Mkapa, hata siku 3 kaburini bado, leo anakuja kumzushia haya, tena kwa kutumia lugha ya kifedhuli kama hii
Wewe Mkuu Maalim Mohammed Said ni mtu wa kutumia maneno haya kumzungumzia Mkapa?!, "Mwandishi mpumbavu peke yake ndiye anaeweza kuchagua uamuzi wa kijinga kama huu.
Benjamin Mkapa hakuwa mtu zuzu".
I think this is too much!.
Thanks God, Mkuu Maalim Mohammed Said ni mtu mwerevu anayejua vyema kusoma nyakati, anamjua vizuri JPM, naamini anazijua vyema sababu zilizopelekea "wale jamaa" waendelee kuhifadhiwa kule 'mahali salama', hivyo tangu baada ya kumtolea angalizo lile, sasa yuko makini kwa kupunguza kuipush ile agenda yake ambayo ndio the motive behind most of his writings, na by the time 'jamaa' anamaliza, "if at all atamaliza", the time left will be too little too late to keep pushing his agenda forward!.
Paskali