Kwanza niweke bayana mimi ni mshabiki (sio mpenzi) wa Simba Sports Club, mabingwa wa nchi.
Kutokana na kushabikia klabu yetu pendwa, nimejikuta nikamfuatilia (follow) Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Bilionea Mo Dewji.
Namfuatilia Twitter mpaka Instagram.
Baada ya mechi ya Simba na Kaiser Chief, tajiri alitupia pale Twitani kuwa Alikua ana mipango ya kujizawadia Ferrari ama Royce Rolls lakini ameamua kuachana na mipango hiyo baada ya kipigo cha mbwa mwitu pale FNB Soccer City. Akamalizia kusema Simba ni zaidi ya furaha ya binafsi.
Juzi kati akaweka video Instagram akiwa anaimba nyimbo y Tundaman.Video hiyo ilifuatiwa na video nyingine akiwa gym akijenga misuli.
Sikatai Duniani kuna matajiri wengi wenye vituko lakini sio hulka ya Mo Dewji tunayemfahamu.
Sababu ni nini? Kipigo cha Sauzi ama kuna yanayoendelea nyuma ya Pazia.
Tajiri anaonekana ana mawazo mengi. Nini Tatizo?