Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Siku zote kinachoinua nyumba ni msingi.Naomba kuelimishwa hapa, ni nini kinafanya nyumba kuonekana ndefu?
Nimepata utata Sana, baada ya kulinganisha nyumba mbili ambazo zimejengwa kwa kozi 11 hadi lenta lakini moja inaonekana ndefu na nyingine ni fupi, je shida hua ni nini Hadi kuleta utofauti huo?
Napenda kujenga nyumba ndefu ambayo inaleta mwonekano mzuri nje na ndani mzunguko wa hewa n mkubwa je natakiwa nizingatie mambo gani?
Inapendekezwa msingi usiwe chini ya 60cm hapa ni sawa na ngazi 4.
Mimk binafsi hupendelea 75cm hii ni ngazi 5.
Ngazi 4 hadi barazani then kuingia ndani ya nyumba toka barazani ni ngazi moja jumla zinakuwa 5 hadi kuingia sebuleni.
Walling....boma linakuwa na laini 11 hadi 12 hii hutegemea na ukubwa wa nyumba.
Hapo kwa vyovyote nyumba itakuwa juu baada ya kuezeka ambapo kutakuwa na laini 3 hadi 4 juu ya lenta.
Gebo ya bati nitagawa kwa 2.2 hadi 2.3.
Hapo nyumba itakuwa bomba sana.
Kugawa kwa 2 mara nyingi huwa hazivutii.
Note; epuka nyumba yenye msingi mfupi yaani unaingia na baiskeli bila kikwazo huwa hazipendezi na ziko hatarini kuingiza maji ndefu.