Nini kimempata Shiza Ramadhani Kichuya?

Nini kimempata Shiza Ramadhani Kichuya?

Alianza kwa kasi ya mbwembwe ndani ya klabu ya Simba,hakujua kuwa kuna wale waliomtangulia walianza na mbwembwe na kushindwa....
Akitokea timu ya Mtibwa Sugar, katika mechi 13 za awali Ligi Kuu alifanikiwa kufunga magoli 9.

Ikumbukwe!
Alianza kwa kasi ya mbwembwe katika Ligi Kuu, baada ya kufumania nyavu mara tisa ndani ya michezo 13 pekee!

Mara ya mwisho winga huyu kufunga goli ni dhidi ya Stand United mwezi wa kumi na moja , mjini Shinyanga, akifunga goli lake kwa mkwaju wa penati.

Tangu mchezo huo imeshapita michezo 11 bila winga huyu kufumania nyavu za timu pinzani, michezo mitano ya Ligi Kuu Bara African Lyon, Tanzania Prisons, JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Ndanda FC hali kadhalika michezo 6 ya kombe la Mapinduzi KVZ, Taifa Jang'ombe, Jang'ombe Boys, URA, Yanga na Azam.

Michezo 11. Hii hijawahi kutokea kwa mchezaji yeyote yule wa Dar es salaam Young Africa SC, mara ya mwisho mfumania nyavu wa Mabingwa watetezi na wa kihistoria wa LigiKuu Bara kucheza mechi nyingi bila kusalimiana na nyavu ilikuwa mwaka 1983- ambapo mshambilizi hatari wa Yanga SC kipindi hiko ''Makumbi Juma'' alicheza michezo 8bila kusalimiana na nyavu.
Mkuu najua unajipooza kwa kujadili ya simba hivi unajua chirwa ana muda gani yanga na kafunga magoli mangapi achia gharama ya usajili wake na mshahara kwa mwezi? Kichuya ni winga na chirwa ni streka unashangaa nini kutofunga? Hata asingefunga goli hata 1 kwetu poa tunachotaka ni msaada wake kwenye timu ndo maana hakai benchi kama chirwa mnaemlipa pesa nyingi bila kazi yoyote.. Ukikaa bila kuiwaza simba unadhani utakufa? Ulileta uchambuzi hewa hapa mwisho ukaukimbia uzi wako leo tena umekuja na kichuya tena duuhh hongera mkuu
 
acha kuamini kuwa kuongoza ligi ndio kuwa bingwa...

nilikuthibitishia hili msimu uliopita.....ila bado hujajifunza.

mu mtegemeaye kwenye kutupia magoli ndio huyoooo..."AMESHA KATA UPEPO".
Wewe ndo ulidhani ukishinda 6 basi ndo bingwa mwisho mliishia kuolewa na mnyama
 
UMEENDA MAZOEZINI? ANATUPIA KAMA KAWA...........wewe ni Yanga unataka kumtoa mchezoni na uchambuz wako umejaa ushirikina (natania) maana kufunga depends on chance na majukumu, halionekani kumsumbua sana mana anashauriwa kisaikolojia
 
Mkuu najua unajipooza kwa kujadili ya simba hivi unajua chirwa ana muda gani yanga na kafunga magoli mangapi achia gharama ya usajili wake na mshahara kwa mwezi? Kichuya ni winga na chirwa ni streka unashangaa nini kutofunga?u

napata shida kujua ubora wako kwenye masuala ya soka!

umesema Chirwa ni Striker? hebu rudia tena?
 
Mkuu najua unajipooza kwa kujadili ya simba hivi unajua chirwa ana muda gani yanga na kafunga magoli.

Hebu jiulize chirwa kacheza mechi ngapi na kasalimiana na nyavu mara ngapi...

wastani wake wa mabao kwa kila mechi aliyocheza ni mkubwa sana kuliko mchezaji wowote wa simba, licha ya kuwa anakosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.cheza mechi

hapa tunazungumzia mchezaji kupata nafasi ya kucheza na kushindwa kutupia kwa kipindi kirefu....

chirwa angepata nafasi kama anazopata Kichura za kucheza mara kwa mara basi hakuna ambaye angemkamata kwa mabao.
 
Hata asingefunga goli hata 1 kwetu poa tunachotaka ni msaada wake kwenye timu ndo maana hakai benchi kama chirwa mnaemlipa pesa nyingi bila kazi yoyote..

Huyo Mavugo mnayemlipa pesa kidogo kuliko Chirwa amempita mabao mangapi Chirwa?
 
Wewe ndo ulidhani ukishinda 6 basi ndo bingwa mwisho mliishia kuolewa na mnyama

nimekuwa nikipiga watu sita sita hata huku kwenye ligi.....

ni kawaida yetu yanga..

nadhani kwenu si kawaida hii...
 
Msimu wa tatu matopeni wanaanza vizuri lakini lazima wapotee mwishoni.
Imeishakuwa kawaida yao!
ni wepesi sana kusahau nina imani kipindi hiki ndicho kitakuwa fundisho kwao....pale watakapoona na kushuhudia Mabingwa watetezi wakibeba ndoo kwa mara nyingine..
 
Mkuu..

Hivi bado tu Potable Alcohol, 4GLTE haijaisha..?
Tangu mpate mabao ya matuta mmekuwa na mihimko na mabao!

sisi tunapiga watu bao 6 tena ndani ya uwanja wa dakika 90. huwa hatungojei kutengewa mipira ya matuta.

hii ni tofauti kubwa sana kati ya klabu ndogo na klabu kubwa!lol
 
Tangu mpate mabao ya matuta mmekuwa na mihimko na mabao!

sisi tunapiga watu bao 6 tena ndani ya uwanja wa dakika 90. huwa hatungojei kutengewa mipira ya matuta.

hii ni tofauti kubwa sana kati ya klabu ndogo na klabu kubwa!lol
Kama ni hivyo mbona nilikutwanga 5-0 ndani ya dak 90, halafu kwani matuta yanatokana na netball au football..?
 
Hapo ndipo nilitegemea uzungumze.....sio mabao ya kutengewa mipira ya penati...

lakini pia usisahau kuwa msimu huo unaifanga yanga bao 5 mwisho wa msimu yeye (yanga sc) akanyanyua NDOO YA LIGI wewe ukabaki na kujidai na mabao 5..

Yanga ndiyo timu ya kwanza kuibamiza Simba kichapo cha paka mwizi cha 5-0 hapo tarehe 01/06/1968


Kama ni hivyo mbona nilikutwanga 5-0 ndani ya dak 90, ?
 
Sie tunapiga 3 kushuka ila point 3 nyie mnapiga 6 na kuendelea na point 7 kila mechi...

usiigize umbumbumbu! najua wafahamu kuwa anaye wawezesha kupiga zaidi ya 3 ameyeyuka kama baiskeli ya barafu...

alafu kama unajua kuwa kila ushindi una alama 3 ,haijalishi wa bao 1,2,3,4,5,6,7,8......cha kushangaza mmekuwa mkishangilia bao 4 za penalty kana kwamba zilikuwa na alama 8.
 
Mavugo anagoli ngapi na amefika lini na chirwa je huu msimu wa pili kafikisha goli 6 tangu aje?
usihangaike kwa kuzunguka chini ya uvungu.

linganisha mechi lukuki alizocheza Mavugo na mechi kadhaa alizo cheza Chirwa.....Licha ya kuwa wote wameingia msimu mmoja.

nani amecheza mechi chache na kutupia mabao lukuki?

jibu swalai kwanza ......

kama hujui hata hili wewe utakuwa mshabiki maandazi.
 
Huyu jamaa ni mnafiki balaa! Mbona Ngoma hachezi kwenye kiwango chake hatuhoji.Kila siku wewe na simba tu! Mwache Kichuya akiwa bora atatufaa siyo kumponda tu humu.
 
Back
Top Bottom