Nini kinafanya nyumba kuonekana ndefu?

Nkondo 2

Senior Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
181
Reaction score
144
Naomba kuelimishwa hapa, ni nini kinafanya nyumba kuonekana ndefu?

Nimepata utata Sana, baada ya kulinganisha nyumba mbili ambazo zimejengwa kwa kozi 11 hadi lenta lakini moja inaonekana ndefu na nyingine ni fupi, je shida hua ni nini Hadi kuleta utofauti huo?

Napenda kujenga nyumba ndefu ambayo inaleta mwonekano mzuri nje na ndani mzunguko wa hewa n mkubwa je natakiwa nizingatie mambo gani?
 
Oooh Sawa mkuu umeniongezea uelewa, nashukuru
 
Kama sio hivyo inawezekana ardhi ilipojengwa hiyo nyumba ina rutuba sana hivyo hiyo nyumba inaendelea kukuwa.
 
Urefu wa tofali na mortar baina ya course moja na nyingine.
Mortar ni ule udongo unaowekwa chini kabla ya tofali kulazwa , kama fundi hayupo makini anaweza akaweka layer kubwa ya mortar , hii huwa inasababisha nyumba kuonekana ndefu pia
 
Idadi ya kozi za msingi. Wengine wanaweka kozi 3, wengine hadi 7 lazima uione tofauti.
 
Noted
 
Urefu wa tofali na mortar baina ya course moja na nyingine.
Mortar ni ule udongo unaowekwa chini kabla ya tofali kulazwa , kama fundi hayupo makini anaweza akaweka layer kubwa ya mortar , hii huwa inasababisha nyumba kuonekana ndefu pia
Umeeleweka mkuu, shukran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…