Nini kimepelekea gari za nissan Y62 isifanye vizuri kama nissani y61 na y60

Nini kimepelekea gari za nissan Y62 isifanye vizuri kama nissani y61 na y60

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa magari ya Toyota na Nissan kwa hapa Tanzania. Ambayo kwa kiasi kikubwa yamefanikiwa kuteka soko la magari kwa nchi yetu kwa kiasi kikubwa. Kama kichwa kinavyojieleza toleo la Nissan y62 lina muda sasa lakini sioni watu wakiyakimbilia kama ilivyo tokea kwa matoleo ya Nissan Y61 na Y60. Uzi tayari

NISSAN Y60
View attachment 1667836

NISSAN Y61
View attachment 1667837

NISSAN Y62
View attachment 1667838
Kuhusu sura napenda ya y61 na Y62 ya mwaka jana ambayo ni facelifted!
 
Ni kweli mkuu. Ila kuna kampuni zinafanya kubadilisha pia na zipo zilizobadilishwa baada ya kuuzwa niliharibu kuuliza gharama ikawa kubwa sana
Mkuu gharama za kubadili LHD kwenda RHD inategemea na watu utakao wapa.
Kipindi cha nyuma Airport karibu na High way bar kulikuwa na Wathailand wanafanya hizo kazi za kubadili LHD kwenda RHD na bei Yao nadhani ilikuwa ya kuchekesha maana walikuwa na gari nyingi Sana.
 
Hahahaha. .. Mimi nilitaka ibadilishwe kule kule kwa Biden kuna Garage zinapewaga hiyo kazi kabla ya kuexport ila ikawa bei mlima
 
Back
Top Bottom