Nini kinaendelea kati ya viongozi wa Simba na Manara?

Mr_X

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
1,170
Reaction score
2,335
Kwa ufatiliaji wangu wa mitandao ya kijamii mpaka muda huu katika harusi ya ndugu yetu Manara Jana, sijamuona kuongozi yeyote wa Bodi ya Simba, sio Moo, Hans, Babra wala Rage. Je, hii inamaana gani hawakupewa mialiko au?

Nimemuona hadi GSM pale, nimeona viongozi wengi na mashabiki wengi lialia wa Yanga wanampongeza ila Mo hata kupost insta hajapost, Simba SC nao insta hawajapost.

Je, inamaanisha kuna sintofahamu ndani ya Msimbazi kati ya matajiri na Manara au ni Mimi tu sijapata kuona ila walikuwepo wote?
 
Nasikia kuna "kamgogoro" ka chinichini Tangu Wamkane kwenye ile taaŕifa yake ya kiuchochezi juu ya Mashabiki wa Yanga kuingia kwenye mechi ya Plateau.

Uongozi ulimkana na kusema sio kauli ya klabu kuzuia mashabiki
 
Umesema kweli, nadhani kitu kimoja hata viongozi wanatamani sana wamuondoe Manara, wanaamini sana kwamba manara anajipatia umaarufu kupitia matangazo mbali mbali na wadhamini sema kinachowazingua ni reaction ya mashabiki Manara ameshajijenga saaana hata wakimuondoa hiyo reaction ya mashabiki sijui itakuaje tu.

Nimeongea hivyo kufuatia ile issues ya Kaduguda kwenda WASAFI then akajisafisha peke yake zigo lolote la lawama akamptupia Manara.

Ni mawazo yangu tu lakini.
 
Mkuu alishasema hataki mapicha picha, yeye anataka kazi tu kwahiyo tusubirie ma-anko na ma-anti
[emoji28][emoji28][emoji28]walitakiwa wakampe support jamaa anapambana sana
 
Nasikia kuna "kamgogoro" ka chinichini Tangu Wamkane kwenye ile taaŕifa yake ya kiuchochezi juu ya Mashabiki wa Yanga kuingia kwenye mechi ya Plateau.

Uongozi ulimkana na kusema sio kauli ya klabu kuzuia mashabiki
Kwa hiyo ndo kadhira hadi hajawaalika kwenye mnuso wake
 
Kati ya makundi mengi ya wanadamu moja ya makundi ni ANAEJUA KAKOSEA ILA HAKUBALI WAZI lakini akikaa peke yake moyoni anajua kakosea na anajirekebisha, kundi jingine ni ANAEAMINI yeye huwa hakosei na hata hadi watu anao waamini wakimwambia hapa umekosea Basi wanakuwa maadui zake. Manara yupo kwenye kundi moja wapo hapo
 
Ila kama wewe mleta uzi ni mtoto wa kiume asee hebu jicheki asee aibu naona mimi "eti kwa nini mo, babra nk nk hawajampost".

[emoji3] Viongozi wa simba nadhani bando hawana.
 
Binafsi naamini kuwa uwezo wa mamba ni kwenye maji so ukimtoa nguvu hiyo hata yy Manara mara kadhaa amesema hii kuwa hakuna mtu maarufu kuliko Simba na yanga mfano hata MO GSM na wengine walipata umaarufu kwa kuwa kwao humo wakitoka nani atawajua? So anajua uzito wa brand ya simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…