tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Katibu wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kanda ya Kaskazini, Charles Odero amesimamishwa na chama hicho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Taarifa ya kusimamishwa kwa Odero imetolewa jana, Julai 30, 2025 na katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totian baada ya kupokea tuhuma za mwenendo usioridhisha wa mwanachama huyo.
Soma pia: Mwanaharakati Odero Charles Odero ajitosa kuwania nafasi ya Uenyekiti CHADEMA Taifa
Odero alikuwa ni miongoni mwa wagombea watatu wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi uliofanyika Januari 21, 2025, wengine wakiwa ni Freeman Mbowe na Tundu Lissu.
Katika uchaguzi huo, Tundu Lissu aliongoza kwa kura 513, Mbowe akapata kura 482 na Odero akiambulia Kura moja huku tatu zikiharibika kati ya kura 999 zilizopigwa siku hiyo.
Source: EATV