Nini kinafanya nyumba kuonekana ndefu?

Nini kinafanya nyumba kuonekana ndefu?

Naomba kuelimishwa hapa, ni nini kinafanya nyumba kuonekana ndefu?

Nimepata utata Sana, baada ya kulinganisha nyumba mbili ambazo zimejengwa kwa kozi 11 hadi lenta lakini moja inaonekana ndefu na nyingine ni fupi, je shida hua ni nini Hadi kuleta utofauti huo?

Napenda kujenga nyumba ndefu ambayo inaleta mwonekano mzuri nje na ndani mzunguko wa hewa n mkubwa je natakiwa nizingatie mambo gani?
Siku zote kinachoinua nyumba ni msingi.
Inapendekezwa msingi usiwe chini ya 60cm hapa ni sawa na ngazi 4.
Mimk binafsi hupendelea 75cm hii ni ngazi 5.

Ngazi 4 hadi barazani then kuingia ndani ya nyumba toka barazani ni ngazi moja jumla zinakuwa 5 hadi kuingia sebuleni.

Walling....boma linakuwa na laini 11 hadi 12 hii hutegemea na ukubwa wa nyumba.
Hapo kwa vyovyote nyumba itakuwa juu baada ya kuezeka ambapo kutakuwa na laini 3 hadi 4 juu ya lenta.

Gebo ya bati nitagawa kwa 2.2 hadi 2.3.
Hapo nyumba itakuwa bomba sana.

Kugawa kwa 2 mara nyingi huwa hazivutii.

Note; epuka nyumba yenye msingi mfupi yaani unaingia na baiskeli bila kikwazo huwa hazipendezi na ziko hatarini kuingiza maji ndefu.
 
Ni paa ile senta canch anaweka labda cm 270 au 300 .
Au inategemea baada ya linta juu linta tena anapitisha kozi 3 za tofali.
Na kama ndani umeona chumba kirefu ni ile blandering inapigwa juu kabisa (nchi 3 kutoka juu mwisho wa tofali mbao inapita)

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa unaweka 270 au 300cm kwa kigezo gani?
Kuinuka kwa paa huwa na sababu hasa span ya ukuta.
Ili upate hiyo height ya 270 hadi 300 lazima upana wa nyumba uzidi 7m.

Mfano; upana wa nyumba uwe 700m gawa kwa 2.3=318cm

Hivi ndivyo height za gable hupatikana mkuu

Kuna fundi anapuyanga kunyanyua nyumba bila kufuata kanuni ni uharibifu wa nyumba
 
kuna mambo kadhaaa.

1. urefu wa msingi (ni sahihi)

2. idadi ya kozi za tofali mfano. kozi nne alafu lenta ndogo kuzia nyufa za madirisha then kozi 9 lenta tena then kozi tatu za mwisho.

3. urefu wa paa (sio sahihi sana).

NB. UREFU WA PAAA UKIZIDI UREFU WA UKUTA NI KITUKO, UKUTA UKIZIDI PAAA NI KITUKO KINGINE

SO.... lazima kuwe na uwiano kati ya ukuta na paa.
Ungeeleza kitaalam basi namna ya kupata urefu wa ukuta na heigt ya gable
 
Kuna nyumba paa refu kuliko urefu wa kuta. Sipendi kabisa nyumba za paa ndefu.
Naam hizo huwa ujenzi usiozingatia kanuni.
Michoro iliyochorwa na mtaalam huwa ina vipimo vyote kuanzia;

1. Urefu wa msingi
2. Urefu wa ukuta kwenda lenta.
3. Urefu baada ya lenta.
4. Urefu wa gebo/gable

Hii tunaita section;

Angalia mchoro hapo chini.

20220430_133520.jpg
 
Paa linapaswa kuwa nusu ya urefu wa ukuta.
Sio sahihi mkuu.
Kuna namba maalum ya kugawa paa mfano ukitaka paa lako liwe 45° utagawa upana wa nyumba kwa 2. Hii ni kwa majengo kama kanisa nk.
Nyumba nyingi tunagawa kwa 2.2 hadi 3.

Hii ni kutokana na oendekezo la mtu lakini isiwe chini ya 2 utakuwa umeharibu nyumba
 
Sio sahihi mkuu.
Kuna namba maalum ya kugawa paa mfano ukitaka paa lako liwe 45° utagawa upana wa nyumba kwa 2. Hii ni kwa majengo kama kanisa nk.
Nyumba nyingi tunagawa kwa 2.2 hadi 3.

Hii ni kutokana na oendekezo la mtu lakini isiwe chini ya 2 utakuwa umeharibu nyumba
Hapo wewe unakokotoa pitch size? Mimi nimeegemea kimuonekano tu. Pia nafikiri akili yangu ilikuwa upande wa gabled/pitched/peaked roof style.

Mf. nyumba yenye urefu wa ukuta wa futi 10 na upana wa futi 20 inaweza kuvutia ikiwa na paa lenye futi 10? (pitch size: 12/12=45° )

Nilichomaanisha sasa; Nyumba hiyo hiyo yenye urefu wa ukuta wa futi 10 na upana wa futi 20 inaweza kuvutia kimuonekano ikiwa na paa lenye urefu wa futi 5 yaani pitch size yake iwe 6/12 = 26.57°

Jinsi nilivyoipata hiyo pitch size hapo juu; Nimechukua upana wa nyumba futi 20 gawa kwa 2 nikapata 10 zikazidisha mara 6 gawa kwa 12 kupata hizo futi 5 yaani kwa kila inch 6 paa litapanda kwa inch 12.
 
Msingi kuwa na kozi 3 ni below std.
Inapaswa kuw 60cm ambayo ni kozi 4 na kuendelea.
Hesabu kama hizo alikuwa ananipigia fundi baada ya kukuta keshaanza kupigilia mbao.

Paa nililiona ni refu sana. Nilimwambia ashushe mpaka urefu ninaoupenda halafu ndo aanze kupiga hesabu anayoitaka yeye.

Baada ya kuishusha ndo ikawa hivi.
View attachment 2206475
 
Back
Top Bottom