Nini kimejificha kwenye Uteuzi wa Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu? Nini maana yake kihistoria na upi mwelekeo wa Nchi baada ya Uteuzi huu?

Baada ya kufatilia mjadala huu kwa ukaribu Sana na kuona wengi Wakitoa Presidential Decree mbalimbali zinazolindwa na katiba nimeona sio vibaya kama na mimi nitakuja na Historia kwa sababu historia huwa haidanganyi na ndio suluhisho
Maandiko ni marefu, hayana maana yoyote.

Reconciliation.
Resiliency.
Reform.
Rebuilding.

Ukizielewa falsafa zake hutopata shida ya kuumiza kichwa bila sababu.
 
Fafanua vizuri huo mstari mimi unanichanganya
Ok ngoja niende pole pole ili unielewe Mwaka 1985 October Rais wa Jamhuri ya Muungano Mwl J.K.Nyerere Alitangaza kung'atuka na kuachia nchi....

Kipindi hicho Ali hassani Mwinyi alikuwa amechaguliwa kuwa Rais wa Tatu wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Kitendo cha Mwinyi kuwa Rais wa zanzibar kilimpa Cheo kikatiba kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba kabla ya marekebisho (Kipindi hicho katika ikiwa ni ya chama kimoja)

Baada ya Nyerere kung'atuka Mwinyi alichaguliwa kuchukua nafasi ya Urais wa Tanzania na kuachia Nafasi aliyokuwa nayo ya Urais wa zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Mh Idris Abdul Wakil ambaye ndo alikuwa Rais wa 3 wa zanzibar.....

Tuanze na hapo mkuu sijui umenielewa????
 
Maandik9 n arefu, hayana maanabyoyote.

Reconciliation.
Resiliency.
Reform.
Rebuilding.

Ukizielewa falsafa zake hutopata shida ya kuumiza kichwa bila sababu.
Ok nazielewa zote hizo...
Ila unafikri Why now...
Na unafikiri kwanini kila hii nafasi ikitokea huja na changamoto ambayo hujitokeza ndani ya serkali na nafasi hii huwa kama Ni njia ya Serkali kurekebisha changamoto (Kwa mujibu wa Historia)
 
Ok nazielewa zote hizo...
Ila unafikri Why now...
Na unafikiri kwanini kila hii nafasi ikitokea huja na changamoto ambayo hujitokeza ndani ya serkali na nafasi hii huwa kama Ni njia ya Serkali kurekebisha changamoto (Kwa mujibu wa Historia)
Vitu mbona vipo wazi, ukimtazama tu Majaliwa anaonesha kuwa hayupo sawa kiafya.

Tujikumbushe, siku hii ndipo Majaliwa alianza kudhoofika:

Your browser is not able to display this video.
 
Vitu mbona vipo wazi, ukimtazama tu Majaliwa anaonesha kuwa hayupo sawa kiafya.

Tujikumbushe, siku hii ndipo Majaliwa alianza kudhoofika:

View attachment 2734901
Kwa mujibu wa video shida kubwa ya Waziri mkuu ni kupata Homa ya Uchaguzi 2025 (2025 Fever), Na kingine kilichotajwa ni serkali ya Mpito...

Sasa Katiba iko Wazi kwamba kama Waziri mkuu atashindwa kumudu Majukumu yake kwa ugonjwa kiafya (Kama ulivyosema)

Angetengua uteuzi wake akateua mwingine au kama kingekuwa kigumu kwake Angetumia Kipengele Katiba Ibara 53(A) na kupeleka pendekezoK wa wabunge wake yeye kama mwenyekiti wa CCM waomba hati ya dharura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu hivyo kuacha Bunge kutengua uteuzi wa WMkuu...

Au njia hiyo ilikuwa pia ngumu??

CC; FaizaFoxy
 
DR Mambo AMP,, umeandika vizuri lakini umebabaika, hapa nakusahihisha

(awamu ya kwanza) Rais wa Zanzibar ni Abeid Aman Karume, Januari 13, 1964 - Aprili 7, 1972 (awamu ya pili) Aboud Jumbe Mwinyi, Aprili 11, 1972 - Januari 29, 1984 (awamu ya tatu) Ali Hassan Mwinyi, Januari 30, 1984 - Oktoba 24, 1985) (awamu ya nne) Rais wa Zanzibar, Idris Abdul-Wakali Nombe, Oktoba 24, 1985 - Oktoba 25, 1990.

Zanzibar huko huko, ndipo baadae walifuata akina Dk Salmin Amour Komando, awamu ya 5 - Aman Abeid Karume 'Karume Junior' awamu ya 6 - Dk Ali Mohamed Shein, awamu ya 7 na Dk Hussein Mwinyi 'Mwinyi 'Junior' - awamu ya 8..
 
Hapana, hiyo haikuwa kwa waziri mkuu, hiyo ilikuwa kwa Ndugai, lakini majaliwa ujumbe ulimfikia.

Gang lile lile ni kubwa sana, mama alifanya vizuri kulikata makali mdogo mdogo.
 
Dah shukrani sana Nilikuwa nimesahau kidogo kuhusu Aboid Jumbe nashukuru Kunielewesha
 
Hapana, hiyo haikuwa kwa waziri mkuu, hiyo ilikuwa kwa Ndugai, lakini majaliwa ujumbe ulimfikia.

Gang lile lile ni kubwa sana, mama alifanya vizuri kulikata makali mdogo mdogo.
Ila naona bado lipo Sana Hili genge na ndo linaloshirikiana na Wapinzani kutaka kumdondosha..
we unafikir Wapinzani wanapata wapi Profile na Information nyeti namna hiyo ambazo zipo ndani ya serikali..

Na limeweka Mizizi Mpaka kwenye TISS na ndo maana mama Kampa Ubalozi Yule mkubwa wa TISS Alikuwa Pandikizi
 
Dah shukrani sana Nilikuwa nimesahau kidogo kuhusu Aboid Jumbe nashukuru Kunielewesha
Hata kwa Dk Salim 'you are wrong' tatizo kwa sasa sina muda wa kutosha

Kwa muhtasari, Dk Salim amekuwa waziri mkuu baada ya kifo cha Edward Moringe Sokoine kilichotokea baina ya Morogoro na Dar es Salaam, saa 11: 46 jioni Alhamisi, Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari 'Morogoro Road.'

Kuliibuka madaia ya baadhi ya watu waliohusisha tukio hilo la ajali na njama dhidi ya kiongozi huyo, aliyetokea kupendwa sana na watu wa watanganyika hadi kuonekana kumfunika Nyerere.

Dk Salim, aliteuliwa na Nyerere kuwa waziri mkuu kufuatia kifo cha Sokoine. Alishika wadhifa huo kwa kipindi kifupi sana, takriban kama miaka miwili.

Uchaguzi Mkuu wa 1995 uliomleta madaraka Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Tanzania, Dk Salim ilibidi asiendelee na cheo hicho ingawa alionekana kufit yaani, kuimuda mno nafasi hiyo.

Ali Hassan Mwinyi (Rais wa awamu ya pili) alichukuliwa kwamba ni Mzanzibari, ilhali hakuwa mzanzibari hata chembe hata wa kujiandikisha ni mzaramo wa Mkuranga, Tanganyika.

Mwinyi alipelekwa Zanzibar kusoma dini kama alivyoeleza mwenyewe kwenye kitabu chake. CCM hasa Nyerere, ndio waliompachi (waliombatiza) Uzanzibari.

Kwa mnasaba huo kwamba Mwinyi ni Mzanzibari, ikaonekana waziri mkuu awe Mtanganyika ndipo alipoteuliwa Warioba na ndipo kilipobuniwa cheo cha Naibu Waziri Mkuu kwa ajili ya kumfuta machozi Dk Salim au niseme alipewa kama zawadi. Lilikuwa wazo la Nyerere.

Kumuondoa Dk Salim katika uwaziri mkuu na kumrudisha katika uwazi wa kawaida, ilionekana itatoa picha mbaya, ni kumdhalilisha au nikumshushia heshima na utu. Dk Salim aliheshimiwa sana ndani na nje ya Tanzania.

Hicho ndio chanzo cha Dk Salim kuwa waziri wa kawaida na wakati huo huo kuwa Naibu Waziri Mkuu.

Waswahili wana msemo: 'uso umeumbwa na haya' Nyerere alimpenda sana Dk Salim, hakupenda kumdogosha, aliona aibu kumshusha.

Kuhusu Samia Suluhu kwa kuanzisha tena cheo cha Naibu Waziri Mkuu kwa sasa ambapo nchi imejaa viongozi watupu kila kona, namchukulia kuwa ni rais anayebabaika, bila kujua anachokifanya.

Sidhani kuwa kuna tija yoyote kwa watanganyika, kuwapo na naibu waziri mkuu, isipokuwa gharama za uendeshaji wa nchi, basi..
 
Hata kwa Dk Salim 'you are wrong' tatizo kwa sasa sina muda wa kutosha
Mkuu ulisoma vizuri nilichoandika Kuhusu Dr Salim Ahmed Salim Nafikiri Umerudia Nilichoandika kumuhusu sema sikuzungumzia Kuhusu Ajali ya sokoine...

Ila kuhuus Waziri Mkuu Kuwa Ahmed salim baada ya sokoine Nafikir Nimelisema na nimesema chote ulichosema nashangaa unasema Am wrong...Wakati unarudia kile kile nilichosema 🤣🤣
 
Duh! Kiukweli sijaelewa chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…