Securelens
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 316
- 541
Kadri tunavyokaribia uchaguzi idadi ya wapiga debe wa CHADEMA mitandaoni inazidi kupungua siyo tu hapa JF bali hata huko facebook, twitter na sehemu zinginezo. Inaonekana wamepima upepo na kuona maji ya Dkt Magufuli ni masafa marefu. Wachache wanaojitutumua wanachangia kwa unyonge sana na kwa kukata tamaa.
Baadhi wameanza hoja za kujifariji na wengine wameanza kutaka kufanyike kikao cha pamoja cha maridhiano kati ya JPM na Lissu kabla ya matokeo kutangazwa. Mwelekeo wa hoja hizi ni angalau Lissu afikiriwe kupewa cheo. Ndugu zangu tukubali tu ukweli kwamba maji ya JPM ni marefu. Baadhi ya wapiga debe wa CHADEMA mmejitahidi kumnadi mgombea wenu kadri mlivyoweza lakini bahati mbaya mlikosea tangu mwanzo. Hamkuchagua mtu sahihi kwa wakati sahihi.
Mgombea wenu hauziki. Mnajua wenyewe nini watanzania wamesema juu yake na ni kwa nini hakukubalika. Ndiyo siasa ilivyo. Mmejifunza kupitia makosa. Tukutane tena 2025 Mungu akitujalia uzima. Wengi wenu najua tukijaliwa uzima miaka mitano ijayo mtazamo wenu utakuwa umebadilika kabisa na mmekuwa wana CCM ndaki ndaki.
Mtabadilika baada ya kushuhudia makubwa atakayofanya Rais Magufuli kwa Tanzania kwa miaka mitano ijayo. Tuombe uzima. Ushauri wangu, fanyeni uamuzi mgumu, chagueni Dkt Magufuli tarehe 28 Oktoba japo mioyo yenu bado itakuwa migumu, jitahidini tu mmpe kura zenu. Kumpa kura Dkt Magufuli kutawasaidia sana kisaikolojia ndiyo maana wanasema, If you cannot beat them, join them.