Nimepata kutumia Nissan Hardbody NP 300, Toyota Hilux Vigo na Ford Ranger Speed 2.0 l na 3.2 L, Kwenye barabara za mbavu za mbwa Nissan Hardbody ni nzuri kwa maana ni nzito na hai hami kama hizo gari nyingine, ni nzito na inatulia tu. Kuhusu kwenye matumizi ya 4WD Nissan ni full manual na ina nguvu sana 4WD. Ford ranger zina automatic 4WD ina kitufe kama cha kuongeza sauti kwenye radio za zamani unazungusha tu kupata gia ya 4WD, Sema kuhusu Luxury na comfortability ndani ya cabin Ford rangers ni nzuri ikufuatiwa na Toyota Hilux then Nissan.