Nini kinafanya Marekani kuwa imara?

Nini kinafanya Marekani kuwa imara?

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,026
Naomba kudadisi wataalamu mbalimbali watujuze nini kinafanya taifa hili kufanya vizuri katika section zake hadi kupelekea kuwa taifa kubwa na imara. Taifa hili la kibeberu limepiga hatua kubwa sana katika mambo yake, elimu, sanaa, technolojia, jeshi, huduma za kijamii kama afya mpaka dhambi taifa hili linaongoza.

Nini kipo nyuma ya hili taifa la kibeberu, watu wake, geografia, uchawi, mungu au nini. Taifa hili linaongoza kuchukiwa ni vitaifa vidogo maana huvishushia laana zake na kuviacha vikilia. Kinachonichosha ni namna ambayo sector binafsi inanguvu sana huko, mpaka kuwa na makampuni binafsi yanayotengeza silaha.

Pesa yake ina nguvu sana kiasi cha kutumiwa na mataifa mengi katika biashara zao za kimataifa. Na ushamba wangu nimekuta dola ikitumika huko Congo DRC nikabaki najiuliza why? Wataalamu nisaidieni.

Kumekuwa na mjadala kuwa mataifa pinzani yanataka kuongusha matumizi ya hii sarafu, je, wataweza? Je, ni kweli vitaifa dagaa vinalazimishwa kutumia hii sarafu au lah! Wajuvi tusaidieni wenye kupenda kuelimika na kujifunza.
 
HILI NI TAIFA LA KISHETANI.

80 YA MAPATO YANAENDA VATCAN.
 
1.Utawala wa sheria,
2. Kuendeshwa kitaasisi zaidi kuliko one man show,
3.kuwa na wageni wahamiaji kutoka sehemu zote za dunia.
4. Kuheshimu haki za umilikaji mali kibinafsi( private property rights)
5. Uhuru mkubwa
 
Kukandamiza nchi nyingine kimabavu

Ku favor makampuni ya ndani

Kubania makampuni ya nje

Ufirauni
Sio kweli marekani ndo nchi anayoruhusu ufungue kampuni hata bila hata ushirika na raia wa kimarekani, unafungua kampuni marekan na hujawahi hata fika Marekani.

Makampuni ya Kimarekani yamejipanga sana kwenye research ndo maana wanafanya vizuri kampuni kama google we unafikiri ni rais kushindana nao.
 
Kuchapisha makaratasi halafu yanakubalika kama sarafu ya dunia.Siku ikitokea sarafu shindani watayumba sana.
 
Kuna mkono Wa Mungu umempa uwezo , duniani hapa lazima awepo kiongozi , Marekani ameiongoza vizur hii dunia kwa kudumisha uhuru, tofaut na wengine walipewa mamlaka wakaishia kuwa wababe akina Napoleon wa ufaransa , akina Hitler wa ujeruman , walidumbukiza Dunia kwenye machafuko wakanyang'anywa
 
Sio kweli marekani ndo nchi anayoruhusu ufungue kampuni hata bila hata ushirika na raia wa kimarekani, unawefungua kampuni marekan na hujawahi hata fika marekani

Makampuni ya kimarekan yamejipanga sana kwenye research ndo maana wanafanya vizuri kampuni kama google we unafikiri ni rais kushindana nao
Kama ilikuwa tayari kuwapa mtaji makampuni za ndani na kuwabania huawei na ZTE
 
Sio kweli marekani ndo nchi anayoruhusu ufungue kampuni hata bila hata ushirika na raia wa kimarekani, unawefungua kampuni marekan na hujawahi hata fika marekani

Makampuni ya kimarekan yamejipanga sana kwenye research ndo maana wanafanya vizuri kampuni kama google we unafikiri ni rais kushindana nao
Hili swala linanishangaza sana jinsi walivyoweza ku engineer huu mfumo, kinachonidatisha zaidi ni makampuni binafsi kuunda na kutengeneza silaha inawezekanaje.
 
Back
Top Bottom