...Kwa mujibu wa maelezo ya wakala wake Damas Ndumbaro, Haruna alikatisha mkataba wake na hiyo timu aliyokuwa akichezea huko Sweden kwa sabau kubwa mbili 1. Haoni kama kuna maslahi kuendelea kuichezea hiyo timu kwa nikipato apatacho kwa mtazamo wake ni kidogo 2. Kiwangi cha soka sweden haoni kama ni cha ushindani ingawa kuna maelezo kuwa hiyo timu ime-qualify kucheza kombe la ulaya????!!!!
Lakini kwa maoni yangu nilichoona kwa upande wa Haruna ni upeo mdogo wa kujua mambo na pia kukosa dhamira ya kucheza soka la ushindani. Haruna yeye hataki kukatwa kodi kwenye mshahara wake (pay as you earn), alitafutiwa nyumba lakini akatakiwa alipie kodi mwenyewe.
Nimegundua wachezaji wetu wengi wa soka wana akili finyu sana (sitaki kuzungumzia elimu hapa) maana kama ni elimu akina George Weah walipiga soka ulaya na hawakuwa na elimu sana au akina Kanu, Toure. isipokuwa wanakosa dhamira ya kweli kutaka kucheza soka ulaya na pia kukosa malengo. Hivi kwa timu kuweza kupata tiketi ya kucheza ubingwa wa ulaya si ndio ilikuwa njia ya yeye kuonyesha umahili wake ili aonekane na hatimaye kupata timu kubwa zaidi na hatimaye kupata mkataba wenye maslahi zaidi??
Kwa hiyo Haruna ameona bora kurudi simba...Kweli akilini nywele!!!
:frusty::frusty: