Monstgala
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 1,079
- 1,036
Nikiwa napitia topic kadhaa katika jukwaa hili nikakutana na topic moja inayohusu roho (soul) kwamba iko katika kiungo gani katika mwili wa binadamu akiuliza bwana Petro E. Mselewa . Katika kusoma maoni ya wachangiaji ambayo ni ya kufikirisha sana nikajikuta katika swali la nini kinafanya binadamu awe binadamu au kwa kukuhusisha zaidi unaweza sema nini kinafanya wewe uwe wewe katika mwili wako au chochote kinachousiana nawe. Unaweza ukaona kwamba ni rahisi kujibu swali hilo lakini ukitulia zaidi na kutafakari nini ni wewe zaidi katika mwili wako kwa kuhusisha scenarios mbalimbali zinazowezekana au zinaleta maana kisaikolojia basi utakuta swali hili si rahisi lakini pia linajenga sana ufahamu wa mimi au wewe kama binadamu au mtu ni nini? hasa.
Utaona kwamba mimi nataka kujadili zaidi kuhusu wewe kama binadamu ni nini? Na sio kujua roho iko wapi hivyo mada hii inajengwa kutaka kuelewa nafasi za kila kitu ambacho sisi tunaona ndio utu au ubinadamu au nafsi zetu.
Nimefanya utafiti, nimetafakari na nimesoma mambo mengi na theories kadhaa kuhusu suala hili hivyo niko tayari kujadili na kufahamishana kwa kina mambo mazito na ya msingi sana ambayo hakika yatakufanya uelewe zaidi wewe ni nini ingawa unaweza kuwa ulikuwa unachukulia kirahisi concept hii.
Twende pamoja. Nini kinafanya wewe uwe wewe? Ubongo? Mwili? Roho? Ufahamu wako? au nini unachojua wewe?
Mwili (Kiwiliwili)
Mkuu Eiyer, shukrani. Unasema binadamu ni muunganiko wa mwili na roho, sawa ni mtazamo mmoja wapo lakini kitu cha ziada sana katika kutafakari hapa si suala la "binadamu ni nini" bali ni kipi hasa kinafanya mtu fulani ajione/ajitambue/ajihisi/ejielewe etc., kwamba ni yeye katika mjumuisho wote wa vitu vinavyoonekana na visiivyoonekana lakini vinavyoelezewa kama sehemu ya mtu.
Umetaja mwili + roho lakini kwa fikra thabiti zilizowazi za kinadharia zinaweza kutuonesha jinsi mwili wa mtu usivyo centre kwa kuwa ukipewa mwili wa mtu mwingine bado ule u-wewe wako utakuwa haukuondoka na mwili wako wa mwanzo. Ni fikra ngumu kidogo lakini zinaelezeka na zinaweza kuwa conceived na kukubalika. Hili linaondoa hoja yako kwamba lazima mwili wako na roho yako viwe vile vile ulivyozaliwa navyo ili uwe wewe. Kivipi? Nitaelezea kidogo kuhusu mwili.
Tunajua kwamba kuna maendeleo makubwa katika fani ya utabibu ambapo suala la kubadilishwa viungo vya mwili kwa kuwekewa vya mtu mwingine (organ transplants) si ajabu wala si geni tena. Viungo muhimu kabisa katika mwili wa binadamu kama moyo, mapafu, figo, ini, ngozi na vinginevyo vinapandikizwa katika mwili wa mtu mwingine na kufanya kazi kama kawaida. Pia majimaji katika mwili kama damu, maji etc pia yanaweza kubadilishwa na kuwekwa mengine na mtu huyu akaishi. Mwili mzima (kiwiliwili) kubadilishwa ni jambo lililo njiani na ni katika miaka miwili jambo hili linatarajiwa kufanyika katika utabibu kama litafikiwa kipitishwa na jamii. Linapingwa sana jambo hili lakini tayari kuna neurological surgeons na scientists wameweka wazi tafiti zao na majaribio ya uwezekano na jinsi ya kufanya operation hizi za ajabu kidogo.
Kwa hiyo kitu hiki kama kimefikia mahali hapo basi hatuna budi kudadavua katika fikra kwamba katika watu wawili wanaofanyiwa operation hii (1) Anayetoa kiwili-wili (mwili mpaka shingoni) na (2) Anayetoa kichwa, ni nani hasa atakuwa ni yule mtu baada ya operation hii. Kwa kuwapa identity watu hawa tuseme bondia na mwanasoka wanafanyiwa operation hii, kiwili-wili cha bondia na kichwa cha mwanasoka, nani atakuwa huyu mtu baada ya operation? majibu ya wengi yanaweza kuwa labda mwana soka kwa kuwa ndiye mwenye kichwa.
Lakini kabla hatujaanza kudhani tumemaliza mtihani huu twende mbele kidogo. Ikiwa operation hii itawezekana basi pia mbadilishano wa sehemu hizi kuu za mwili zitakuwa zimewezekana (Mfano kichwa na kiwiliwili). Hivyo Bondia na mwanasoka waki-swap vichwa, nani haswa atakuwa bondia na nani mwanasoka baada ya full body transplant operations hizi? Kwa maana hapa tutakuwa na kichwa cha mwanasoka chenye mwili wa bondia wenye mikono iliyokomaa kwa kutupa masumbwi na pia kichwa cha bondia chenye mwili wa mwanasoka wenye miguu yenye vigimbi na tayari kupiga chenga na dana-dana.
Utambulisho wa asili wa watu hawa au ule utu wao unasimamia wapi kwenye vichwa au miili yao? Kama ni vichwa basi hoja yako ya mwili tutakuwa tumeipunguza mpaka kubakiza kichwa na kama ni kiwiliwili basi hoja yako itakuwa imeondolewa kichwa kama sehemu muhimu ya wewe ni nani. Hivyo je unaweza kusema ni kichwa na roho ndio ndio kinamfanya mtu awe yeye?
Kichwa
Lakini kichwa pia si kiungo ambacho hakina organs zinazoweza kubadilishwa na katika nadharia tayari viungo na sehemu muhimu kichwani vinaweza kuondolewa na kupandikizwa vingine. Pua, macho, masikio, ulimi etc ni baadhi ya viungo vinavyoweza kuwekewa mbadala kinadharia na tafiti halisi ziko tamati wakati baadhi ya viungo tayari sehemu zake kuu zinaweza kuondolewa na kupandikizwa za mtu mwingine mfano cornea transplants ambapo corneal ya jicho iliyoathiriwa inatolewa na kupandikizwa ya mtu mwingine (organ donor). Hii ni wazi baada ya muda si mrefu jicho zima litawezekana kupandikizwa la mtu mwingine na pia viungo vingine kichwani. Unaweza kusema basi vyote zi muhimu katika kubeba ule "u-mimi na u-wewe wa mtu" kama ubongo lakini nitaelezea thought experiments zenye kuuweka kwenye mizani na kusambaratisha hoja ya ubongo kama ndiyo sehemu iliyo utu au centre ya mimi au wewe ni nini.
Ubongo
Mkuu sajumo , nimevutiwa na mfano wako wa watoto wawili katika familia moja waliolelewa na wazazi wale wale. Tangu mtoto ana-develop ubongo tumboni kwa mama yake tayari ubongo ule unaanza kufanya kazi kubwa. Ukiachilia mbali upande wa ubongo unaohusika na kuendesha mwili mfano mapigo ya moyo, kubalance joto na kupumua, pia upande mwingine wa ubongo hasa ubongo wa mbele unaendelea kuzalisha neurons ambazo hizi hukusanya information nyingi sana kwa ajili kiumbe kuzitumia katika mazingira yake. Information zisizo na umuhimu hufutwa au hufutika kwa kukosa kurudiwa-rudiwa lakini baadhi ya information hujikita na kuwa na nguvu zaidi. Utaona mtoto aliyezaliwa siku chache anakuwa anaitambua sauti ya mama yake na kutulia pale anapoisikia hii ina maana anaweza kuwa kaisikia na kuizoea sauti hii ambayo tayari imejikita katika kumbukumbu ndani ya ubongo wake.
Pamoja na mazingira kuchangia uelewa na character ya mtu kwa kiasi kikubwa lakini si kigezo pekee. Mfano kuna genes ambazo hizi ni codes zenye nguvu ambazo tayari mtoto anazirithi kutoka kwa wazazi wake wawili nusu-nusu. Codes hizi (DNA) zina information muhimu ambazo ndizo huendesha mpangilio mzima wa mwili uweje na pia ubongo utafuata codes hizi za msingi katika ku-develop lakini kwa yale ambayo mtu atajifunza itakuwa ni matokeo ya mazingira kwa kiasi kikubwa.
Lakini pia viumbe vina uwigo mpana wa kufanya uchaguzi, kipi utunze katika ubongo na kipi usitunze. Katika hili hata mapacha wa kufanana (identity twins) waliokulia katika mazingira ya aina moja na wanaofanya kila kitu kwa pamoja bado hawawezi kuwa sawa kutokana na mfumo wa ubongo unapelekea uchaguzi binafsi. Mfano kwa dakika moja tu mapacha hawa wameletewa chai katika vikombe vinavyofanana. Ingawa kunywa kikombe cha chai kwa kawaida ni kama kitu kisicho kisicho na complication lakini ubongo wa kila mmoja katika tendo hili la kunywa chai utakuwa na ishara za umeme zaidi ya bilioni na baadhi zitatunzwa na nyingine zita-decay kwa muda mfupi.
Katika ishara hizi kila moja ni choice na hivyo mwisho wa siku experience ya chai katika kikombe inaweza kuelezewa kwa namna tofauti sana na mapacha hawa na hii ni kwa maelezo tu lakini implicit knowledge inayokuwa imetunzwa ubongoni itatofautiana kwa asilimia kubwa na pia kuna ishara zitakazofanana. Information ipi itunzwe na ipi ifutwe itategemea vigezo kadhaa pia ikiwemo previous experience ambayo hii ita-link ya yale uliyowahi kuyatunza mwanzo (mfano ladha, harufu etc) na pia mara ngapi ishara hizi zitajirudia au kuwa na kitu kingine cha kushikilizia ili iweze kudumu.
Ufahamu
Mkuu IGWE, Ufahamu wako kuhusu wewe ni sehemu moja ya jibu kwa kuanzia lakini ukifikiri zaidi unaweza kuona jinsi "ufahamu wako" pia unavyopwaya katika kukufanya ndio iwe sehemu kuu ya wewe ni nini.
Ufahamu unaangukia katika Data theory, kwamba yale uliyoyafahamu na kuyatunza katika ubongo wako kama kumbukumbu na uelewa wa kila kitu kuhusu wewe na yanayokuzunguka ndio sehemu halisi inayofanya wewe uwe wewe. Mfano mawazo, fikra, ndoto, emotions, personality, kumbukumbu, matumaini, hofu na mambo mengine yanayotunzwa katika ubongo haya yote ni data fulani katika maisha yako na hivyo ni center ya mtu.
Kwa nadharia ikitokea sehemu ya mwili wa mtu A akapewa mtu mwingine mtu B (katika surgical operations) lakini ubongo ukabaki na ukawekwa kwa mwili wa mtu B, basi tunaweza kusema katika mbadilishano huu Mtu A bado ni ule ubongo wake na data zake na mtu B ni ule ubongo wake na data zake pia.
Lakini tukienda mbali kidogo kinadharia, kwamba mtu A na mtu B wafanyiwe mbadilishano wa data peke yake bila kuchukua ubongo au sehemu ya mwili, yani mtu A awekewe kumbukumbu na experience (ufahamu) za mtu B na vice-versa kwa mtu B. Basi ufahamu huu ndio utakuwa utambulisho wa mtu A na mtu B ni yupi hata kama ni katika miili tofauti na ile waliyozaliwa nayo!!
Hivyo basi ufahamu (kumbukumbu, experience etc) unabeba maana kubwa ya nini hasa ni sehemu inayofanya mtu fulani awe yeye.
Ugumu unakuja pale tunapoanza kufikiri kwa kufanya majaribio ya kinadharia. Bernard Williams katika tourture test aliiweka pabaya hii concept kwamba ufahamu ndio haswa sehemu kuu ya mtu. Mfilosofia huyu anasema katika situation ya kwanza ikiwa mtu A na mtu B baada ya kufanyiwa mbadilishano wa data kwenye bongo zao alafu wakaamshwa, kila mmoja atajikuta katika mwili wa mwenzie. Katika hamaki hii mtu B anaona mtu A ni yeye kwa kuwa mwili ule anaujua lakini akili yake iko katika mwili mwingine. Sasa mtu B akiulizwa kati ya ninyi wawili mmoja wenu atapitia maumivu makali sana ya mateso chagua awe nani? (mfano), Ni nini jibu la mtu huyu? Kwa wengi logical answer ni awe mwenzangu yule tu (Mtu A). Hii ni kwa kuwa mwili mtu B aliomo ndani yake katika wakati huo ndio haswa unahisi kuulinda. Kwamba popote pale ufahamu wangu unapoenda na mimi ndipo nipo. Jibu litabaki hivyo hata kama ukiambiwa kwamba katika mateso hayo baadae kumbukumbu zile zitafutwa na hakuna kati ya mtu A au B atakayekumbuka ni nani aliteswa.
Kuna majaribio mengine kadhaa pia ya kinadharia lakini labda kwanza unaona hii iko sawa?
Karibuni wanajukwaa.

Last edited by a moderator: