Nini kilitokea katika " Big Bang " ?

Nini kilitokea katika " Big Bang " ?

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
28,481
Reaction score
28,749
Sayansi ina habari nyingi sana,na vimbwanga kadha wa kadha. Sasa kuna maswali nataka kuuliza juu ya suala la Big Bang.

1. Nataka nipewe uthibitisho wa tukio hili kama kweli lilitokea. Na kama lilitokea,swali la pili linafata kutokana na na tukio hilo.

2. Kabla ya Big Bang kutokea,hali ilikuwaje ?

3. Mchakato wa maumbile ulikuwaje kuwaje baada ya tukio hilo kutokea ?

4. Nini kilisababisha Big Bang kutokea ?

Nitafurahi sana nikipatiwa majibu ya maswali yangu.
 
Mlipuko mkuu au mlipuko asilia (kwa Kiingereza Big Bang ) ni nadharia ya ki sayansi kuhusu chanzo cha
ulimwengu inayojaribu kueleza sababu ya kutokea kwa nyota , magalaksi na anga kwa jumla jinsi tunavyoviona leo.
Kutokea kwa ulimwengu
Kufuatana na nadharia hii ulimwengu ulitokea mahali pamoja padogo sana penye joto na densiti kubwa, pasipo na nyota wala atomi wala umbo lolote. Hali hiyo inaelezwa ilikuwa ya pekee.
Takriban miaka bilioni 14 iliyopita [1] anga la ulimwengu lilianza kupanuka haraka na katika
mchakato huo atomi ziliundwa zilizoendelea kujenga
mata tunavyoijua na kuwa nyota na magalaksi.
Ulimwengu unaendelea bado kupanuka na wakati huohuo kupoa. Nafasi ya ulimwengu inapanuka na katika mwendo huu halijoto inapungua.
Jina
Jina la "Big Bang" lilibuniwa na mwanafizikia Fred Hoyle aliyepinga nadharia hii, lakini wengine walioitetea walipenda jina, hivyo likabaki. [2]
Athari ya Doppler na mlipuko mkuu
Sababu za kubuni nadharia ya mlipuko mkubwa ni kutafuta maelezo kwa vipimo vinavyopatikana kuhusu anga la ulimwengu.
Sababu muhimu zaidi ni mabadiliko ya nuru ya galaksi ambazo zinaonekana kuwa mbali sana. Nuru hiyo inasogea kwa upande wa nyekundu zaidi katika spektra yake. Huu msogeo wekundu (ing.
redshift ) wa nuru ya nyota za mbali huelezwa kwa
athari ya Doppler . Maana yake ni kwamba, kama kitu kinaelekea kwenda mbali nasi, rangi yake huelekea kuwa nyekundu zaidi kwa sababu mwendo wake hupanusha masafa ya mawimbi ya nuru. Nyekundu ina urefu mkubwa zaidi kati ya mawimbi ya nuru ya rangi zinazoonekana. Kadiri jinsi mwelekeo mwekundu unavyoongezeka vile, kitu kina mwendo wa haraka zaidi kuelekea mbali nasi.
Dalili nyingine ni mnururisho wa mandharinyuma (ing. cosmic background radiation ) uliowahi kutabiriwa kinadharia na wanafizikia tangu miaka ya 1930. Iligunduliwa na kuthebitishwa kwa njia ya vipimo tangu mwaka 1964. Huu ni mnururisho dhaifu sana usio na asili katika nyota au galaksi yoyote; leo hii wanasayansi wengi wanaiona kama mabaki ya nishati wa mlipuko mkuu inayoendelea kijaza ulimwengu.
Kutokana na vipimo hivyo wanasayansi wengi kabisa wa fizikia na astronomia wanaona ya kuwa nadharia ya mlipuko asilia inaeleza vizuri zaidi vipimo vinavyopatikana kuhusu ulimwengu. [3]
Nadharia hii inaonekana pa kupatana na makadirio kuhusu viwango vya elementi vya ki kemia vinavyogunduliwa katika anga la ulimwengu.
Kuna tofauti ya mawazo kama mlipuko mkuu ulikuwa chanzo kabisa cha ulimwengu au kama uliwengu mwingine ulikuwepo kabla yake, na labda mwendo wa kupanuka unaweza kurudishwa katika mwendo wa kukaza siku moja hadi mata yote kuwa mahali pamoja na kulipuka tena. [3]
Falsafa na dini
Nadharia hii ina umuhimu pia kwa falsafa na dini , ambazo pia zinaeleza chanzo cha ulimwengu, k.mf. kwa kusema umeumbwa na Mungu .
Kuna wafuasi wa dini mbalimbali wanaopinga nadharia hiyo wakiona hailingani na imani yao. [4]
Kinyume chake wako wengine wanaosema kuwa nadharia ya mlipuko mkubwa inalingana vema na
hoja ya uumbaji unaoendelea kupitia sheria za maumbile zinazozidi kugunduliwa na sayansi .
Mwanzilishi mwenyewe wa nadharia hiyo alikuwa
Georges Lemaitre (1894 - 1966 ), padre wa Kanisa Katoliki kutoka Ubelgiji . Ndiye aliyependekeza nadharia hiyo mwaka 1927 , akifuatwa na wengine wengi zaidi na zaidi.
Kwa mtazamo wa padri huyo na Wakristo wengine kadhaa ni kwamba si lazima kusadiki masimulizi ya
Biblia kuhusu uumbaji yanaeleza matukio kihistoria au kisayansi, bali yanadai msomaji akubali kuwa
asili ya vitu vyote vilivyopo ni Muumba.
Hata sayansi inafundisha kuwa mata haiwezi kujianzisha. Kama ipo, ni lazima iwe na asili nje yake.
 
Zurri, post: 28313732, member: 483599"]Sayansi ina habari nyingi sana,na vimbwanga kadha wa kadha. Sasa kuna maswali nataka kuuliza juu ya suala la Big Bang.

1. Nataka nipewe uthibitisho wa tukio hili kama kweli lilitokea. Na kama lilitokea,swali la pili linafata kutokana na na tukio hilo.

Big Bang ilitokea,Kuanza kwa big bang ni kama vile unapoamka kutoka usingizini,Unakuwa totally assleep with no consciusness kisha bang unaamka.Uthibitisho wakwamba big bang ilitokea ni universality of natural elements-zote zimeundwa kwa Atoms zenye protons na neutrons na kwamba idadi ya protons,neutrons na electrons ndio inatofautisha elements tofauti and hence matter.Kama unakubaliana nanchochote kati ya nilivosema hapo basi unakubali kwamba Big bang ilitokea

2. Kabla ya Big Bang kutokea,hali ilikuwaje ?
Kabla ya big bang all wa still and calm letsay there was only emptyness/ utupu/ukiwa yaani nothing had taken form,everything formless which simply means unstable and unstable things keep changing untill they find stability that is when they start taking form.So before big bang the universe was unstable,volatile,everchanging,empty

3. Mchakato wa maumbile ulikuwaje kuwaje baada ya tukio hilo kutokea ?
All that was needed was stability,balance,and everything that came out of the Big bang had one purpose to create stability humans included.And the cycle continues to maintain that stability and the universe will end if that stability comes to an end

4. Nini kilisababisha Big Bang kutokea ?
Kama nilivosema the universe was unstable so as usual unstable things will keep looking for stability and at one point and time will find it and hence the cause of the big bang was the unstability of the universe
Nitafurahi sana nikipatiwa majibu ya maswali yangu.

Tuendelee
 
hivi ni kwamba ukuweza kujibu kwa lugha ya muuliza swali...
Au mkitaka kudanganya ndio huwa mnaongea kingereza
 
Achana nao hao wakuze Teknokojia Maana mengne hawana uwezo navyo
 
Back
Top Bottom