Nini kimekufurahisha au kukukwaza kwenye majukwaa ya JF toka mwaka 2025 uanze?

Nini kimekufurahisha au kukukwaza kwenye majukwaa ya JF toka mwaka 2025 uanze?

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Watu wanaokosa lugha za staha wananiuzi sana. Ila nyuzi zilizonifurahisha nikacheka sana in 2025 ni 👇 .

Mtu niliyemfurahia sana 2025 ni mzee mwenzangu Ushimen 🙈
 
Nyuzi za kububujisha machozi za Lucas Mwashambwa
Screenshot_20250310-114358~2.jpg
 
Hakijanichukiza Wala kunifurahisha ila ni kushangaza kua habari za maana zinazoibuliwa katika kuwaweka watanzania wawe macho na serikali yao zinapata engagement za watu wasiozidi 100, ila habari za kijinga za uswahili uswahili zisizo na kichwa Wala miguu zinapata engagement ya zaidi ya watu kuanzia maelfu na maelfu kwa idadi
 
Mimi huwa nachukizwa na watu wanaotumia haya maneno "huna akili au "wewe ni mjinga" na phrase nyingine za aina hiyo pale ambapo umeenda kinyume na hoja zao au umetoa hoja yako halafu hawajaipenda.

Tujifunze kutoa hoja jamani.
 
Hakijanichukiza Wala kunifurahisha ila ni kushangaza kua habari za maana zinazoibuliwa katika kuwaweka watanzania wawe macho na serikali yao zinapata engagement za watu wasiozidi 100, ila habari za kijinga za uswahili uswahili zisizo na kichwa Wala miguu zinapata engagement ya zaidi ya watu kuanzia maelfu na maelfu kwa idadi
Ni reflection ya jamii zetu na uhalisia wa mambo ulivyo. Hili ni eneo zuri sana la kufanyia utafiti ili kuelewa mienendo na mitazamo halisi ya watanzania. .

Binafsi naamini watu wengi hawana capacity ya kupokea maswala ya msingi, yenye tija na wanakuja kwenye majukwaa mitandaoni kwa ajili ya kupata ahueni na kujifurahisha.
 
Mimi nimechukizwa na mada nyingi za dini zinazoletwa na watu wasio kuwa na Elimu ya dini na kupelekea wasio kuwa na Elimu hiyo kuchangia kwa kupotosha na pia nimechukizwa sana na mada za kudhalilisha ukuu wa Mungu (mfano: Kumfananisha Mungu na Kiumbe nk)
 
Back
Top Bottom