Nini kimejificha kwenye Uteuzi wa Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu? Nini maana yake kihistoria na upi mwelekeo wa Nchi baada ya Uteuzi huu?

Nini kimejificha kwenye Uteuzi wa Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu? Nini maana yake kihistoria na upi mwelekeo wa Nchi baada ya Uteuzi huu?

Baada ya kufatilia mjadala huu kwa ukaribu Sana na kuona wengi Wakitoa Presidential Decree mbalimbali zinazolindwa na katiba nimeona sio vibaya kama na mimi nitakuja na Historia kwa sababu historia huwa haidanganyi na ndio suluhisho
Maandiko ni marefu, hayana maana yoyote.

Reconciliation.
Resiliency.
Reform.
Rebuilding.

Ukizielewa falsafa zake hutopata shida ya kuumiza kichwa bila sababu.
 
Fafanua vizuri huo mstari mimi unanichanganya
Ok ngoja niende pole pole ili unielewe Mwaka 1985 October Rais wa Jamhuri ya Muungano Mwl J.K.Nyerere Alitangaza kung'atuka na kuachia nchi....

Kipindi hicho Ali hassani Mwinyi alikuwa amechaguliwa kuwa Rais wa Tatu wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Kitendo cha Mwinyi kuwa Rais wa zanzibar kilimpa Cheo kikatiba kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba kabla ya marekebisho (Kipindi hicho katika ikiwa ni ya chama kimoja)

Baada ya Nyerere kung'atuka Mwinyi alichaguliwa kuchukua nafasi ya Urais wa Tanzania na kuachia Nafasi aliyokuwa nayo ya Urais wa zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Mh Idris Abdul Wakil ambaye ndo alikuwa Rais wa 3 wa zanzibar.....

Tuanze na hapo mkuu sijui umenielewa????
 
Maandik9 n arefu, hayana maanabyoyote.

Reconciliation.
Resiliency.
Reform.
Rebuilding.

Ukizielewa falsafa zake hutopata shida ya kuumiza kichwa bila sababu.
Ok nazielewa zote hizo...
Ila unafikri Why now...
Na unafikiri kwanini kila hii nafasi ikitokea huja na changamoto ambayo hujitokeza ndani ya serkali na nafasi hii huwa kama Ni njia ya Serkali kurekebisha changamoto (Kwa mujibu wa Historia)
 
Vitu mbona vipo wazi, ukimtazama tu Majaliwa anaonesha kuwa hayupo sawa kiafya.

Tujikumbushe, siku hii ndipo Majaliwa alianza kudhoofika:

Vitu mbona vipo wazi, ukimtazama tu Majaliwa anaonesha kuwa hayupo sawa kiafya.

Tujikumbushe, siku hii ndipo Majaliwa alianza kudhoofika:

View attachment 2734901
Kwa mujibu wa video shida kubwa ya Waziri mkuu ni kupata Homa ya Uchaguzi 2025 (2025 Fever), Na kingine kilichotajwa ni serkali ya Mpito...

Sasa Katiba iko Wazi kwamba kama Waziri mkuu atashindwa kumudu Majukumu yake kwa ugonjwa kiafya (Kama ulivyosema)

Angetengua uteuzi wake akateua mwingine au kama kingekuwa kigumu kwake Angetumia Kipengele Katiba Ibara 53(A) na kupeleka pendekezoK wa wabunge wake yeye kama mwenyekiti wa CCM waomba hati ya dharura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu hivyo kuacha Bunge kutengua uteuzi wa WMkuu...

Au njia hiyo ilikuwa pia ngumu??

CC; FaizaFoxy
 
Ok ngoja niende pole pole ili unielewe Mwaka 1985 October Rais wa Jamhuri ya Muungano Mwl J.K.Nyerere Alitangaza kung'atuka na kuachia nchi....

Kipindi hicho Ali hassani Mwinyi alikuwa amechaguliwa kuwa Rais wa pili wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Kitendo cha Mwinyi kuwa Rais wa zanzibar kilimpa Cheo kikatiba kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba kabla ya marekebisho (Kipindi hicho katika ikiwa ni ya chama kimoja)

Baada ya Nyerere kung'atuka Mwinyi alichaguliwa kuchukua nafasi ya Urais wa Tanzania na kuachia Nafasi aliyokuwa nayo ya Urais wa zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Mh Idris Abdul Wakil ambaye ndo alikuwa Rais wa 3 wa zanzibar.....

Tuanze na hapo mkuu sijui umenielewa????
DR Mambo AMP,, umeandika vizuri lakini umebabaika, hapa nakusahihisha

(awamu ya kwanza) Rais wa Zanzibar ni Abeid Aman Karume, Januari 13, 1964 - Aprili 7, 1972 (awamu ya pili) Aboud Jumbe Mwinyi, Aprili 11, 1972 - Januari 29, 1984 (awamu ya tatu) Ali Hassan Mwinyi, Januari 30, 1984 - Oktoba 24, 1985) (awamu ya nne) Rais wa Zanzibar, Idris Abdul-Wakali Nombe, Oktoba 24, 1985 - Oktoba 25, 1990.

Zanzibar huko huko, ndipo baadae walifuata akina Dk Salmin Amour Komando, awamu ya 5 - Aman Abeid Karume 'Karume Junior' awamu ya 6 - Dk Ali Mohamed Shein, awamu ya 7 na Dk Hussein Mwinyi 'Mwinyi 'Junior' - awamu ya 8..
 
Kwa mujibu wa video shida kubwa ya Waziri mkuu ni kupata Homa ya Uchaguzi 2025 (2025 Fever), Na kingine kilichotajwa ni serkali ya Mpito...

Sasa Katiba iko Wazi kwamba kama Waziri mkuu atashindwa kumudu Majukumu yake kwa ugonjwa kiafya (Kama ulivyosema)

Angetengua uteuzi wake akateua mwingine au kama kingekuwa kigumu kwake Angetumia Kipengele Katiba Ibara 53(A) na kupeleka pendekezoK wa wabunge wake yeye kama mwenyekiti wa CCM waomba hati ya dharura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu hivyo kuacha Bunge kutengua uteuzi wa WMkuu...

Au njia hiyo ilikuwa pia ngumu??

CC; FaizaFoxy
Hapana, hiyo haikuwa kwa waziri mkuu, hiyo ilikuwa kwa Ndugai, lakini majaliwa ujumbe ulimfikia.

Gang lile lile ni kubwa sana, mama alifanya vizuri kulikata makali mdogo mdogo.
 
DR Mambo AMP,, umeandika vizuri lakini umebabaika, hapa nakusahihisha

(awamu ya kwanza) Rais wa Zanzibar ni Abeid Aman Karume, Januari 13, 1964 - Aprili 7, 1972 (awamu ya pili) Aboud Jumbe Mwinyi, Aprili 11, 1972 - Januari 29, 1984 (awamu ya tatu) Ali Hassan Mwinyi, Januari 30, 1984 - Oktoba 24, 1985) (awamu ya nne) Rais wa Zanzibar, Idris Abdul-wakati Nombe, Oktoba 24, 1985 - Oktoba 25, 1990.

Zanzibar huko huko, ndipo baadae walifuata akina Dk Salmin Amour Komando, awamu ya 5 - Aman Abeid Karume 'Karume Junior' awamu ya 6 - Dk Ali Mohamed Shein, awamu ya 7 na Dk Hussein Mwinyi 'Mwinyi 'Junior' - awamu ya 8..
Dah shukrani sana Nilikuwa nimesahau kidogo kuhusu Aboid Jumbe nashukuru Kunielewesha
 
Hapana, hiyo haikuwa kwa waziri mkuu, hiyo ilikuwa kwa Ndugai, lakini majaliwa ujumbe ulimfikia.

Gang lile lile ni kubwa sana, mama alifanya vizuri kulikata makali mdogo mdogo.
Ila naona bado lipo Sana Hili genge na ndo linaloshirikiana na Wapinzani kutaka kumdondosha..
we unafikir Wapinzani wanapata wapi Profile na Information nyeti namna hiyo ambazo zipo ndani ya serikali..

Na limeweka Mizizi Mpaka kwenye TISS na ndo maana mama Kampa Ubalozi Yule mkubwa wa TISS Alikuwa Pandikizi
 
Dah shukrani sana Nilikuwa nimesahau kidogo kuhusu Aboid Jumbe nashukuru Kunielewesha
Hata kwa Dk Salim 'you are wrong' tatizo kwa sasa sina muda wa kutosha

Kwa muhtasari, Dk Salim amekuwa waziri mkuu baada ya kifo cha Edward Moringe Sokoine kilichotokea baina ya Morogoro na Dar es Salaam, saa 11: 46 jioni Alhamisi, Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari 'Morogoro Road.'

Kuliibuka madaia ya baadhi ya watu waliohusisha tukio hilo la ajali na njama dhidi ya kiongozi huyo, aliyetokea kupendwa sana na watu wa watanganyika hadi kuonekana kumfunika Nyerere.

Dk Salim, aliteuliwa na Nyerere kuwa waziri mkuu kufuatia kifo cha Sokoine. Alishika wadhifa huo kwa kipindi kifupi sana, takriban kama miaka miwili.

Uchaguzi Mkuu wa 1995 uliomleta madaraka Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Tanzania, Dk Salim ilibidi asiendelee na cheo hicho ingawa alionekana kufit yaani, kuimuda mno nafasi hiyo.

Ali Hassan Mwinyi (Rais wa awamu ya pili) alichukuliwa kwamba ni Mzanzibari, ilhali hakuwa mzanzibari hata chembe hata wa kujiandikisha ni mzaramo wa Mkuranga, Tanganyika.

Mwinyi alipelekwa Zanzibar kusoma dini kama alivyoeleza mwenyewe kwenye kitabu chake. CCM hasa Nyerere, ndio waliompachi (waliombatiza) Uzanzibari.

Kwa mnasaba huo kwamba Mwinyi ni Mzanzibari, ikaonekana waziri mkuu awe Mtanganyika ndipo alipoteuliwa Warioba na ndipo kilipobuniwa cheo cha Naibu Waziri Mkuu kwa ajili ya kumfuta machozi Dk Salim au niseme alipewa kama zawadi. Lilikuwa wazo la Nyerere.

Kumuondoa Dk Salim katika uwaziri mkuu na kumrudisha katika uwazi wa kawaida, ilionekana itatoa picha mbaya, ni kumdhalilisha au nikumshushia heshima na utu. Dk Salim aliheshimiwa sana ndani na nje ya Tanzania.

Hicho ndio chanzo cha Dk Salim kuwa waziri wa kawaida na wakati huo huo kuwa Naibu Waziri Mkuu.

Waswahili wana msemo: 'uso umeumbwa na haya' Nyerere alimpenda sana Dk Salim, hakupenda kumdogosha, aliona aibu kumshusha.

Kuhusu Samia Suluhu kwa kuanzisha tena cheo cha Naibu Waziri Mkuu kwa sasa ambapo nchi imejaa viongozi watupu kila kona, namchukulia kuwa ni rais anayebabaika, bila kujua anachokifanya.

Sidhani kuwa kuna tija yoyote kwa watanganyika, kuwapo na naibu waziri mkuu, isipokuwa gharama za uendeshaji wa nchi, basi..
 
Hata kwa Dk Salim 'you are wrong' tatizo kwa sasa sina muda wa kutosha
Mkuu ulisoma vizuri nilichoandika Kuhusu Dr Salim Ahmed Salim Nafikiri Umerudia Nilichoandika kumuhusu sema sikuzungumzia Kuhusu Ajali ya sokoine...

Ila kuhuus Waziri Mkuu Kuwa Ahmed salim baada ya sokoine Nafikir Nimelisema na nimesema chote ulichosema nashangaa unasema Am wrong...Wakati unarudia kile kile nilichosema 🤣🤣
 
Baada ya kufatilia mjadala huu kwa ukaribu Sana na kuona wengi Wakitoa Presidential Decree mbalimbali zinazolindwa na katiba nimeona sio vibaya kama na mimi nitakuja na Historia kwa sababu historia huwa haidanganyi na ndio suluhisho

Lini Hiki cheo kilikuwepo na watu walioteuliwa,Na nani kateuliwa haya huwa ndo maswali ya kwanza kabisa lakini swali kubwa na la Kiphilosophy na la kielimu sana huwa Why....

Why ni swali nililotegemea kwa Wananchi wengi kuuliza hasa Wanachama wa ccm wenyewe..

Why now wakati nchi ipo kwenye Minong'ono mingi na why now not in 10 years Ago,Why now and not in 20 years ago...
(Akili kichwani mwako sasa...)
Na kilikuwepo Tangu 1985 why hakikuendelea mpaka leo kiwe kinateuliwa kwenye wakati nchi ikIwa kwenye MPASUKO

Kama una Akili timamu lakini THEN LAZIMA UJIULIZE PIA....

Why Dr Ahmed salim Ahmed 1986 -1989

Why Augustino Mrema in 1993-1994

Why Dotto Bitteko in 2023

Mara nyingi Hawa Manaibu Waziri wakuu walikuwa wakiteuliwa pale nchi inapoonyesha kugawanyika vipande Huku mihimili ikikaa kimya nitatoa Ufafanuzi kwa kila mmoja hapo juu..

Ndo maana nikasema insteady ya kushabikia mnatakiwa kusali kuomba Mungu kama ndicho ninachokiwaza basi Nchi inaelekea kubaya....

Tatizo vijana wa siku hizi wavivu sana kusoma Historia wao ni kushinda mitandaoni na kufata Jamii au watu wao wanacho amini bila kufata ukweli wa Jambo lenyewe..

SASA NAOMBA MNIAZIME MUDA WENU NIFAFANUE....

Why Dr Ahmed salim Ahmed 1986 -1989

Dr Salim A. Salim alikuwa waziri wa ulinzi, na naibu waziri mkuu, wakati wa awamu ya kwanza ya mzee Mwinyi,Na sio nyerere kama watu wanavyosema

Kipindi hicho joseph warioba alikuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa raisi.

Kumbuka kuwa Salim Salim ndiyo alichukua nafasi ya Edward Sokoine ambaye alifariki akiwa waziri mkuu.

Kipindi Salim akiwa waziri mkuu, Nyerere alikuwa Raisi, na Mwinyi alikuwa raisi wa ZNZ na makamu wa muungano.

Mwinyi alilazimika kuteua waziri mkuu toka bara baada ya kuchukua madaraka toka kwa Mwalimu Nyerere. Katiba ilikuwa inaelekeza kwamba ikiwa Raisi atatoka ZNZ basi waziri mkuu atatokea Tanganyika na ndiye atakayekuwa makamu wa kwanza wa raisi wa muungano.

..katika mazingira hayo, Joseph Warioba, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, aliteuliwa kuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa raisi.
Salim Salim aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi.

sasa hii ndo situation Ilivyokuwa kwa Usalama wa Nchi Ilikuwa ni Lazima Kufanya hivyo ili Kuepusha migogoro Nchini......

Why Augustino Mrema in 1993-1994

Nafikiri Wengi wenu Mnaweza mkaelewa Situation Ya Mrema Ilivyokuwa kipindi hicho mpaka Kuteuliwa kuwa NW mkuu..

Naanza na hansard za Bunge, June 24, mwaka wa 2011, Mhe. A. Mrema, (TLP, Vunjo) ambae alikuwa analalamika bungeni kwamba hajapewa mafao yake ya Unaibu Waziri Mkuu .

Hansard, Bunge la Jamhuri: "Mheshimiwa Mwenyekiti... ukiacha kazi utapewa asilimia 80 ya mafao yako ya mshahara wako, nipeni basi hata asilimia 20. Mnasema hiki cheo changu hakikuwa kwenye Katiba, Rais ndiye anaanzisha cheo. Hata Mawaziri wetu wanaanzishwa kwa decree ya Rais. Ilikuwaje cheo ambacho Mwalimu Nyerere alianzisha, akasimamia akakaa pale Dkt. Salum Ahmed Salum, Naibu Waziri Mkuu wa pili Agustino Lyatonga Mrema."

mrema aliteuliwa naibu waziri mkuu katikati ya kipindi cha uwaziri mkuu wa cygwiyemisi malecela, kulitokea malalamiko toka kwa mawaziri wenzake kwamba mrema anawaingilia ktk majukumu yao. sasa ili kuzima malalamiko hayo raisi mwinyi akaona amteue kuwa naibu waziri mkuu.

Malalmiko yalizidi kuwa anaingilia kazi zisizo zake nafikiri wengi wanakumbuka malumbano kati yake na mama Mary Chipsi Chipungahelo

Wakati Mrema ni waziri wa mambo ya ndani alikuwa anafanya mamaamuzi mengi kinyume na sheria hiyo ilisababisha apewe naibu waziri Jaji Mweisumo ili kuzuia serikali kuingia katika migogoro mengi ya kisheria.

SWALI KUBWA LA KUJIULIZA WHY MH BITTEKO NA WHY SASA
Kwa kupitia historia jiulize Why sasa ? nchi inapokuwa kwenye Minong'ono mingine na kutokea kutaka kugawanyika kuhusu Diiipii weedi na Nyaraka mbalimbali za kidini na kiserikali Why baada ya kubdilishwa kwa DG TISS why sasa ??

Nyerere aliwahi kuulizwa kuhusu hiki cheo Mwaka 1986 , aliulizwa, kwa nini kumeanzishwa cheo ambacho hakipo kwenye Katiba, akajibu, "Katiba haijasema awepo, wala haijakataza asiwepo..."

Huu utata unakuja kwa sababu sisi hatuna "enumerated powers doctrine" kwenye mfumo wa Katiba yetu, kama baadhi ya nchi, ambapo, kama kitu kwenye Katiba hakijasemwa kwamba kiwepo maana yake kimekatazwa!
Duh! Kiukweli sijaelewa chochote.
 
Back
Top Bottom